PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 444
- 618
Mgombea wa Urais wa JMT kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amesema endapo atapewa ridhaa ya kuunda Serikali katika kipindi kijacho cha miaka mitano, moja ya vipaumbele vyake vikuu itakuwa kufanya utafiti mkubwa wa maeneo yenye madini nchini ili kuongeza mchango wa sekta hiyo katika uchumi wa taifa na ustawi wa Watanzania.
Akizungumza leo, Jumapili Oktoba 12, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika wilayani Mbogwe, mkoani Geita, Samia amesema uamuzi huo unalenga kuongeza maeneo ya uchimbaji na kutoa fursa zaidi kwa wachimbaji wadogo, hasa vijana wa Kitanzania, ambao wengi wao wanategemea sekta hiyo kama chanzo cha ajira.
“Hapa Mbogwe, kipindi hiki cha miaka mitano tunayomalizia, tulianzisha mkoa wa kimadini ili tuweze kusogeza huduma za kimadini karibu na wachimbaji. Tunapokwenda mbele, mkitupa ridhaa, tunakwenda kufanya utafiti mkubwa wa maeneo ya madini. Kama mnavyojua, nchi yetu imepimwa kwa asilimia 16 tu, na hayo ndiyo madini tunayochimba sasa. Tunataka kupima zaidi tujue madini yaliyopo na yapo wapi ili tuyachimbe kwa faida ya Watanzania,”
Ameongeza kuwa, baada ya kukamilika kwa tafiti hizo, kipaumbele cha kwanza cha serikali yake kitakuwa ni kuwaendeleza wachimbaji wadogo, akisema kundi hilo ndilo lenye nafasi kubwa katika kutumia rasilimali za nchi kwa faida ya wananchi wenyewe.