Samwel Sitta: Sina muda wa kulumbana na UKAWA

Samwel Sitta: Sina muda wa kulumbana na UKAWA

MBUNGE wa Jimbo la Urambo Mashariki Samwel Sitta, amepokelewa kwa kishindo Jimboni kwake Urambo na kuhutubia katika Viwanja vya Mwananchi Square.

Sitta akihutubia wapigakura wake alielezea jinsi mchakato wa Bunge Maalum la Katiba ulivyokwenda hadi alipokabidhi Katiba inayopendekezwa kwa Rais Dkt.Jakaya Kikwete.

Katika hotuba yake hiyo, Sitta ambaye alikuwa Mwenyekiti wa bunge hilo, alielezea jinsi katiba ilivyotoa haki za wakulima, wafugaji, haki za watoto, baraza la vijana la Taifa, hamsini kwa hamsini kwa wanawake katika nafasi za uongozi na mengineyo.

Aidha, amewataka wana Urambo na watanzania kuipitia Katiba inayopendekezwa kwa kina na ufasaha kwani imekidhi vigezo na matakwa ya wananchi yenye maslahi mapana ya vizazi kwa vizazi.
===================

10418983_802870006443650_17526327949523614_n.jpg

Samwel Sitta wakati wa shughuri ya kumsimika.
10704076_802869316443719_2623104900641162220_n.jpg

Mhe. Samwel Sitta akihutubia wananchi wake katika mkutano wa kumpongeza kwa kazi ngumu ya kuliongoza Bunge Maalum
10710696_802870223110295_8112502459661380857_n.jpg

10365728_802870863110231_469350024327703825_n.jpg

Kaka maelufi au Maherufi????Hayo maelfu yako wapi???Cha maana kaenda kuzungumza nini huko licha ya UKAWA???
 
Nimefanikiwa kutembelea tovuti ya utoaji mikopo VICOBA ambayo ni www.vicobatanzania.wapka.mobi nimejiunga na kupatiwa mkopo nimechukua mil.10 mil.5 nahitaji kuwekeza ktk biashara ya duka la jumla la vinywaji mil.5 nyingine nataka kununua kiwanja.

Wana JF kwa mwenye wazo lolote au ushaur kuhusu biashara ya duka la jumla anisaidie nawaomba.

Anzisha uzi tuje mama, humu tena mmmh kazi
 
MBUNGE wa Jimbo la Urambo Mashariki Samwel Sitta, amepokelewa kwa kishindo Jimboni kwake Urambo na kuhutubia katika Viwanja vya Mwananchi Square.
Sitta ni shujaa wa taifa hili, kwa kazi nzuri sana iliyotukuka ya kuzitoshesha zile kura za ndio, na kila atakakopita atopokelewa kwa shangwe kama hii ya Urambo, nimeshauri Sitta ndie awe mgombea wa CCM, 2015!.
Kufuatia Sitta Kuonyesha Ushupavu katika Katiba, Jee Tumpe Urais 2015!.
[h=3]Hongera Sana Samuel Sitta!, 2015 Utatufaa Sana Ukiwa Rais Wetu!.[/h]Pasco
 
Kwikwikwi maelfu ya watu...Leo Kibanda maiti ni shida...Kama hapo ni nyumbani Sitta kapokewa hivyo akienda kwa wengine si watamnyea? Mimi naandaa kinyesi akija kwetu namwagia bwe.ge kabisa huyo!!!

Hili ni janga la kitaifa.hana jipya huyu ndumi la kuwili
 
Hala bwana SItta kama kweli hii katiba ni watu wote kwa nini CCM tu ndio waliohudhuria huo mkutano??
 
Anatia huruma! You can tell by his face. Tabora kuweni wajanja mle nae hizo alizochuma kwa ulaghai. Shame on him!
 
Mkuu Mama Zakia Meghji aliongeza idadi za kura za Zanzibar hadi zikatosha kwa mujibu wa Samwel Sitta!!! ... atokeo ya kura za BMK na mchakato mzima inatupa ishara tosha jinsi ambavyo chaguzi zinavyoendeshwa hapa Tanzania... Sasa naamini kwa CCM haijawahi kushinda Zanzibar kihalali toka mfumo wa vyama vingi ulipo asisiwa hapa nchini...
SUALA JE ZNZ katiba yake inaweza kura za ndio kukidhi haja ya matakwa ya sharia yaani 2/3 za ndio ili ikubarike?

Bara naona hakuna mushkirah ila Znz mmh!

Mtihani huo.
 
anajipa moyo tuu sitta ni mnafiki sana hao watu mbona wamevaa sare za ccm wameshonewa kwa ghaama za pesa zetu hii ni aibu kwa serikaki ya ccm kuwadahaa wanachi kwa kanga au t-shirt ili waje kwenye mikutano
 
MBUNGE wa Jimbo la Urambo Mashariki Samwel Sitta, amepokelewa kwa kishindo Jimboni kwake Urambo na kuhutubia katika Viwanja vya Mwananchi Square.

Sitta akihutubia wapigakura wake alielezea jinsi mchakato wa Bunge Maalum la Katiba ulivyokwenda hadi alipokabidhi Katiba inayopendekezwa kwa Rais Dkt.Jakaya Kikwete.

Katika hotuba yake hiyo, Sitta ambaye alikuwa Mwenyekiti wa bunge hilo, alielezea jinsi katiba ilivyotoa haki za wakulima, wafugaji, haki za watoto, baraza la vijana la Taifa, hamsini kwa hamsini kwa wanawake katika nafasi za uongozi na mengineyo.

Aidha, amewataka wana Urambo na watanzania kuipitia Katiba inayopendekezwa kwa kina na ufasaha kwani imekidhi vigezo na matakwa ya wananchi yenye maslahi mapana ya vizazi kwa vizazi.
===================

10418983_802870006443650_17526327949523614_n.jpg

Samwel Sitta wakati wa shughuri ya kumsimika.
10704076_802869316443719_2623104900641162220_n.jpg

Mhe. Samwel Sitta akihutubia wananchi wake katika mkutano wa kumpongeza kwa kazi ngumu ya kuliongoza Bunge Maalum
10710696_802870223110295_8112502459661380857_n.jpg

10365728_802870863110231_469350024327703825_n.jpg

Haya ndio maelfu ya wananchi ?.Hivi ni kwa nini ccm mmezoea maigizo namna hii!!!!?.
 
Wanasiasa bwana! Anasimikwa mara ngapi? Au kila kukiwa na tukio anasimikwa? Hizo haki mbona zinakazaniwa sana wakati ni dhahiri hazitatekelezeka. Kwani katiba ya sasa haina hizo haki, mbona makundi hayo hawazipati?
 
there is apossibility hawa watu(hasa watu wazima) wamekusanywa na mabasi toka kigoma, mbeya, singida iringa shinyanga na na maeneo ya nzega , igunga. watu wa kijijni hawawezi kuwa hivi

Pesa ya kuwasomba watu kuwaleta hapo ilitolewa kwenye zile pesa za Gadafi ambazo Membe amezichimbia kwa
Handaki mafichoni akiogopa kuziweka Benk Maana anajua mahakama ya Hague itambeep , hizo pesa kawagawia Dr Kigwangwala, mwandosya, Sita na Dialo ili wamsaidie kumchafua Lowasa kwenye mitandao.
 
Barubaru, #15 :

Kwa mujibu wa rasimu ya ccm iliyoanza kuandaliwa siku nyingi tu mafichoni na akina Chenge na wenzake, sasa Ndio katiba inayopendekezwa, na ukiangalia ukurasa wake wa mwisho Inasema:

• Mambo ambayo mabadiliko yake yanahitaji kuungwa Mkono kwa zaidi ya nusu ya kura halali zilizopigwa na wananchi wa Tanzania bara na zaidi ya nusu ya kura halali zilizopigwa na wananchi wa Tanzania Zanzibar Katika kura ya maoni ni:

1. Muundo wa muungano.

2. Uwepo wa serikali ya jamhuri ya muungano.

3. Kubadilisha masharti ya ibara ya 129(i)c ya katiba inayopendekezwa.

Kwa maana hii, mapendekezo ya rasimu ya tume ya jaji warioba kuhusu upitishwaji wa katiba mpya kwa theluthi Mbili (2/3) Kama utaratibu ulivyo duniani kote, mapendekezo haya ya 2/3 yamechakachuliwa. Badala yake, kilichoingizwa na akina Sitta, Chenge na wenzao ni 50.01%.

Kwa maana nyingine, ccm imeshajipangia utaratibu wa kutafuta Ushindi wa just 50.01%. Na baadae akina MwanaDiwani watakuja humu kujadili Kwamba "Ushindi ni Ushindi" Kama vile suala la katiba mpya ni sawa na la uchaguzi wa Diwani.

CCM inajua wazi Kwamba kufuata utaratibu wa theluthi Mbili kungeinyima rasimu yake ya katiba kura za kutosha, kwani kwa jinsi Hali ilivyo, two thirds hata kwa Tanzania bara zingekuwa Ngumu sana kupatikana.

Aliyeunda muungano ni TANU na ASP, atakayevunja muungano ni CCM.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Ni rahisi kwa Tembo kupenya kwenye Tundu la Sindano kuliko Sita na Membe Kuwa Rais wa Tanzania .
 
No matter who will be ccm presindential candidate, because of their hypocrite mission on new katiba will face hard time. It won't be easy for them!
Muta, ilikuwa ngumu dana ndani ya BMK, ikija kwa wananchi, it's as simple as abc!.
Pasco
 
Binafsi nilikuwa Simkubali kabisa Mh. Samwel Sitta hasa jinsi alivoendesha Bunge la Tissa kwa kulifanya Jukwaa la kusakama wapinzani wake wa Kisiasa lakini baada ya kupumzishwa na kuona jinsi Nguli wa Siasa, Mwanamke wa Karne Anne Makinda akiongoza Bunge kwa kanuni na Sheria bila ya ushabiki nae kajifunza na Hatimae kafanikiwa kutuletea Katiba Pendekezwa Bora kabisa kusini mwa Jangwa la Sahara kama alivoahidi. Hongera Sitta Hongera Comrade Andrew Chenge

Utakuwa mgombea mwenza wa Sitta.
 
Zanzibari subutu. Mliona mkutano wa wanzanzibari leo. Wanaita katiba pendekezwa ni rasimu ya chenge na sita. Na majina ya wajumbe wa bmk waliopiga kura ya ndio yataandikwa kwa supu ya ngisi.
 
majority wana umri kama wa sita! ndo maana wanasema liwalonaliwe maana hawana uchungu nao!
 
Back
Top Bottom