Samaki waliokufa ufukweni Dar, hawakufa kwa sumu - Waziri

Kuna tatizo na tatizo niliona mwanzoni tuu baada ya wao kuhamia eneo la tukio wao walipelekewa sampo na mpeleka sampo anasema tusubiri majibu kutoka kwa wataalamu wakati samaki wanaendelea kuokotwa baharini...Nchi ngumu sana hii
 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki ametoa ripoti ya uchunguzi wa samaki walionekana wakizagaa katika fukwe za Hospitali ya Aga Khan na Ocean Road, akisema hawakufa kwa sumu.

Tukio la samaki kilogramu 164 kuonekana kuzagaa katika maeneo hayo lilitokea Julai 21 mwaka huu, ambapo Serikali ilichukua sehemu ya sampuli ya samaki hao kwa ajili ya kupeleka maabara kuzifanyia uchunguzi huku 156 zikiteketezwa.

Katika maelezo yake, Ndaki amesema katika uchunguzi wao walibaini aina tisa samaki hao waliokuwa wamezagaa ambao ni kui, mkizi, janja, tambanji, chaa, kuku bahari, kolekole pandu, kaa, kambamiti na kambakochi.

“Kwa ujumla, samaki hawa hupatikana kwenye kina kifupi cha maji na wengi wao walikuwa wachanga. Sehemu kubwa ya matumbo ya samaki hayakuwa na chakula, ingawaje kui, mkizi na tambanji walikutwa na dagaa, kaa na uduvi katika matumbo yao.

“Samaki waliochunguzwa walikuwa na hali nzuri, ngozi ilikuwa haikutatuka na ikiwa na rangi angavu, macho yao yalionekana meusi na angavu, na mapezi yalikuwa angavu bila utelezi. Walikuwa na nyama imara na hakukuwa na harufu mbaya,” amesema Ndaki katika mkutano wake na wanahabari leo Jumatano Julai 28, 2021 Dodoma.

Ndaki amesema hatua hiyo inaondoa uwezekano wa vifo vyao vimetokana na sumu au vilipuzi. Hata hivyo, samaki wengi walionekana kuwa na midomo wazi kuashiria kuwa walikosa hewa au walikufa wakitafuta hewa.
Kwa nini walikosa hewa?...why.?..sio kitu cha kawaida...huyu waziri anapenda mteremko sana kwa hiyo uchunguzi uliofanyika ndio huu..
Tanzania ina vichekesho sana
 
Back
Top Bottom