Samsung yakiri Tv zao zinanasa sauti

Samsung yakiri Tv zao zinanasa sauti

poposindege

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
456
Reaction score
175
Samsung imewaonya wateja wake kuhusu kutojadili mambo yao ya kibinafsi mbele ya televisheni zao.

​
Onyo hilo ni kwa wale watazamaji ambao hudhibiti televisheni zao kwa kutumia sauti.
Baadhi ya runinga hizo za kisasa husikiliza mambo ambayo wanasema na zinaweza kuwasilisha ujumbe kwa Samsung au mashirika yanayohusiana na Samsung kibiashara.

Onyo hilo limetolewa baada ya habari kuchapishwa katika gazeti la mtandao "Daily Beast" iliyochapisha sehemu ya sera za Samsung zinazosimamia umiliki wa kibinafsi wa televisheni zao.

Sera hiyo inaelezea kwamba televisheni hizo zitakuwa zinasikiliza watu katika chumba kimoja wakijaribu kutoa amri na maswali kutumia vibonyezi.

"Iwapo maneno ambayo umeyatamka ni ya kibinafsi au ya kisiri , basi ujue kuwa habari hiyo itakuwa kati ya habari zilizonaswa na kusambazwa kwa watu wengine." Samsung imeonya.

Chanzo:
bbc
 
Zinarushaje hizo data kwenda kwenye database yao? nadhani hapo ni smart_tv tu.
 
Samsung hawana muda na kunasa maongezi yako, we mtanzania ambaye hata TV hajaconnect kwenye internet analaumu nini, kuhusu TV zao kunasa sauti hili halihitaji kutangazwa maana linajulikana wazi smart TV zao zina mic na camera mtu unaweza kutumia skype kuwasiiliana sasa mtu anajua yote haya afu bado anauliza kama inanasa sauti kweli!

Hivi unajua wangesema wanatunza maongezi ya kila mtu duniani, tusema wauze TV 50million, wanamrekodi mtu masaa 10 kwa siku afu wanatunza kwenye server zao, tuseme kila saa moja ni 20MB ya Audio, masaa 10 ni 200MB, kwa mwaka kila TV moja iwe imewatumia Audio 73GB, kwa TV 50million unajua hizo ni Petabyte 3,650, hiyo audio data hata server za Google hazina uwezo wa kuprocess, hawana muda wa kujenga data centre kwa mabilioni kisa kutunza maongezi ambayo 99% unakuta hayana umuhimu wowote...

na tukisema wanakaa wanakusikiliza kila wakati ni uongo, hamna watu 50million wa kukaa wanasikiliza kila mtu kwa wakati moja kujua unaongea nini....hata tukisema wanatumia software kucapture some keywords kama neno kill, itabidi waunde data centre ya kuprocess audio kama 10Petabyte kila siku, ambayo si kitu kidogo, na wewe sijui unakaa kuongea kuhusu kumuua flani mbele ya TV kwa sababu ipi...
 
ufafanuzi mzuri
 
Samsung hawana muda na kunasa maongezi yako, we mtanzania ambaye hata TV hajaconnect kwenye internet analaumu nini, kuhusu TV zao kunasa sauti hili halihitaji kutangazwa maana linajulikana wazi smart TV zao zina mic na camera mtu unaweza kutumia skype kuwasiiliana sasa mtu anajua yote haya afu bado anauliza kama inanasa sauti kweli! .....
Umenikuna kuna watu wanaleta hofu kwa wengine bila sababu.
 
Mwisho tutaambiwa toilet paper zinapiga picha aarrrrrrrgh
 
Kampuni ya kutengeza runinga ya Samsung imekiri kuwa runinga zake zimekosea kwa kutuma sauti za wateja wake bila ya kubana majina na anuani ya wateja husika.Kosa hilo linamwezesha mtu wa tatu kubaini anuani na hata kudakua tabia za watazamaji wake wa runinga.

Hitilafu hiyo ilibainika baada ya uchunguzi uliofanywa na taasisi ya usalama wa mitandao huko Uingereza.
Samsung imesema kuwa inafanya kila iwezlo kuhakikisha wanatoa mfumo utakao bana majina na sauti ya wateja iliisijulikane wala kungamuliwa na mtu wa tatu.

"Samsung inachukulia usalama wa wateja wake kwa umakini mkubwa sana kwa hivyo tutahakikisha kuwa kuna proframu itakayofumba sauti majina na anuani ya wateja wetu," Taarifa hiyo ilisema.

"Runinga zetu za kisasa ''Smart'' zinazouzwa hivi sasa zinaprogrammu hiyo maalum na kwa zile za awali ninawahakikishia kuwa tutawatengenezea programmu yenye uwezo kama huo hivi karibuni.''

Mapungufu haya ni baadhi tu ya matatizo yaliyoikumba kampuni hiyo ambayo imekuwa ikiitengeza bidhaa za kielektroniki. Mnamo Februari tarehe 10,Samsung ililazimika kubadili sera zake baada ya mtaalamu mmoja kubaini kuwa runing za Samsung zilikuwa zinanakili na kupeperusha taarifa za siri za wateja wake bila ya idhini yao.

Wiki iliyopita wateja wa runing zake walilalamikia mfumo ambao ulikuwa unazima runinga yao kisha inaonesha matangazo ya kibiashara. Aidha sauti zingine za wateja zilikuwa zinatumwa kampuni ya Nuance.
Baadhi ya runinga hizo za kisasa husikiliza mambo ambayo wanasema na zinaweza kuwasilisha ujumbe kwa Samsung au mashirika yanayohusiana na Samsung kibiashara.

Onyo hilo limetolewa baada ya habari kuchapishwa katika gazeti la mtandao "Daily Beast" iliyochapisha sehemu ya sera za Samsung zinazosimamia umiliki wa kibinafsi wa televisheni zao. Sera hiyo inaelezea kwamba televisheni hizo zitakuwa zinasikiliza watu katika chumba kimoja wakijaribu kutoa amri na maswali kutumia vibonyezi.

''Iwapo maneno ambayo umeyatamka ni ya kibinafsi au ya kisiri , basi ujue kuwa habari hiyo itakuwa kati ya habari zilizonaswa na kusambazwa kwa watu wengine.'' Samsung imeonya.
Kutokana na kukabiliana kuhusu taarifa ya sera yake ,Samsung imetoa taarifa kufafanua jinsi sauti hizo zinavyofanya kazi.

Inasisitiza utambuaji wa sauti unajulikana tu baada ya mmiliki kuchagua kutumia sauti badala ya kubonyeza kifaa cha kiungia mbali (remote control). Samsung imesema kama mteja atakubali kutumia kifaa cha kugundua sauti, sauti hiyo itatambuliwa na mtu wa upande wa tatu baada ya amri ya kuitafuta sauti hiyo.

Upande watatu ambao unatafsiri sauti kutoka kwa wamiliki hufasiriwa na kampuni inayoitwa Nuance, ambayo imehitimu kutambua sauti.

Samsung si kampuni ya kwanza kujipata mashakani kwa kutumia vinasa sauti kwenye mashine na bidhaa zake.
Mwishoni mwa mwaka wa 2013,mshauri wa maswala ya kiteknolijia kutoka Uingereza aligundua kuwa televisheni yake ya LG ilikuwa inakusanya habari kuhusu tabia yake ya utazamaji wa televisheni.

Chanzo: BBC News
 
Mi sina tatizo kama zilishani-record, kikubwa tu wasimtumie wife hizo picha/video
 
Huu ulimwengu wa hacking na cybercrime ni mgumu sana. Jana tu tumesoma NSA wanatumia PC kuiba nyaraka.
 
Haitokuja kutokea siku ambayo teknolojia mpya ikapokelewa bila changamoto kama hizi, kumbukeni hii ni dunia ya ushindani ambapo kila kampuni inajaribu kumuaibisha kampuni nyingine ili kuushinda ubongo wa wateja. Kwa hiyo suala la Samsung siyo ishu kubwa kwani ata laptop yako, desktop au simu inaweza kutuma data kibao ikiwemo picha na sauti mtandaoni... Ni hadi pale mtu au watu(mfano anonymous) au shirika kama NSA watakapoamua kukufuatilia wewe kwa nia nzuri au mbaya ndipo unapoweza kuichukulia Samsung ni dhaifu. Kwa sababu nia ya Samsung kuweka hizi features ni njema, kukuwezesha wewe kuwasiliana na uwapendao kupitia mtandao.
Hii mi teknolojia, ni soko na biashara ya watu wengi.. Ukichukulia mfano wengi wanaotoa tahadhari (whistle blowers) ya vitu kama hivi ni kampuni za cyber security kama McaFee, BitDefender na Kaspersky ambao wao wanajaribu kuibadili ishu kama hii kuwa sehemu ya biashara ambapo wataanza kuuza Anti Malware programs kuilinda smart television yako.
Na sio kweli kuwa Samsung watakuja kukusikiliza chumbani kwako au kuangalia unachokifanya.. Kwa hiyo basi usianze kufunika TV yako au kuziba camera. Cha muhimu ni kuangalia sites unazotembelea kwa smart tv yako na kuhakikisha ni salama, ..
 
Back
Top Bottom