Samwel Sitta: Siyoi Sumari hakuwa Chaguo la wanaCCM

Hata maandiko yanasema wacheni wafu wazike wafu wao imefika wakati mbingu ya mungu imeamua kufunguka msiache kuomba na kusali kisa mmeshinda tunaitaji ukombozi wa jumla toka kwa mungu
 
jamani kufa kwa ccm ni muda wake na wala si siasa za makundi. Gamba ni kitu kilichokufa na hakuna namna ya kurudisha uhai tena. Sana sana laweza kumwagiwa maji ili lionekane ni hai lakini litanuka tuu. BYE forever to ccm
 
Kweli kuweweseka ni kama chafya. Sasa huyu babu mnafiki hapa anatoa ujumbe mwingine tofauti na anaodhani anautoa: CCM inapochagua viongozi na wawakilishi huwa hakuna umakini na uzingativu wa mambo na ndio maana tuna mawaziri kama Ngeleja na Mponda, Sitta na Wassira.

Maiti ya CCM inanuka vibaya jamani.

Sasa nimuombe mwenyekiti wa chama awakusanye wale wachezabao wa mwembe yanga (ze so called wazee wa DSM) akawahutubie. (maana hiyo ndio intellectual forum yake)
 
Tatizo la Sita,siku ikipita bila kutajwatajwa na vyombo vya khabari Tz anajihisi kuumwa,.ila hana lolote na unafiki wake!
 
Alikuwa wapi kusema siku zote? Je angeshida angesema hivyo? Huo ni unafiki, kwa nafasi yake ndani ya CCM, anajua mahali muafaka kwa kupeleka malalamiko yake, na kama yasingesikilizwa, CCM siyo mzazi wake, angeweza kutoka. Aina hii ya wanasiasa hawafai huko CCM wala hata upinzani.
 
Nimeshangazwa sana kusikia Mh. S. SItta
akisema Sioi hakuwa chagua la wanaccm maana kapandikizwa
kwa mizengwe.

Akiongea kwa masikitiko kwa ccm kuzidi kudhoofika na kutokukubalika
kwa wananchi amamuomba mwenyekiti wa chama kusafisha chama ili nyota
ya chama ianze kung'ara. Hii ni kwa mjibu wa sitta baada ya kuongea na waandishi wa HAbari

images



Mytake:

Naona chama kinazidi kuparaganyika na sitta anazeeka vibaya
maana unafiki wake ndo unamponza
Mzee Sitta si mnafiki .Chama na Magamba wana upeo mdogo sana wa kusoma alama za nyakati ,ndio maana viongozi wote wenye maamuzi ni wazee waliokuwa viongozi tokea miaka ya 75-90.Kwahiyo kumwita Sitta mnafiki ni kama kumpa sifa kuwa anaelewa mambo ila unafiki unamsumbua .Huyu haelewi anachosimamia hata siku moja kwa kuwa anauelewa mdogo wa kuchanganua mambo.Siku zote anahadaa watu kwa uzoefu wake ili hali hana maono.
 
Kaazi mnayo mwaka huu wana ccm na naomba kutokuelewana kwenu na Makundi yaendelee hivihivi mpaka mtakapoingia kaburini wabaya wakubwa nyie watu,na mlaaniwe sana tena sana alaaaaaaah!
 
hata yeye anatakiwa awe cleaned kwa kuanzisha ccj ndani ya ccm!!
 
Ni kutapatapa. Wananchi sasa wanaikataa CCM bila kujali nani amegombea. Huko Kirumba CCM iliposhindwa ambapo yeye ndiye alikuwa kinara wa kampeni anaelezeaje? Sasa watu wanachagua mabadiliko wala hawaangalia nani anagombea.
 
Du nashindwa kumuelewa 6, anasema baada ya tukio, je, hakujua toka mapema kuwa si chaguo la chama? Na kwanini walikaa kimya wakati wa mchakato wa uteuzi? Kulilipotiwa kuwa kulikuwa na suala la rushwa liakazimwa juu juu! Hayo ndo majibu!
 
Jamaniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii,yeuwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii,sioi siooleeeeeeeeeeeeeee,Kiruuuuuuuuuuuu.....sioleeeewiiiiii

we...acha Bana....Mchmba.....Sioi....rudi kenya.....siasa kwako F.................................Sie tunarudi Mjengoni...Bye SIOI
 
Sitta na Mwakyembe ni wanafiki na wana njaa kali sana. Mbona yeye alikuwepo Mwanza kufunga kampeni na mgombea wao kabwagwa kwa percent karibu sawa na Arumeru ina maana na Masamaki wa Kirumba hakuwa chaguo la chama. Kama chama kinajiwekea wagombea bila kufuata demokrasia kwa nini hawajitoi na kujiunga na chama kingine kama sio njaa tu.
Kwa hiyo anachofanya Sitta ndio ile tulisikia wanasema TUSHINDWE TUHESHIMIANE???
 
Back
Top Bottom