Samaki waelea ufukweni Dar. Serikali yachunguza chanzo…

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
42,591
2,000
Kama kuna watu wanaandaa chakula kichafu ni mama ntilie, kuna siku nilimuona mmoja anaosha vyombo kwa kutumia maji ya mvua yanayotiririka chini.

Ni kweli Mkuu ,Wengi USafi ni Zero ,Maji wanayooshea vyombo hawabadilishi ,ni hayo hayo kuanzia asubuhi vyombo wanavyosuzia vibakuli vya supu mpaka usiku,maji yamejaa sabuni yupu! Muhudumu wa chakula ana toothpick anajichokonoa mdomoni anaishika shika akitoka hapo hanawi mikono anaenda moja kwa moja kukuhudumia!
 

Kyokola

JF-Expert Member
Sep 5, 2014
1,408
2,000
Naamini katika mazingira hao ni kwamba wamekufa,

Hivi kweli mtu unakuta samaki kafa mwenyewe unabeba ukalee???
Huku ni kuendekeza njaa kulikopitiliza,

unafika nyumbani na lijibesi lako unajifanya umetoka kununua samaki kumbe umeokotaaa, ukiua familia???
Eti familia imelazwa au imekufa(yote hatuombei yatokee) kisa pelege????

Hofu yangu ni hao samaki kuingizwa kitaa na kuuzwa. Maana raia tunanunua tu pasipo kujali. Ukikuta wamepangwa utachagua tu pasipo kujua kama wameokotwa na hawajavuliwa.
 

Isanga family

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
8,934
2,000
Mpo busy kuandika barua mara sijui sample imepekekwa huku ishu ya emergency kwa maisha ya watu ilitakiwa jana hiyo hiyo kuwe na majibu...huku wananchi wakiendelea kuwaokota na kuwauza..
 

gigabyte

JF-Expert Member
May 27, 2015
2,191
2,000
Hilo tumezoea kule ziwani, kuna kipindi samaki hasa sangara huwa wanaelea, ni kwenda kukamata tu unaenda na kitoweo nyumbani bila nyavu yaani. Wenyewe wanasema wanakuwa wamekosa hewa ya kutosha ndani ya maji ila kwa baharini sina experience.
Sawa kabisa.hicho kipindi wanaita kiferezi.ata mwaka huu mwezi wa pili na tatu walikufa sangara wengi sana.
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
170,188
2,000
Maeneo ya Ufukwe wa Bahari kuanza nyuma ya Hospital ya Agha Khan, viwanja vya Gymkhana mpaka nyuma ya Ikulu kuelekea soko la Feri.

Kuna Samaki wengi wamekufa, wanaokotwa na wananchi na kuelekea soko Feri kuuzwa.

TAHADHALI KWA WANANCHI SAMAKI HAO BADO HAWAJATHIBITISHWA KAMA WANAFAA KWA MATUMIZI YA BINADAMU. NI VIZURI TUKAJUA NINI KILICHOWAUA.

CHUKUENI TAHADHARI.
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
170,188
2,000
Ni vema kuepuka kitoweo cha samaki wa maji bahari kwa siku mbili tatu hizi hasa kutoka kwa wachuuzi mitaani
Mama ntilie
Migahawa na mabanda ya chakula
Michemsho ya samaki kwenye vilabu vya pombe
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom