GE2025 Samia: CCM tunataka ushindi wa heshima tuwazibe midomo wale wengine

GE2025 Samia: CCM tunataka ushindi wa heshima tuwazibe midomo wale wengine

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,317
Reaction score
18,493
Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) amewaomba wananchi na wanachama wa CCM kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi la upigaji wa kura Oktoba 29, 2025 ili kukiwezesha chama hicho kupata ushindi wa heshima na wa kishindo.

Dkt. Samia ameyasema hayo Septemba 10, 2025 wakati akizungumza na maelfu ya wananchi wakati wa kampeni za chama hicho wilayani Igunga mkoani Tabora, akiahidi pia kuendelea kuwatumikia kwa juhudi zaidi katika kuwaletea maendeleo.

"Mtakapokuja na ushindi wa heshima kwa jina jingine ushindi wa kishindo wa Chama Cha Mapinduzi tutaweza kuziba midomo wale wengine lakini la pili inapendeza sana kuona wananchi mnajaa sana kwenye viwanja vya mikutano namna hii, sasa idadi iende ikajionesshe kwenye masanduku ya kura vinginevyo wenzetu watatucheka".


 
Simba au yanga vs timu ya shule ya mbugwesembe ni ushindi wa heshima.
 
Hakuna uchaguzi humo ni utapanyaji wa Hela za walala hoi na kupotezeana muda.

Watu walishauri ajitangaze tu yeishee!!
 
Heathrow airport vs mafia airport ni ushindi wa heshima mwambieni mwenyekiti wenu watanzania washaelimika sana wanasubiri njiti ya kiberiti kwenye tank la Petro truck Nepal comes to TZ soon.
 
Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) amewaomba wananchi na wanachama wa CCM kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi la upigaji wa kura Oktoba 29, 2025 ili kukiwezesha chama hicho kupata ushindi wa heshima na wa kishindo.

Dkt. Samia ameyasema hayo Septemba 10, 2025 wakati akizungumza na maelfu ya wananchi wakati wa kampeni za chama hicho wilayani Igunga mkoani Tabora, akiahidi pia kuendelea kuwatumikia kwa juhudi zaidi katika kuwaletea maendeleo. "Mtakapokuja na ushindi wa heshima kwa jina jingine ushindi wa kishindo wa Chama Cha Mapinduzi tutaweza kuziba midomo wale wengine lakini la pili inapendeza sana kuona wananchi mnajaa sana kwenye viwanja vya mikutano namna hii, sasa idadi iende ikajionesshe kwenye masanduku ya kura vinginevyo wenzetu watatucheka”.


 
Ushindi wa heshima utoke wapi wakati uchaguzi wenyewe umekataliwa? Wale wapinzani feki nao ni wa kuwatambia kuwashinda. Walau chadema ingeshiriki halafu uishinde huo ushindi kidogo ungeonekana wa heshima, ila hawa kina mwalimu, gombo na wapuuzi wenzao hakuna ushindi wa heshima hapo
 
Ushindi wa heshima dhidi ya mamluliki wako uliowahonga magari ya kifahari ya kuzugia mtaani, huku mpinzani halisi wa kukunyoosha eti unamtengenezea kesi ya mchongo!!

Mambo mengine yanatia aibu na pia kustaajabisha.
 
Ukisikia kuchanganyikiwa ndiyo huku!

Huo ushindi wa heshima utapatikana kwa njia gani wakati washindani wako unawateka, unawaua, unawapoteza, unawasingizia kesi za uwongo, unaunda Tme huru ya uchaguzi fake, kila kitu ni ushetani mtupu!

Huu ni uchaguzi wa aibu na wa hovyo kuliko uchaguzi wowote ambao umewahi kufanyika katika nchi hii. Ni aheri hata ule uchaguzi wa mfumo wa chama kimoja.

Huu hauna sifa hata 1% ya kuitwa uchaguzi.
 
Back
Top Bottom