Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,539
- 4,854
SANAA YA ARUSHA.
1)Mwanzo ilianza vyema,kama nuru ikawaka
Tulionajambo jema,wengi wakajumuika
Lakini bado mapema,kama taa yazimika
Hi sanaa ya Arusha,kama dira yapoteza.
2)Wasanii wa filamu,ujumbe utasikika
Japo hali yenu ngumu,msije kukasirika
Nisemacho siyo sumu,hili linatambulika
Hi sanaa ya Arusha,kama inakuwa janga.
3)Agesta ilo shamiri,leo tena iko wapi ?
Nauliza kishairi,tuloyafanya mangapi ?
Ama tulitenda shari,ama tulikosa wapi ?
Hi sanaa ya Arusha,kama haieleweki.
4)Aizagi msomeki,hivi mmefia wapi ?
Ama mlokosa kiki,sasa mfungo wa pipi
Mmekufa kama nyuki,sema hili ama lipi ?
Hi sanaa ya Arusha,kama ni pata potea.
5)ililetwa tidifaa,sanaa kuunganisha
Uwanjani tulijaa,kwa furaha na bashasha
Leo nayo yapotea,wachache wanaifisha
Hi sanaa ya Arusha,kama haina wenyewe.
6)kila mara mageuzi,vyongozi watimuliwa
Yakitajwa wazi wazi,yapo yanayoibiwa
Nani alivunja nazi,ni bora tungeambiwa
Hi sanaa ya arusha,kama ina matapeli.
7)Leo huyu kesho yule,
Digega akaja Fredi
Au twendeni kule,tukaogee magadi
Mkosi upite vile,sana iwe yetu jadi
Hi sanaa ya Arusha,kama mpira wa kona.
8)Chalo baada ya chinga,akashika usukani
Gizani bila ya mwanga,gari likenda shimoni
Magesa akajifunga,kimya asiseme nini
Hi sanaa ya Arusha,kama vile inakufa.
9)Kisa pesa nauliza,ndo kinachotuangusha ?
Wengine kinawaliza,chozi chini wadondosha
Ndoto mnazimaliza,na moto mnaviwasha
Hi sanaa ya Arusha,kama mzoga wa paka.
10)Ningelikuwa rahisi,hatua ningechukua
Ngumu isiyo rahisi,hukumu ningeamua
Vyovyote mtavyohisi,ujumbe wawafikia.
Hi sanaa ya Arusha,wapi inaelekea.
Shairi=SANAA YA ARUSHA
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha
+255624010170
iddyallyninga@gmail.com
[HASHTAG]#mimimalenga[/HASHTAG]
1)Mwanzo ilianza vyema,kama nuru ikawaka
Tulionajambo jema,wengi wakajumuika
Lakini bado mapema,kama taa yazimika
Hi sanaa ya Arusha,kama dira yapoteza.
2)Wasanii wa filamu,ujumbe utasikika
Japo hali yenu ngumu,msije kukasirika
Nisemacho siyo sumu,hili linatambulika
Hi sanaa ya Arusha,kama inakuwa janga.
3)Agesta ilo shamiri,leo tena iko wapi ?
Nauliza kishairi,tuloyafanya mangapi ?
Ama tulitenda shari,ama tulikosa wapi ?
Hi sanaa ya Arusha,kama haieleweki.
4)Aizagi msomeki,hivi mmefia wapi ?
Ama mlokosa kiki,sasa mfungo wa pipi
Mmekufa kama nyuki,sema hili ama lipi ?
Hi sanaa ya Arusha,kama ni pata potea.
5)ililetwa tidifaa,sanaa kuunganisha
Uwanjani tulijaa,kwa furaha na bashasha
Leo nayo yapotea,wachache wanaifisha
Hi sanaa ya Arusha,kama haina wenyewe.
6)kila mara mageuzi,vyongozi watimuliwa
Yakitajwa wazi wazi,yapo yanayoibiwa
Nani alivunja nazi,ni bora tungeambiwa
Hi sanaa ya arusha,kama ina matapeli.
7)Leo huyu kesho yule,
Digega akaja Fredi
Au twendeni kule,tukaogee magadi
Mkosi upite vile,sana iwe yetu jadi
Hi sanaa ya Arusha,kama mpira wa kona.
8)Chalo baada ya chinga,akashika usukani
Gizani bila ya mwanga,gari likenda shimoni
Magesa akajifunga,kimya asiseme nini
Hi sanaa ya Arusha,kama vile inakufa.
9)Kisa pesa nauliza,ndo kinachotuangusha ?
Wengine kinawaliza,chozi chini wadondosha
Ndoto mnazimaliza,na moto mnaviwasha
Hi sanaa ya Arusha,kama mzoga wa paka.
10)Ningelikuwa rahisi,hatua ningechukua
Ngumu isiyo rahisi,hukumu ningeamua
Vyovyote mtavyohisi,ujumbe wawafikia.
Hi sanaa ya Arusha,wapi inaelekea.
Shairi=SANAA YA ARUSHA
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha
+255624010170
iddyallyninga@gmail.com
[HASHTAG]#mimimalenga[/HASHTAG]