Sarafu mpya yatolewa leo na BOT

Sarafu mpya yatolewa leo na BOT

JK tumsifu kwa lipi alilotuachia zaidi ya kushusha thamani hela ya Tanzania ni aibu nchi zinapiga hatua Tz inamongonyoka
 
Ukiona noti zinabadilishwa kuwa sarafu,ujue fedha inashuka thamani
 
Hivi naomba kuuliza sababu iliyosababisha hadi thamani ya fedha zetu kushuka??Hivi kuna sababu gani ya msingi ambayo inapelekea taasisi za fedha kuweka hesabu ambazo hazieleweki??
Mfano..unaangalia balance benki unakuta kuna Tsh.345471.93 wakati sarafu za Tsh.5;10;20 na senti hazifanyi kazi??Hivi nikifika benki niombe kuchukua fedha zote watanipa na masalia yangu yote??Hayo masalio huwa yanaenda wapi??Hivi sisi Wata
nzania huwa tunaibiwa bila kujijua??
Hizo sarafu kwanini zimefutwa??
Wizara ya fedha na BOT waliangalie swala hili kwa umakini mkubwa..
 
Watanzania wengi hawaelewi nini
maana ya kutengeneza sarufu kwa
pesa iliokuwa note. Hili ni anguko la
thamani ya fedha. Kwa maana
nyingine miatano itaungana na
sarafu nyingine kwenda kununua pipi
na mafungu ya nyanya. Haitakuwepo
tena kwenye mauzo na manunuzi.
mfno kama bati linauzwa 16500
linakwenda kuuzwa 17000
kuondokana na usumbufu wa
sarafu. Sasa wajinga wa ccm hapa
wanashangilia na kumpongeza
Mwigulu eti uchumi unakua, Uchumi
unaokuwa unajireflect kwe maintain
the status qou ya pesa yenu. Uchumi
wowote unaobadili note kuwa sarafu
ni uchumi ambao sekta yake fedha
inayumba. Hii inamaana vitu
vimepanda bei kiasi 500 miatano
imekuwa ya kununua bidhaa za chini
sana. Pia gharama ya kuitengeneza
mia tano ya note ni kubwa kuliko
thamani yake. Wananchi watanzania
ni watu wa mia tano yaani hali zao
kiuchumi ni mbaya kiasi mia tano ni
pesa inashikwa na watu wengi sana
hivyo kuchakaa zaidi.
 
Kuna mtu kanifundisha uchumi kidogo, nikaona tushare kwa pamoja!
KWA TREND HII YA BOT; UCHUMI WA TANZANIA ULALE MAHALI PEMA PEPONI.

Siungi mkono hoja ya Benki kuu (BOT) kufuta noti ya Sh.500/= na kuifanya sarafu. Huu ni wendawazimu mkubwa katika sekta ya uchumi "the most unpleasant economic decision" kwa sababu zifuatazo;

MOSI; fedha yoyote inapobadilishwa kuwa sarafu kutoka noti ni kuishusha thamani. Hii ni kwa sababu kiuchumi inabadilika matumizi na kuanza kutumika zaidi ktk sekta ya uchumi mdogo km wa wauza njugu mtaani, mama lishe, na maeneo mengine yasiyozalisha sana kiuchumi (less productive sector).

Maeneo yenye uzalishaji mkubwa (lead productive sector) yatashindwa kuitumia fedha hii kwa kuwa tu ni ya sarafu. Kw mfano kuanzia sasa haitakua rahisi kukuta sarafu hizi za 500/= maeneo kama Airport, Migodini au Supermarket.

Hiki ni kiashiria cha kushuka kwa thamani kwa fedha hiyo. (Indicator for currency devaluation).

Hivi hatujiulizi kwanini Marekani hadi dollar moja ni ya noti sisi 500/= tunaweka sarafu?? Dollar moja ina single digit lakini ipo kwenye noti, sisi tunalazimisha kuweka 500 kwny sarafu wakati ina tripple digit. Tunaforce Galloping inflation.

PILI; unapotengeneza sarafu ya pesa kubwa ina maana sarafu zinapotea na kujiondoa ktk mzunguko wa fedha. So tutegemee siku si nyingi sarafu za sh.100/= na sh 200/= hazitakuwepo tena mtaani.

Ikifikia hatua hii ujue nchi imeanza kuyumba kiuchumi na mfumko wa bei umevuka kiwango cha kawaida (extention from Moderate inflation to Galloping inflation).

Wenzetu Kenya hadi sarafu ya sh.10 inatumika. Ukienda Nairobi, Mombasa au maeneo mengine ya Kenya utata watoto wakinunua madafu, ice cream au matunda kwa sh.10.

Hapa kwetu sarafu ya sh.10 ilikufa na Nyerere. Ya sh.5 ikaenda na Sokoine. Ya sh.20 na 50 zimemfuata Kawawa. Sasa benki kuu wanalazimisha sarafu ya sh.100 na ya sh.200 zikamfuate Karume mahali pema peponi. Noti ya sh.1,000/= nayo inakaribia kwenda ahera maana BOT wameleta sarafu ya sh.1,500/=.

TATU; BOT kuwa wametoa hoja mufilisi kuwa wamefuta noti ya Sh.500/= na kuireplace kwa sarafu baada ya kugundua noti hiyo inachakaa haraka sn na inadumu kwa muda mfupi mno kwenye mzunguko.

Hoja hii ni mufilisi kwa sababu solution ya noti kuchakaa mapema si kureplace sarafu bali ni kuimarisha noti hiyo kwa kuitengeneza kwa material imara zaidi.

Hivi noti ya 10,000/= nayo ikichakaa mapema BOT wataleta sarafu instead?? Huu ni wendawazimu.

Mojawapo ya sifa za fedha imara ni uwezo wa kukaa kwny mzunguko muda mrefu (durability). Sasa fedha inapopoteza durability dawa sio kubadili muundo wake (changing of currency format is not a solution for impermanency)

Lakini hata hivyo BOT wameonesha hawakufanya utafiti wa kina kabla ya kuleta sarafu ya 500/=. Wanasema zinachakaa haraka ukilinganisha na noti nyingine. Hii ni hoja dhaifu sana kutolewa na mtu anayejiita Profesa wa uchumi Benno Ndullu.

Yani Profesa Ndulu anataka noti ya 500/= na ya 10,000/= zidumu kwenye mzunguko kwa muda sawa?? Yani 10,000/= ikidumu miaka miwili, 500/= nayo idumu miaka miwili. Bila shaka hapo ndo ataona noti ya 500/= haichakai haraka.

Hii ni "akili ndogo kujaribu kutawala akili kubwa". Noti ya 500 haiwezi kulinganishwa na noti nyingine kwenye mzunguko kwa sababu ina frequent circulation. Yani ktk uchumi noti yenye thamani ndogo huwa inazunguka zaidi kuliko ya thamani kubwa.

Hivyo noti ya 500/= inaweza kupita kwenye mikono ya watu 2000 ndani ya mwezi mmoja wakati ile ya 10,000/= imepita kwenye mikono 20 tu kwa mwezi.

Hii ni kwa sababu mzunguko wa noti hizi hutegemea matumizi. Ya 500/= itazunguka kwny daladala, wauza magazeti, vijiwe vya kahawa etc, wakati ile ya 10,000/= itazunguka Supermarket, Airport, hoteli kubwakubwa etc.

Hivyo ni dhahiri kuwa noti ya 500/= itaanza kuchakaa mapema kuliko noti ya 10,000/= au ya 5,000/= au noti nyinhine kubwa. Sasa cha ajabu Profesa Beno Ndulu hajui hili na badala yake ameona solution ni kuleta sarafu. Aibu gani hii kwa mtu anayejiita Profesa wa uchumi kushindwa kujua vitu common km hivi ambavyo hata muuza machungwa wa Keko anavijua??
 
Juzi kati banki kuu ya tanzania imetangaza ubadilishwaji wa noti ya 500 na kuwa sarafu,sababu niliyoimaster kwa haraka ni kuwa noti za mia tano zinawahi kuchakaa mana zipo katika mzunguko mkubwa wa watu kana kwamba hazirudi banki kuu kwa uharaka,hoja yangu ni kutaka kuuliza wana jf mzunguko huu wa noti mpaka inachakaa mikono mwa watu unahashiria nini katika taifa,je ni kukuwa kwa uchumi au kudhorota kwa uchumi?mana buku kumi haina nafasi katika mikono ya watu wengine ila jero mamaaaa,na je bot mmekaa vikao vingapi katika kujadili ubadilishwaji huu mana mmekula tena pesa za umma kama sitting allowances,huku noti hiyo haina muda toka muibadili!! Na kulikuwa na sababu gani ya kubadili ile noti
 
Mkuu Sio Kuchakaa Kwa Kifupi Noti Ya 500 Ni Mbovu Mbona 1000 Haichakai Haraka Na Wakati Nayo Ina Mzunguko Mkubwa.
 
unafikiri nini kifanyike ili thamani ya shiringi ya tz isishuke ,,
 
:spy:WATUELEZE MKAKATI WA KUINUA SHILLING YETU:hand: SIO KUTUTENGEZEA MAHELA OVYO. WANATAKA KUPIGA CHENGA JUKUMU MUHIMU enheee..:spy:
 
Back
Top Bottom