Samson Mwigamba: CHADEMA kuna ubaguzi

Mko wachache sana mliobaki kwa MBOWE na SLAA , na mwisho wenu ni uchaguzi ndani ya CHAMA.
hakuna mtu atakaekulewa zaidi tutasema wewe ni mamluki kutoka ccm maana kazi zinazofanywa na Mboe na Silaa kila mtu anazifahamu na ni viongozi wenye malengo yanayoeleweka na kuelezeka,mbali na chadema hata kwenye vyama vingine hakuna viongozi unaweza kuwafananisha nao
 

Kuna taasisi za kushughulikia hayo na takukuru wapo na ofisi ya mkaguzi mkuu ipo na ofisi ya msajili wa vyama ipo na kama kuna malalamiko hata mahakama ipo kuaddress issue kama hizo pale unapoona haki inavunjwa au inaelekea kuvunjwa
 

Ulitaka kusema nini? au ndo kutetemeka kwa sababu ya kupigwa za uso na Mwigamba?
 
Hivi MwanaDiwani hauna kazi ya Kufanya zaidi ya kusubiria matukio ya CHADEMA na kuanza kuhangaika hapa JF kama mtete na post zako..???
Hivi unalipwa kiasi gani na kama ukiamua kufanya legimate work hauwezi ukapa kipato zaid ya Buku 7 per day????
 
Last edited by a moderator:

Basi kalale
 

Hilo la kufanyakazi hata MWIGAMBA mwenyewe amewasifia, lakini siyo sababu ya matumizi ya udikteta, siyo sababu ya kuvunja Katiba, siyo sababu ya matumizi holela ya fedha za CHAMA hasa ukizingatia kuwa sababu kubwa ya kupatika kwa fedha hizo ni kazi nzuri wa wasomi waliomo ndani ya chama na siyo hao vilaza wanaozivuja.
 
CCM tumeshawajua ni mafisadi na hawafai kupewa Nchi 2015 lakini hivi pia kuna ubaya gani tukiwachunguza na hawa wetu wenyewe kama wana maadili au la maana hatutaki tena surprises huko Ikulu kama hii ya JK.
 
Chadema it is a chagga movement, kama wewe si mchaga utapata shida sana
 

Mr Rocky, Huyu Mwigamba ananishangaza sana...!Kama ulivyosema hayo malalamiko yake kwa nini asingeyatolea ndani ya uwanja wa mapambano...?Sasa yuko nje ya uwanja anababwaja hivi yeye kama mwanasiasa aliyekomaa,ameona wapi hapa duniani mwanasiasa akasaliti chama chake au viongozi wake na wanachama wenzake,halafu akategemea kufanya mabadiliko akiwa nje ya uwaja wa mapambano hata kama Hoja zake ni za msingi...? ETHIC za uongozi wa chama amezipuuza makusudi kwa usaliti,anategemea nini.....???

===> Analalamika KATIBA imechakachuliwa,kwa vipegele vya uchaguzi kunyofolewa hivyo kuwafanya akina Mbowe kuendelea kukaa madarakani...! Ok,na atupe ushahidi wa (kimaandishi) maamuzi ya vikao vilivyopitisha hayo madai yake...?

===> Anadai Mheshimiwa Mbowe pamoja na kazi nzuri waliofanya katika uongozi wao,sasa UWEZO wao umeshuka(Deteriorate)licha ya mafanikio makubwa sana uongozi ulivyofanya.....! Ok,siku ya majanga ilipompata alianza kuwasifia viongozi hivyo hivyo, kwa nini asingeunganisha na hili takwa lake au mtazamo wake kuwa wao viogozi sasa WAMECHOKA (they can't deliver anymore)hapohapo kwenye kikao ili kuzidi kukiboresha Chama kama kweli anania hiyo,badala ya kuzungumza tena kwa kujificha kwenye mitandaoooo....????? This GUY,why so....!
Atuambie ametumia vigezo gani kupima na kuthibitisha KUCHOKA KWA UONGOZI ndani ya Chadema....???

====> Look anadai kuwa hata member wengine ndani ya Chadema (likely viongozi)kuwa nao wanatumia ID fake kama yeye alivyotumia hivyo anataka (justify)kuhalalisha ujinga wake aliofanya hivyo apate (cover-up)sitara kwa uvunjaji sheria,maadili,ya uongozi....????? What a mess is this guy...?
Hakumbuki Mkuu wa Kaya aliwahi kusama "Akili ya kuambiwa,kusikia ,kuona,.....changanya na ya kwako"kabla hujafanya uamuzi. Yeye anaja Miiko na Maadili ya Uongozi kwa kuwa Boss wako anavunja sheria na wewe unavunja.....?????? How such a guy became a Reginal Party Chairman....??? Cowardly.

====> Asiyekuwa mwaminifu kwa jambo dogo;hata kwa jambo kubwa hafai.
CHADEMA kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu tuwe waangalifu sana kwa mambo kama haya.Mengi yatajitokeza,hivyo TUKESHE NA KUWA MACHO.
Bravo CHADEMA.
 
Wakati wengine wanawazo kutafuta mbinu mbalimbali za kustawisha chama na kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya watanzania wewe unawazo uenyekiti. Kimsingi huyu hata akipewa hicho cheo hataweza maana tayari ameonyesha uchu wa madaraka wa hali ya juu. Akaongoze familia yake.
 
Ukiona MaCCM yanamtetea mtu au yanashupalia jambo ujue kuna maslahi yao sio bure.

Kweli Jacque lakini hawapati kitu, wakati huu elimu ya uraia imesambaa sana watu hawadanganyiki tena."Sio ile miaka ya 90 watu wakijitambulisha kuwa ni wapinzani wanazomewa,siku hizi ukisema wewe ni CCM watu wanakuzomea"....by Njelu Kasaka
Bravo mbele kwa mbele mpaka kieleweke.
 
Lengo ni kukinusuru CHADEMA na si vinginevyo, Akiondoka CHADEMA bado kinaendelea kuendeshwa kama Kampuni, Ni lazima akomae huko huko ili wa-ufyate.

Siku si nyingi mkuu utaona Mwenyekiti kwa CCM Taifa wakimpokea kwa mbwembwe zote, let's watch and see....
 
MwanaDiwani karibia mtakuwa vichaa, Akina Shonza wamechuja sasa ni mwigamba..
 
Last edited by a moderator:
Wanaanzisha thread wanaitana ili wajijibu!!! Hata ufanyeje Mwigamba wewe ni kama dot tu kwa CDM!! CDM ni zaidi yako, ni watanzania!! Who is this creature Mwigamba, mchumia tumbo!!! Mwanaume anayehongwa namdharau sana!!! Huna sifa za kuwa mwanaume kama unahongwa!!!! Tusikubali kuwa kupe!!!1
 
Na dhambi ya ubaguzi ni mbaya kuliko chochote, Ukishazoea kula nyama ya binadamu hutaacha - Nyerere
 
MwanaDiwani karibia mtakuwa vichaa, Akina Shonza wamechuja sasa ni mwigamba..

Mkuu the Quest, hajui wakishamtumia wanamtupa kama toilet paper!!! Ajiulize kina Shonza, na mwenzio na hata akina Nakaaya wako wapi siku hizi!!! Hata kwa kazi za sanaa kachuja maana alidharaulika!!! Ukimwona kwa sasa Nakaaya kazeeka kuliko bibi yangu.
 
Na dhambi ya ubaguzi ni mbaya kuliko chochote, Ukishazoea kula nyama ya binadamu hutaacha - Nyerere

Kama mwandishi na ambaye aliona CDM kina ubaguzi kilichomfanya akae CDM tangu 2004 ni kitu gani??? Mambo yalivyotoka hadharani ndipo anakiponda!!!! Maneno ya mkosaji hayo!!! Aende SSM akasimame katika majukwaa kama mamluki wenzio na hakun kitu!!!! Hivi kina M7 na lile kundi la Zito liko wapi kwa sasa??? Dead!!! Chezea CDM wewe. Hivi huwa najiuliza Zitto Kabwe akiwa katika vikao vya chama anathubutu kuanfalia watu usoni!!! Hana soni huyu!!
 
Hapa nashangazwa sana,pengine moderators wata take a note on this.

Umetumia neno "ubaguzi" ili tu kukipaka matope chama cha chadema na kukipa sura mbaya mbele za macho ya wanananchi.

Kiukweli malalamiko yake ni kwamba kina profesa Baregu,Dr Mkumbo et al,wanasikilizwa kuliko yeye.Sasa chama kina ubaguzi gani hapo kama kuna viongozi ambao maoni yao yanasikilizwa zaidi?

Pengine angekuwa mjanja,basi angewatumia hao viongozi "wanaosikilizwa" kufikisha hoja,hao wanaosikilizwa,na si kujitetea kwa usaliti wa wazi kabisa.Sanasana wewe mwenyewe ndo ulijipindua ukaweka na linki ya computer yako...ukaumbuka.

Mleta hoja heading yako ni ya kipotoshaji,elezea ubaguzi wa chadema kwa kutumia muktadha wa hoja ya thread hii.
 
Na dhambi ya ubaguzi ni mbaya kuliko chochote, Ukishazoea kula nyama ya binadamu hutaacha - Nyerere
Hata Nyerere kuna viongozi alikuwa akiwasikiliza na kuna wengine alidiriki hata kuwaita "wahuni",na wasiliti wengine hata nchi walikimbia chini ya utawala wake.Mfano wako ni irrelevant kama ilivyo kwa heading ya thread hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…