Samwel Sitta ashangiliwa sana UDSM


alipokua TIC hakuwa na authority kwa kila uwekezaji kua na data kwanza kijana kabla ya kurukia jambo, tanzania tunapata 3% toka tanzanite one, hawa hawakupita TIC walienda kwa ofisi ya rais Mkapa moja kwa moja,. hapa inaonyesha kuna uwezekano wa Richmond kupita kwenye ofisis nyingine na siyo TIC na hata kama ilipita pale Sitta siyo mjinga wa kupitisha kitu cha ajabu akiwa mkurugenzi aje akipinge baadae kwa kuita feki ni ujinga hata kwa mtu asiokua na uzoefu au hata fisadi mroho yeyote. Richmond ikama ilipita TIC ilipita kwa Ole Naiko mtu wa karibu wa EL kwa sababu alikua anakaimu nafasi wakati wa kuelekea kwa kampeni za uchaguzi 2005.

Kama hili hujafanya umakini kulijua basi hata hilo la ofisi ya ubunge/uspika tuna mashaka nalo kwani kredibiliti na uchambuzi wako usiokua na upande unatia mashaka tayari kwa hoja yako ya hapo juu
 

Huko kote alikopita Sitta nakushauri tumia muda wako na busara yako ndogo kufanya utafiti utajua madudu aliyoyaacha, mfano mdogo tu Sitta aliitafuna CDA hadi sasa imeshindwa kutengemaa kwa ufisadi wake.
 
Samwel Sitta ndiyo kiongozi wa CCM anayekubalika na wananchi wa Tanzania kuliko mtu yoyote yule kutokana na kupinga ufisadi kwa vitendo. Ukweli ndiyo huo. Hata CHADEMA wanamuheshimu Sitta kwa hili na rekodi yake ya uongozi haina doa.
hapo kwenye wekunduunaongelea vitendo vipi haswa alivyofanya sitta vinavyoonyesha anapinga ufisadi?mimi nimemsikia mara kadhaa akilalamika kwenye vyombo vya habari kama alivyofanya mengi!
 
hapo umenena!ni ujuha sitta kwenda ITV na kulalamika wakati uwezo wa kumface J.K anao
 

Wait.....Sitta ambaye hakuwa Mbunge, hakuwa mjumbe wa NEC, hakuwa mjumbe wa Kamati Kuu, hakuna na ushawishi wowote kwenye chama eti alikuwa na mchango mkubwa sana kwenye "mtandao" kuliko Lowassa, aliyeliasisi kundi hilo, kuliongoza kimkakati na kufanikisha ushindi mpaka eti Sitta astahili wakati ule kuwa Waziri Mkuu na sio Lowassa?unahitaji kuwa zuzu kuliamini hili..

...Ni kweli kabisa, umbumbumbu wa watanzania ndio unaowafanya waamini vitu vya kitoto kama hivi,amka mchana ungalipo..
 

mkuu naona hujanielewa! Huamini kitu gani? Kwa taarifa yako muasisi wa mtandao ni JK, EL na RA, Sitta ni kama wanamtandao wengine wa kawaida. Vikao vyao vilikuwa vikifanyikia TIC na kumbuka kampuni feki nyingi zimesajiliwa na TIC wakati wa Sitta. sasa angalia linkage yao na mtandao na akina Richmond. Ni makampuni yaliyosajiliwa kwa manufaa yao wanamtandao wakijua wanachukua nchi. Zinduka angalia hesabu zao zilivyokuwa. Sitta aliutaka u-PM, kwa kuwa hakujua hesabu za mapacha 3 (JK, EL na RA) akadhani atapewa. Wenzie wakanyamaza tu, uchaguzi ulipoisha RA akacheza hesabu zake ili kumtolea nje Sitta na u-PM ikabidi wamchomekee uspika wa Bunge. Amini nakwambia Sitta hakufanya hata kampeni kila kitu kilimalizwa na RA. Ndipo EL alipoteuliwa kuwa PM. Hilo linamuuma sana Sitta hadi leo. Ngoma hiyo wengi hatuijuwi hivyo hatuwezi kucheza mdundo wake tunabaki kushabikia tu watu wakitumia vyombo vya habari kwa mameno bila vitendo....loh......nchi yangu Tanzania nakupenda kwa moyo woteeeeee....tuimbe pamoja!
 
kilichomponza sitta ni undumilakwili wake ,hakuchukua upande mapema.kama aliamua kupinga ufisadi angeendelea kufanya hivyo na sio kuuma na kupuliza.kelele zake zimeongezeka sana baada ya kukosa uspika bahati mbaya its too late JK na RA wamemuwahi na kumpunzisha wizara isiyo na tija.hii inatufundisha kuwa wawazi na tuchague kati ya moto au baridi sio vuguvugu.
sitta,mengi,kilango,nape,januari,shibuda ni watu wanafiki niliopata kuwafahamu.
 

rudia nilichosema richmond iliungwa ungwa kwenye ofisi nyingine au tic chini ya Ole Naiko na siyo Sitta, upotoshaji huu hautaruhusiwa hapa.

Kama Sitta alikua anautaka sana uPM hayo ni yake binafsi kila mtu ana yake binafsi mbona hata Lowassa alikua anataka uRais kwa kupitia mgongo wa JK na sasa ni ndoto ndefu( anaanza bifu na kila mtu akiwemo JK na familia yake, membe nk kwa kukatiza ndoto hii takatifu) kitu muhimu ni genius ukiunganisha chuki binafsi na malengo au mwelekeo wa walio wengi yaani sisi wananchi tunamuona mzalendo, hodari na mchapa kazi katika kundi la wezi na wasio wazalendo..Lowassa chuki yake binafsi ameshindwa kuioanisha na malengo, mwelekeo wa wananchi walio wengi kabaki na kundi lake wanaha ha kutumia dola wasafishwe.

Nb: Chuki binafsi iliongoza hata nchi zetu kukombolewa Mugabe asingechukia matendo ya wazungu wadhalimu Zim uhuru ungekuja kama Namibia 90s, vile vile Nkrumah, Nasser, Nyerere, etc ukitoa nafikiri Houghout Boigny aliyekua anataka Wafaransa wasitoe uhuru kwa nchi yake iendelee kuwa katika federation ya ufaransa with a second status kama ilivyo Puerto Rico na US. Hii unayosema" chuki binafsi" ya Sitta itamfanya kama akitaka kugombania urais awe makini zaidi na ufisadi na mfumo wte wa kifisadi anaouchukia na kuwachukia wale wanaouendekeza
 
hapo umenena!ni ujuha sitta kwenda ITV na kulalamika wakati uwezo wa kumface J.K anao

jingalao JK nani kakwambia anashawishika? angekua anashawishika asingefanya madudu kwenye uongozi kua makini jinga Lao..vyombo vya habari ni muhimu na Sitta anavitumia kushinikiza pablik presha ifanye kazi. katika mfumo huu wa kiliberali vyombo vya habari vina nafasi mahsusi kwa wanasiasa kufikisha ujumbe kwa walengwa wote.
 
naamini Jk anashawishhika kupitia mawaziri aliowateua,na kama sitta anaona JK hasikii au haelewi basi sitta ajiuzulu au angekataa uwaziri mapeeema!
vyombo vya habari atuachie sis,kubenea na kina reginald na yeye atumie mbinu zinazoendana na wadhifa wake.
 

...Usijidanganye na kudanganya wengine, kwa nafasi aliyokuwa nayo Sitta kwenye mtandao, cheo cha Uspika kilikuwa ni cheo kikubwa zaidi ambacho angeweza kukipata, na kama angekuwa "kondoo anayejali maslahi yake binafsi", asingesumbuka kamwe kupambana na uovu wakati akijua kuwa kwa kufanya hivyo anahatarisha maslahi yake.

...Wahenga walisema "Usichokijua ni kama usiku wa kiza, na kama hujui kitu, kukaa kimya ni busara zaidi",...wewe endelea kuimba tu wimbo wa "Mnafiki" kama kasuku, ndipo unapopaweza zaidi kwani kadri unavyojaribu kuungaunga hoja ulizozisikia kwenye wimbo huo ndivyo unavyozidi kujivua nguo hadharani...
 
Mkuu haya yana mwisho na mtaujua ukweli,Sitta anabebeshwa sifa asizokuwa nazo tena na wana JF niliokuwa nadhani kwa kelele zilizopigwa humu hawawezi kudanganyika kirahisi.mbona hamjiulizi kuna ufisadi mwingi tu tena wa kutisha lakini hapigi kelele? Ila issue ikiwa ya eddo mishipa inamtoka? Simtetei na sitokuja mtetea eddo lakini hatutaki unafiki! Dr slaa anapambana na ufisadi mpaka kwenye kata na huu ndio mfano wa vitendo.huyu sitta atuambie lile jengo alilojenga kwao urambo eti ofisi ya spika ni tija? Alitaka awe spika wa maisha? Huu ni usaliti tu!
 

...Naona bado haujui mchezo wa siasa unavyochezwa...

...Kuna wengine pia hawakumwelewa Raila Odinga alivyoamua kurudi ndani ya KANU ya Mzee Moi baada ya kupingana nayo akiwa nje kwa muda mrefu bila mafanikio. Sometimes kupambana ukiwa ndani ya vyombo vya maamuzi kunaleta matokeo mazuri na ya haraka zaidi kwa nchi kuliko kupiga kelele ukiwa nje, ata Augustino Mrema analijua hili...
 

...Unaweza kuthibisha kuwa Sitta alijenga ofisi ya Spika wa Bunge wilayani Urambo?tusiimbeimbe tu kama kasuku!!
 
Mkuu eddo mwenyewe alikiri bungeni kabla ya kujiuzulu kuwa issue kubwa si richmond bali ni uwaziri mkuu!!! Hebu fikiria maana ya haya maneno mazito!
 
ina maana Raila Odinga alifanikiwa akiwa KANU au?
 

Ahsante sana Mkuu.
 
Amewahi kukanusha? Madogo haya?

...Wewe uliyeiimba huu wimbo wa Sitta amejenga "Ofisi ya Spika" wilayani Urambo unaweza kulidhibitisha hilo?au ndio yaleyale ya kukaririshwa tu nasi twaimba tu bila kujiuliza kama kawaida yetu?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…