Barubaru,
#15 :
Kwa mujibu wa rasimu ya ccm iliyoanza kuandaliwa siku nyingi tu mafichoni na akina Chenge na wenzake, sasa Ndio katiba inayopendekezwa, na ukiangalia ukurasa wake wa mwisho Inasema:
Mambo ambayo mabadiliko yake yanahitaji kuungwa Mkono kwa zaidi ya nusu ya kura halali zilizopigwa na wananchi wa Tanzania bara na zaidi ya nusu ya kura halali zilizopigwa na wananchi wa Tanzania Zanzibar Katika kura ya maoni ni:
1. Muundo wa muungano.
2. Uwepo wa serikali ya jamhuri ya muungano.
3. Kubadilisha masharti ya ibara ya 129(i)c ya katiba inayopendekezwa.
Kwa maana hii, mapendekezo ya rasimu ya tume ya jaji warioba kuhusu upitishwaji wa katiba mpya kwa theluthi Mbili (2/3) Kama utaratibu ulivyo duniani kote, mapendekezo haya ya 2/3 yamechakachuliwa. Badala yake, kilichoingizwa na akina Sitta, Chenge na wenzao ni 50.01%.
Kwa maana nyingine, ccm imeshajipangia utaratibu wa kutafuta Ushindi wa just 50.01%. Na baadae akina
MwanaDiwani watakuja humu kujadili Kwamba "Ushindi ni Ushindi" Kama vile suala la katiba mpya ni sawa na la uchaguzi wa Diwani.
CCM inajua wazi Kwamba kufuata utaratibu wa theluthi Mbili kungeinyima rasimu yake ya katiba kura za kutosha, kwani kwa jinsi Hali ilivyo, two thirds hata kwa Tanzania bara zingekuwa Ngumu sana kupatikana.
Aliyeunda muungano ni TANU na ASP, atakayevunja muungano ni CCM.
Sent from my iPhone using JamiiForums