Hiyo simu ya Samsung 21s inanipa faida gani. Faida ya simu ni kupiga, kupokea, whatsapp, instagram na kuandika message thats all. Nini tena cha zaidi ya kutumia gharama eti kununua samsung 21s ya nini?.
Mkuu Hizi Kauli hua tunatoaga tuu kujifariji, lakini ukweli zinaongozwa na mambo mawili tuu, either UBAHILI au NJAA.
Ukitaka ujua ni kipi kinakutesa.....
Hata ukiwekewa mezani hapo kam zawadi kati ya hio simu unayosema ilimradi, let's say inauzawa 200,000 tsh na Hii S21 ultra ya 3,000,000tsh.
Hili hata ubishe hapa Ila Utaamka na S21 Ultra,
Sasa baada ya hapo, kubaki nayo au kutobaki nayo ndio utajua nini kinakutesa..
UKIIUZA,
Wewe kinachokutesa ni njaa.....
UKIBAKI NAYO,
Wewe kilichokua kinakutesa ni Ubahili. .
Hakuna asiyependa kizuri Dunia hii, Na jicho hua halidanganyi, litachagua kizuri, halafu Nafsi nayo ita tamani.
Sasa Hali yako ndio itaamua, Utendee haki ya kile jicho na moyo umependa, Au kusaliti jicho na Moyo Halafu Utoe kauli kama hizi..
Kuna mwingine hata kutumia hio ya 200k kwake hawezi, wewe hapo umesema simu iweze kupiga, ku sms, INSTAGRAM na WHATSAPP baasi.
Yeye atakuja kujifariji nae kwa kukuona na wa ajubu, atasema simu ya laki 2 ni ya nini?
Yeye atasema simu ni kupiga na msg....