Samson Mwigamba una nini na Dr Slaa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Samson Mwigamba una nini na Dr Slaa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbalinga, Apr 5, 2012.

 1. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,381
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  Jana nimesoma kwa makini sana makala ya Samson Mwigamba kwenye Tanzania Daima na nikashangaa sana. Nimemtumia ujumbe kumuuliza alikuwa na maana gani lakini mpaka sasa hajanijibu. Hili ndilo nililoligundua katika makala aliyoipa kichwa "Arumeru Mashariki ilikuwa kama operation ya Kijeshi"

  Ameelezea mambo mengi na kuwashukuru watu wengi sana waliofanya kazi ya ukombozi Arumeru, Ameanzia kwa Mh Mbowe, Mameneja wa Kampeni Mchungaji Natse na V Nyerere, Mkuu wa operation John Mrema, Katibu wa CDM wa mkoa, Viongozi wa Bavicha na wengine wengi. Lakini jambo la ajabu ni kuwa hakuna hata mahali ambapo alimtaja Dr Slaa. Sasa mimi nimejiuliza inawezekanaje Mwigamba asimuone Dr Slaa kwenye kampeni? Vyombo vya habari vilituambia kuwa Dr Slaa alipokewa kifalme Arumeru, tulimuona na kumsikia kwenye majukwaa akimnadi Joshua, ni yeye aliyekashifiwa kuiba pesa za ujio wa Papa, ni yeye alitukanwa matusi mazito na Ndugu Lusinde. Sasa inawezekanaje Mwigamba asimtaje katika shukrani zake? Huu ndio ukamamnda gani, hata kama kuna sintofahamu baina yao kwa nini analionyesha hadharani hivyo? Nilitamani niwawekee vipande vya shukrani zake lakini Tanzania Daima online haikuiweka hiyo makala, sijui ni bahati mbaya ama wameistukia kama mimi nilivyofanya?

  Makamanda tuache unafiki, hata kama mtu ameondolewa kuwa mhasibu wa chama sio sababu ya kuweka kinyongo, tujue tu kuwa cheo ni dhamana na si haki ya mtu. Ukombozi utaletwa na watu makini wenye nia ya dhati na wasio na agenda ya siri nyuma yao. Hoja zote ni lazima ziwekwe mezani, zijadiliwe kisha tusonge mbele kwenye mapambano.

  Samson angalia sana usije ukajiweka upande mbaya wa historia ya taifa letu. Katika ujumbe wangu wa jana nilitoa wito kwako uombe radhi wasomaji wako na wana CDM popote pale walipo kwa kosa hilo. Inawezekana ulipitiwa tu na hukudhamiria, kama hivyo ndivyo basi nami utanisamehe.

  SAA YA UKOMBOZI IMEFIKA
   
 2. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  tatizo kubwa ni kwamba tunadhani tuna chama mbadala!!!ukweli ni kwamba watu tunataka mabadiliko!na hilo ndilo wenye macho huwa tunalipigania!!!na ndio tunasema Chadema ya kesho ni zaid ya CCM ya leo!!!tukiandika tunaambiwa si wanachama!!!KUNA MAPUGUFU MENGI TU CHADEMA!!
   
 3. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kwani SLAA ndiye chanzo cha kuondolewa kwenye nafasi hiyo ya uhasibu? hakuwa na sifa au ili mtu mwingine aikamate nafasi hiyo? au aliingia chama hasara?
   
 4. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2012
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hakuna umuhimu wa kuongeza gap, kinachotakiwa ni ku heal gap
   
 5. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 4,802
  Likes Received: 2,748
  Trophy Points: 280
  kama ilivyo kwenye vyuama vyote!
   
 6. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,381
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  Sawa ku heal gape ni kwa Mwigamba kujishusha. Kujitutumua tena kwa kuandika ni hatari sana kwa mustakabali wa chama. Mwigamba anapaswa kuomba radhi period.
   
 7. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,145
  Likes Received: 1,238
  Trophy Points: 280
  Hatuangalii kesho tunaangalia zaidi leo. Tunashughulika na upuuzi wa CCM wa leo, ikifika zamu ya Chadema hapo kesho tutaushughulikia kulingana na wakati husika.

  Acha unazi.
   
 8. j

  joely JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,030
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Kikubwa ni kuwa chadema ni bora kuliko ccm , na wala sio kuwa chadema ni chama cha mitume na manabii(wa ukweli), changamoto ndani ya chadema ni muhimu ziwepo ili viongozi wasije wakageuka miungu watu.

  Issue ya mwigamba inaweza ikawa personal lakini, whatever the case hata chadema wakiwa na mapungufu sio sababu ya kuparaganyika.

  Kuna mamluki chadema wanaofanya mambo yasiyoendana na matarajio yetu hao tumewaona, tumewasikia na tunawafahamu sana kwani waliowatuma hawana makufuri midomoni mwao.

  Lakini pia kuna watu wengine wanafikiri kuwa chadema ni sehemu ya kutimiza ndoto zao, kwao hao nawambia wapotea njia kwani chadema inatimiza kwanza ndoto za watanzania masikini wasio na msemaji.

  Kwa wale wanaoonyeshs chuki kwa sababu binafsi za kimaslahi wakae wakijua kuwa chadema si mtu ila ni umaa


  chadema dhaifu ni bora kuliko ccm ya wanyang'anyi
   
 9. N

  Nabihu JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 277
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  watu wanachagua mabadiliko sio chama.ukichunguza kwa umakini hivi vyama vya upinzan vina matatizo lukuki na kwakwel ht kama ccm itaanguka bd wananchi tutakuwa na kazi kubwa ya kufanya.
   
 10. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #10
  Apr 5, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  hii thread ina uhusiano wowote na TUNTEMEKE au na MZITO KABWELA?
   
 11. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #11
  Apr 5, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,381
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  Jadili hoja tu, hii haina uhusiano wowotw na Tuntemeke. Tuntemeke ana agenda zake za ajabu tu.
   
 12. toghocho

  toghocho JF-Expert Member

  #12
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  ngoja kwanza cdm wamemaliza uchaguzi nina imani dr. slaa, mbowe, zitto na wengine wamesikia na kuona shutuma zote hizo zikiwemo hayo ya mwigamba na dr. kutoiva, watatafuta solution (watakuwa na mikakati ya arusha na kutafakari arumeru so iweisiwe watakaa) everything will be solved, sio makubwa kihiiiiiiiiiiiiivyo!!!
   
 13. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #13
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hayo ni maoni yake.
   
 14. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #14
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Kwani Mwigamba kaondolewa Uhasibu Chamani?
   
 15. k

  kamakak Member

  #15
  Apr 5, 2012
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  tanzania daima ni gazeti la mbowe siyo la chadema.wala msilete unazi mkawa mnatafuna maneno.issue hapo ni urais wa 2015.mbowe ameanza kujipigia debe kupitia gazeti lake.mtayaona mengi hizi ni rasharasha.unfanya mchezo na wachaga wanavyo itaka nchi kwa nguvu zote ili wafanye ufisadi.ona tra wachaga watupu wanakula rushwa tu.nani humu jamvini atabisha kama tra hawali rushwa.
   
 16. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #16
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  **** **** ****
   
 17. TabletFellow

  TabletFellow JF-Expert Member

  #17
  Apr 5, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 928
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CHADEMA pia inahitaji kujivua gamba.... hivi vyama vilikua kimbilio la waliolosti, and now they should change mrengo wao na kufagia takataka zinazohemea kwenye siasa
   
 18. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #18
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,703
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Ktk safari yeyote ile ya mabadiliko ni lazima virus wawepo, hao ambao mnawaona wakienda tofauti wilng za wanamageuzi basi tuwapuuze kwani mwisho wao upo 2 na wala si kigezo cha kuzuia mageuzi. BUT CHADEMA ITAFANIKIWA HARAKATI ZAKE KWA HALI YEYOTE ILE( automatically) KWANI UGUMU WA MAISHA NDIO UTAKAO AMUA MWISHO WA MAGAMBA NA WAPINGA MAGEUZI WOTE NDANI NA NJE YA CHADEMA.
   
 19. bepari1

  bepari1 Member

  #19
  Apr 5, 2012
  Joined: Sep 10, 2011
  Messages: 74
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  you are right mkuu hilo lazima viongozi wetu walifanyie kazi la sivyo tutajaza mamluki ambao watakuja kutuletea shida huko mbele.
   
 20. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #20
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,703
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Ktk safari yeyote ile ya mabadiliko ni lazima virus wawepo, hao ambao mnawaona wakienda tofauti wilng za wanamageuzi basi tuwapuuze kwani mwisho wao upo 2 na wala si kigezo cha kuzuia mageuzi. BUT CHADEMA ITAFANIKIWA HARAKATI ZAKE KWA HALI YEYOTE ILE( automatically) KWANI UGUMU WA MAISHA NDIO UTAKAO AMUA MWISHO WA MAGAMBA NA WAPINGA MAGEUZI WOTE NDANI NA NJE YA CHADEMA.
  Chadema 4 life
  movement 4 critical changes solidarity forever...\/
   
Loading...