Samwel Sitta: Sina muda wa kulumbana na UKAWA

Samwel Sitta: Sina muda wa kulumbana na UKAWA

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2013
Posts
5,536
Reaction score
2,268
MBUNGE wa Jimbo la Urambo Mashariki Samwel Sitta, amepokelewa kwa kishindo Jimboni kwake Urambo na kuhutubia katika Viwanja vya Mwananchi Square.

Sitta akihutubia wapigakura wake alielezea jinsi mchakato wa Bunge Maalum la Katiba ulivyokwenda hadi alipokabidhi Katiba inayopendekezwa kwa Rais Dkt.Jakaya Kikwete.

Katika hotuba yake hiyo, Sitta ambaye alikuwa Mwenyekiti wa bunge hilo, alielezea jinsi katiba ilivyotoa haki za wakulima, wafugaji, haki za watoto, baraza la vijana la Taifa, hamsini kwa hamsini kwa wanawake katika nafasi za uongozi na mengineyo.

Aidha, amewataka wana Urambo na watanzania kuipitia Katiba inayopendekezwa kwa kina na ufasaha kwani imekidhi vigezo na matakwa ya wananchi yenye maslahi mapana ya vizazi kwa vizazi.
===================

10418983_802870006443650_17526327949523614_n.jpg

Samwel Sitta wakati wa shughuri ya kumsimika.
10704076_802869316443719_2623104900641162220_n.jpg

Mhe. Samwel Sitta akihutubia wananchi wake katika mkutano wa kumpongeza kwa kazi ngumu ya kuliongoza Bunge Maalum
10710696_802870223110295_8112502459661380857_n.jpg

10365728_802870863110231_469350024327703825_n.jpg
 
Kweli nimeamini kwenye siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu. Sitta na chenge ni marafiki sasa, wakati walikuwa paka na panya! Turudi kwenye mada, je sitta hao wazee aliowarubuni kumpa uchifu feki amewalipa kiasi gani?
 
Anatia huruma ,inabidi wamvishe maguo ya kichawi au nguo za jadi ,huyo hakosheki ,atakuwa ameshapata Salamu kutoka zenji ! Si ajabu CCM wakamipitisha kila mkoa !
 
Kweli nimeamini kwenye siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu. Sitta na chenge ni marafiki sasa, wakati walikuwa paka na panya! Turudi kwenye mada, je sitta hao wazee aliowarubuni kumpa uchifu feki amewalipa kiasi gani?

Lipumba alipowatapeli kuwatoa Bungeni aliwalipa Tsh ngapi? Tunampongeza sana Mh. Mbowe kwa Uzalendo wake wa kuhakikisha Sitta anakuwa Mwenyekiti wa Bunge kabla hajaingizwa Mkenge na yule Professa Mseja.
 
Binafsi nilikuwa Simkubali kabisa Mh. Samwel Sitta hasa jinsi alivoendesha Bunge la Tissa kwa kulifanya Jukwaa la kusakama wapinzani wake wa Kisiasa lakini baada ya kupumzishwa na kuona jinsi Nguli wa Siasa, Mwanamke wa Karne Anne Makinda akiongoza Bunge kwa kanuni na Sheria bila ya ushabiki nae kajifunza na Hatimae kafanikiwa kutuletea Katiba Pendekezwa Bora kabisa kusini mwa Jangwa la Sahara kama alivoahidi. Hongera Sitta Hongera Comrade Andrew Chenge
 
there is apossibility hawa watu(hasa watu wazima) wamekusanywa na mabasi toka kigoma, mbeya, singida iringa shinyanga na na maeneo ya nzega , igunga. watu wa kijijni hawawezi kuwa hivi
 
Ni kweli hawezi kuwa na muda kulumbana na UKAWA, sio hao tu, bali hawezi kuwa na muda wa kulumbana hata na mtu yeyote anayetetea maslahi ya wananchi, maana yeye amezoea kufuja mali ya umma bila huruma, ona jinsi alivyong'ang'ania kodi ya wananchi iteketee kwa katiba ambayo hata yeye anajua tangu mwanzo haipo kwa kitendo tu cha UKAWA kuwa nje. Ebu fikiria laki tatu kwa siku kwa vicha zaidi ya 400, mara siku walizokaa bure, yaani siku baada ya UKAWA kugoma na kuonekana dhahiri bila maridhiano hakuna katiba, lakini yeye aling'ang'ania hata kumtishia mke wake kuwa angesema No kusingekalika home
 
SUALA JE ZNZ katiba yake inaweza kura za ndio kukidhi haja ya matakwa ya sharia yaani 2/3 za ndio ili ikubarike?

Bara naona hakuna mushkirah ila Znz mmh!

Mtihani huo.
 
there is apossibility hawa watu(hasa watu wazima) wamekusanywa na mabasi toka kigoma, mbeya, singida iringa shinyanga na na maeneo ya nzega , igunga. watu wa kijijni hawawezi kuwa hivi

Naapa hapa siku magamba wakifanya mkutano bila ya kusomba watu kwenye malori hata kama mkutano ni wa M/KT wa chama taifa wakifika watu 500 basi uchaguzi ujao watashinda kwa kishindo.

Watu wanasafirishwa bure na posho juu anayebisha aje hapa
 
Maigizo yaliyokuwako BMK, sasa Sitta ameyahamishia Urambo!!!??? Ovyoooooo!!! Kabla ya hizo blabla, aeleze kwanza Ofisi yake ya Uspika aliyojenga Urambo inatumika vipi kwa sasa!!!!
 
Lipumba alipowatapeli kuwatoa Bungeni aliwalipa Tsh ngapi? Tunampongeza sana Mh. Mbowe kwa Uzalendo wake wa kuhakikisha Sitta anakuwa Mwenyekiti wa Bunge kabla hajaingizwa Mkenge na yule Professa Mseja.

Yaani kuna wanawake wanashida jamani, kwetu Sumbawanga tunamsemo unasema "Mwanachi uwatambi atangi asakwe, nanti wasakwa yalumta" Yaani mwanamke wa tabia haolewi na akiolewa abadan ataachicha" vinginevyo mume naye anatatizo. Ndicho ninachokiona kwako mwanamke unamaneno ya karaha kama mpiga debe sipati picha mtaani kwako, sidhani kama unajirani rafiki, unakinywa kichafu sijapata kuona
 
MBUNGE wa Jimbo la Urambo Mashariki Samwel Sitta, amepokelewa kwa kishindo Jimboni kwake Urambo na kuhutubia katika Viwanja vya Mwananchi Square.

Sitta akihutubia wapigakura wake alielezea jinsi mchakato wa Bunge Maalum la Katiba ulivyokwenda hadi alipokabidhi Katiba inayopendekezwa kwa Rais Dkt.Jakaya Kikwete.

Katika hotuba yake hiyo, Sitta ambaye alikuwa Mwenyekiti wa bunge hilo, alielezea jinsi katiba ilivyotoa haki za wakulima, wafugaji, haki za watoto, baraza la vijana la Taifa, hamsini kwa hamsini kwa wanawake katika nafasi za uongozi na mengineyo.

Aidha, amewataka wana Urambo na watanzania kuipitia Katiba inayopendekezwa kwa kina na ufasaha kwani imekidhi vigezo na matakwa ya wananchi yenye maslahi mapana ya vizazi kwa vizazi.
===================

10418983_802870006443650_17526327949523614_n.jpg

Samwel Sitta wakati wa shughuri ya kumsimika.
10704076_802869316443719_2623104900641162220_n.jpg

Mhe. Samwel Sitta akihutubia wananchi wake katika mkutano wa kumpongeza kwa kazi ngumu ya kuliongoza Bunge Maalum
10710696_802870223110295_8112502459661380857_n.jpg

10365728_802870863110231_469350024327703825_n.jpg

samweli sitta ni janga la kitaifa hana jipya la kutueleza sisi watanzanialabda wana urambo na nakuhakikishia 2015 harudi bungeni tena huyu ndumi la kuwili
 
Kwikwikwi maelfu ya watu...Leo Kibanda maiti ni shida...Kama hapo ni nyumbani Sitta kapokewa hivyo akienda kwa wengine si watamnyea? Mimi naandaa kinyesi akija kwetu namwagia bwe.ge kabisa huyo!!!
 
Back
Top Bottom