Samson Mwigamba una nini na Dr Slaa?

tanzania daima ni gazeti la mbowe siyo la chadema.wala msilete unazi mkawa mnatafuna maneno.issue hapo ni urais wa 2015.mbowe ameanza kujipigia debe kupitia gazeti lake.mtayaona mengi hizi ni rasharasha.unfanya mchezo na wachaga wanavyo itaka nchi kwa nguvu zote ili wafanye ufisadi.wachaga ona tra watupu wanakula rushwa tu.nani humu jamvini atabisha kama tra hawali rushwa.
Lia na baba yako aliyekuwa anamalizia school fees yako kwenye kimpumu.
 
mi nadhani shukrani sio lazima wala sio kitu cha kuomba.kuna usemi tenda wema nenda zako usingoje shukrani.

slaa ametekeleza jukum na wajibu wake,na mwigamba ametii kiu yake kwa kutoa maoni yake kuhusu uchaguzi wa arumeru.

si lazima watu wote waelewane kwa sababu sisi ni binadam.

hata wewe mleta mada si lazima ukubaliane na mawazo yangu wala sikulazimishi.

utakubaliana na facts zilizopo kwenye uchambuzi tu,naomba ndio iwe mwongozo wako.
 
hii thread ina uhusiano wowote na TUNTEMEKE au na MZITO KABWELA?

Kuna baadhi ya watu wakilala wakiamka wanafikiria namna ya kuanzisha ugomvi miongoni mwa viongozi na wanachama wa chadema.
Kuna watu wanatafuta kila mbinu kuweka tension miongoni mwa wanachadema bila sababu yoyote ya msingi.

Kwakuwa tunaelekea kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la arusha mjini, hii inaweza kuwa ndio mwanzo wa chokochoko kama ilivyokuwa wakati wa uchaguzi mdogo wa arumeru mashariki.
 
jana nimesoma kwa makini sana makala ya samson mwigamba kwenye tanzania daima na nikashangaa sana. Nimemtumia ujumbe kumuuliza alikuwa na maana gani lakini mpaka sasa hajanijibu. Hili ndilo nililoligundua katika makala aliyoipa kichwa "arumeru mashariki ilikuwa kama operation ya kijeshi"

ameelezea mambo mengi na kuwashukuru watu wengi sana waliofanya kazi ya ukombozi arumeru, ameanzia kwa mh mbowe, mameneja wa kampeni mchungaji natse na v nyerere, mkuu wa operation john mrema, katibu wa cdm wa mkoa, viongozi wa bavicha na wengine wengi. Lakini jambo la ajabu ni kuwa hakuna hata mahali ambapo alimtaja dr slaa. Sasa mimi nimejiuliza inawezekanaje mwigamba asimuone dr slaa kwenye kampeni? Vyombo vya habari vilituambia kuwa dr slaa alipokewa kifalme arumeru, tulimuona na kumsikia kwenye majukwaa akimnadi joshua, ni yeye aliyekashifiwa kuiba pesa za ujio wa papa, ni yeye alitukanwa matusi mazito na ndugu lusinde. Sasa inawezekanaje mwigamba asimtaje katika shukrani zake? Huu ndio ukamamnda gani, hata kama kuna sintofahamu baina yao kwa nini analionyesha hadharani hivyo? Nilitamani niwawekee vipande vya shukrani zake lakini tanzania daima online haikuiweka hiyo makala, sijui ni bahati mbaya ama wameistukia kama mimi nilivyofanya?

Makamanda tuache unafiki, hata kama mtu ameondolewa kuwa mhasibu wa chama sio sababu ya kuweka kinyongo, tujue tu kuwa cheo ni dhamana na si haki ya mtu. Ukombozi utaletwa na watu makini wenye nia ya dhati na wasio na agenda ya siri nyuma yao. Hoja zote ni lazima ziwekwe mezani, zijadiliwe kisha tusonge mbele kwenye mapambano.

Samson angalia sana usije ukajiweka upande mbaya wa historia ya taifa letu. Katika ujumbe wangu wa jana nilitoa wito kwako uombe radhi wasomaji wako na wana cdm popote pale walipo kwa kosa hilo. Inawezekana ulipitiwa tu na hukudhamiria, kama hivyo ndivyo basi nami utanisamehe.

Saa ya ukombozi imefika

watu wengine bana ni wanafiki , wazandiki wakubwa, na nyie ndo mnaotumiwa kuharibu upinzani, makala hiyo nimeisoma na kamtaja dr. Slaa zaid ya mara 3, ww umesoma tz daima ipi km co umbeya?? Nawachukia sn watu jamii yako, cku zote mnawaza kubomoa, chadema ipo imara sana, na utumbo wako hautafanikiwa! Aibu yako
 
duh kama ni hivyo tunavirus vingi ndani ya chadema inabidi visafishwe vinginevyo mwigamba hutapata kura za maoni mwaka 2015 jimboni kwangu
 
hilo jina lake ni gamba tosha,usipate shida ndugu yangu hao watu ni wale wanaobishana na wakati,kitu ambacho ni kigumu na hakitowezekana daima.mwigamba ni gamba na atakufa na gamba lake
 
msihangaike saana, mabadiliko yanahitajika. ccm is worse than evil. fikiri mwanaoaliwa mvuta bangi mali mnazolimbikiza nani atakula iwapo akaunti zeu zipo new jersey.
 
Slaa ndo president aliye mioyoni mwa Watanzania walalahoi so hata asipotajwa,mioyo yetu imemnukuu vya kutosha sema kilichobaki ni kusubiri tu 2015
 
tatizo kubwa ni kwamba tunadhani tuna chama mbadala!!!ukweli ni kwamba watu tunataka mabadiliko!na hilo ndilo wenye macho huwa tunalipigania!!!na ndio tunasema Chadema ya kesho ni zaid ya CCM ya leo!!!tukiandika tunaambiwa si wanachama!!!KUNA MAPUGUFU MENGI TU CHADEMA!!
Si rahisi namna hiyo, mimi naamini chama chochote kitakachofaulu kukamata dola baada ya CCM kupigwa kumbo kitafanya vizuri zaidi ya hii CCM, iwe CHADEMA au chama chochote kwani CCM ya sasa imejisahau kiasi cha kutomwogopa Mungu wala shetani na wanadhani wao ndiyo wenye hati miliki ya utawala na kamwe hawaondosheki! sasa ikitokea chama kingine kikafaulu kuwashawishi watu kuiondoa na wakafanya hivyo chama hicho kitajitahidi kuwa makini zaidi ili yasiwakute kile kilichowakuta CCM.
Mwisho kabisa ni kwamba hilo likitokea, wananchi watakuwa na kujiamini zaidi katika uamuzi wa kumchagua nani awatawale; kwa maana hiyo kukiondoa iwe CHADEMA au chama chochote kiatachoingia madarakani endapo kitajisahau.
 
Wewe UNAONA MBALI SANA ! Nimekupa jina jipya , kuanzia leo utaitwa DARUBINI KALI PLUS PLUS !
 
Dah! kuna watu wenye kumbukumbu za mbali! huyu aliekumbuka huu uzi na kuibua wakati huu ni mtu wa hatari.Anafaa kuwa mchambuzi wa taarifa za kiintelijensia.
 
Ktk safari yeyote ile ya mabadiliko ni lazima virus wawepo, hao ambao mnawaona wakienda tofauti wilng za wanamageuzi basi tuwapuuze kwani mwisho wao upo 2 na wala si kigezo cha kuzuia mageuzi. BUT CHADEMA ITAFANIKIWA HARAKATI ZAKE KWA HALI YEYOTE ILE( automatically) KWANI UGUMU WA MAISHA NDIO UTAKAO AMUA MWISHO WA MAGAMBA NA WAPINGA MAGEUZI WOTE NDANI NA NJE YA CHADEMA.

living staements ulisema na sasa tumeyaona
 
Back
Top Bottom