SI KWELI Sanamu ya Lissu yazinduliwa Arusha

SI KWELI Sanamu ya Lissu yazinduliwa Arusha

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Au hii habari ni fake news?

1757665961240.png
 
Tunachokijua
Tundu Lissu ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye kwa sasa yupo gerezani kutokana na kesi inayomkabili ya uhaini na uchochochezi.

Madai

Kuanzia Septemba 08, 2025 kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ikionesha sanamu la Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu na ikielezwa kuwa limetengenezwa na kuzinduliwa huko Arusha.

Uhalisia wa madai hayo

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa Taarifa hiyo si ya kweli.

Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao na utafutaji wa maneno muhimu unabainisha kuwa hakuna chanzo chochote cha kuaminika kilichochapisha taarifa kuwa sanamu la Tundu Lissu limetengenezwa na kuzinduliwa huko Arusha.

Baadhi ya watu maarufu na makada wa CHADEMA walioitumia picha hiyo hawakuambatanisha ujumbe kueleza kuwa ni kweli sanamu hilo lipo Arusha ama vinginevyo na badala yake wamekuwa wakiambatanisha jumbe tofauti. Mathalani Tazama hapa

Ufuatiliaji zaidi kwa kutumia nyenzo za kidigitali ikiwemo za kubaini iwapo maudhui yametengenezwa kwa Akili Unde, JamiiCheck imebaini kuwa picha hiyo hiyo ina uwezekano mkubwa wa kuwa imetengenezwa kwa Akili Unde.
1757665355402-png.3470306
Back
Top Bottom