Baada ya Krisimasi naomba tufanye soga zisizokuwa na hapa wala pale.
Najua Mh. Raisi atakuwa amesisitiza kuwa samani mpya za ikulu zinunuliwe hapa hapa Tanzania lakini basi wabongo tujitahidi kidogo katika matengenezo.
Licha ya kuwa rangi ya haya masofa hainivutii (earthtones, kama rangi ya ugoro ingefaa zaidi) lakini huu ufanisi wa matengenezo umekaa kama ni wa wanafunzi wa kutengeneza samani. Angalia hiyo misumari inayomeremeta ilivyokuwa haiko kwenye mstari ulionyooka.
Kwa kifupi utengenezaji wake ni dhaifu sana hivyo kwamba mimi, pamoja na umasikini wangu huu, ningepewa hayo makochi bure ningechukua shingo upande.
Ikulu jamani tuwaunge mkono wajasiriamali wa kibongo lakini tusisitize ufanisi. Unadhani ni nchi gani ya jirani itakayokuja Tanzania kununua samani za ikulu yao zinazoonekana kama hizi.
Haya, punguzeni shibe ya x-mass kwa maoni yenu.
****************************************************
NYONGEZA
Tunachokionesha hadharani ikulu ni tangazo kwa dunia nzima kuhusu ufanisi wetu katika tasnia mbalimbali.
Makochi ya ikulu ni tangazo la tasnia ya useremala na upambaji (upholstery) wa samani hapa Tanzania. Tuwe makini na tunavyojitangaza.
Kama mimi ningekuwa katibu mkuu bwana Ombeni Sefue ningefanya hivi:
Ningemuuliza Rais kama anapendezwa na makochi yaliyopo sasa ikulu.

- Akisema "Haya yanafaa kabisa na sitaki kusikia kitu kingine", basi nitaufyata.
- Akisema nakuachia wewe uitangaze hii tasnia duniani, basi nitawaita watengenezaji wote wa samani Tanzania na kuwapa changamoto waje na design zao nzuri, na itakayoshinda itaipamba ikulu. Kampuni itayaoshinda ikishirikiana na Interior decorator/designer wa ikulu, First Lady, na pengine na Rais itatuletea makochi ya ikulu yatakayoitangaza tasnia hii ulimwenguni.