Samatta wa sasa ni fursa kwa DStv

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
5,365
2,000
DStv inaonyesha ligi ya England, EPL. Samatta kuchezea EPL kutaongeza watanzania ambao wataangalia EPL kwaajili ya kumuona kijana wao Samatat. Hii itaongeza wadau wa DStv, hivyo huu ni muda wa DStv kuangalia upya bei za vifurushi vyake ili watu wengi zaidi hata vijijini wamudu kulipia na kuangalia mechi za EPL kama ilivyo kwa Azam ilivyoenea hata vijijini kwasababu ya ligi ya Tanzania.
 
MERCIFUL

JF-Expert Member
Oct 17, 2011
2,245
2,000
Hebu jiongeze na wewe, huko vijijini wanaweza kulipa Tsh. 109,000 kwa mwezi kununua kifurushi?
Wana mpaka vifurushi vya elfu 19,000 / 26,500 / 29,000 ila nadhani chaneli ambayo hua inaonyesha EPL (SS3) haiko kwenye vifurushi hivi vitatu.
Wafanye mpango ili mechi za AVFC ziwe zinaonyeshwa pia kwenye vifurushi hivi!
 
MERCIFUL

JF-Expert Member
Oct 17, 2011
2,245
2,000
Inasemekana DSTV wapo kwenye hali mbaya sana. Watu wanaangalia TBC1 kwa kuwa ni ya bure na hawalipii vifurushi.
Mie mteja wao wa kifurushi cha 19,000 na TBC1 ipo humo
Kiufupi ni kwamba sekta ya tv,radio, magazeti na ving'amuzi ipo katika hali mbaya sana. Watu mpira wanaangalia kwenye vibanda,bar na kwenye mtandao , wanaacha dstv nyumbani haijalipiwa ni mwendo wa TBC1.
Mkuu, hayo maeneo yote kama yanaonyesha EPL kupitia SS3 basi bado hio ni ya DStv. Najua wapenzi wa EPL ambao nyumbani wana DStv lakini bado wataenda Bar kuangalia mechi!
 
Faru Kabula

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
12,697
2,000
DStv inaonyesha ligi ya England, EPL. Samatta kuchezea EPL kutaongeza watanzania ambao wataangalia EPL kwaajili ya kumuona kijana wao Samatat. Hii itaongeza wadau wa DStv, hivyo huu ni muda wa DStv kuangalia upya bei za vifurushi vyake ili watu wengi zaidi hata vijijini wamudu kulipia na kuangalia mechi za EPL kama ilivyo kwa Azam ilivyoenea hata vijijini kwasababu ya ligi ya Tanzania.
Mahitaji yakiongezeka kuliko bidhaa, bei hupanda. Hapo ni kama unawachochea wapandishe bei, heri ungekaa kimya
 
Akilindogosana

JF-Expert Member
Jan 12, 2020
665
1,000
Mie mteja wao wa kifurushi cha 19,000 na TBC1 ipo humo

Mkuu, hayo maeneo yote kama yanaonyesha EPL kupitia SS3 basi bado hio ni ya DStv. Najua wapenzi wa EPL ambao nyumbani wana DStv lakini bado wataenda Bar kuangalia mechi!
Upo sahihi, ila asilimia kubwa ya watu hawalipii kabisa.

Halafu watu wanapoangalia mpira bar au kwenye kibanda maana yake watu wengi wameacha kulipia nyumbani kisha wanaenda kuangalia tv ya king'amuzi kimoja, nadhani hapo umepata picha kamili. Angalia tangazo la dstv la "watu wapo wapi?" Hilo tangazo linafikisha ujumbe kwa njia ya kificho kwamba Acheni kuangalia mpira bar na kwenye vibanda sisi huku tuna hali ngumu sana, angalizia mpira nyumbani.

Huko nyuma dstv walikuwa na pesa na walikuwa hawajitangazi sana. Ila kwa sasa wanapambana kujitangaza kwa nguvu zote, kushusha bei ya vifurushi na bei ya king'amuzi.
 
kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
5,365
2,000
Wana mpaka vifurushi vya elfu 19,000 / 26,500 / 29,000 ila nadhani chaneli ambayo hua inaonyesha EPL (SS3) haiko kwenye vifurushi hivi vitatu.
Wafanye mpango ili mechi za AVFC ziwe zinaonyeshwa pia kwenye vifurushi hivi!
ni ushauri wa bure kwao
 
kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
5,365
2,000
Mahitaji yakiongezeka kuliko bidhaa, bei hupanda. Hapo ni kama unawachochea wapandishe bei, heri ungekaa kimya
Mkuu kuna uhusiano mkubwa kati ya demand, supply na price. Kama purchasing power ni ndogo demand na supply havifui dafu. Wale fungulia mbwa viwanjani ni mfano halisi wa effect ya low purchasing power kwenye demand and supply.

Lazima DStv waitafute equilibrium ya demand, supply and price haraka hasa kwenye hii awamu ya tano.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom