Samaki Ukishamvua majini..............????? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Samaki Ukishamvua majini..............?????

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Sumba-Wanga, Jan 4, 2012.

 1. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Jana ilikuwa siku ya kwanza ya kazi baada ya mwaka mpya. Kama kawaida wakati wa tea time and hata lunch, colleague hawaachi kulete story za hapa na pale. Basi likaja swala moja ambalo lilileta ubishi na mzozo mkubwa, wanaume wakivuta kwao na wanawake nao wakisema lao. Kuna dada mmoja mwenye ndoa alilalamika kwamba wanaume wengi wanadhani kwamba jukumu lao ni kuoa mwanamke na kumweka ndani, na baada ya hapo ni kuhudumia family kwa mahitaji ya kula, na mavazi., FULL STOP. jukumu jingine la unyumba (ambalo wakina dada walidai kuwa ndio linalowatoa kwa wazazi wao kwenye vitanda na chakula kama kwa waume zao), linasaharika na kupewa umuhimu mdogo. Badala yake, wanaume wengi wanakuwa busy na vimada na mahawara, wanaacha kzai za ndani. Sasa kwa kuwa wanawake nao wanana mahitaji yao ya unyumba, na mume hapatikani, basi ndipo wanapoangukia mikononi mwa serengeti boys/mahawara.

  Kwa kweli hadi mwisho hakukuwa na jibu la kueleweka: wanaume wanadia kwamba samaki ukishamvua kutoka majini hukuna haja tena ya kumpa chakula, na wanawake wanasema hawakufuata chakula na vitanda kwa maana hata walipotoka vipo. Wana JF, mnalionaje hilo?
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 160
  Hili haliwezi eleweka asilani
   
 3. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mhhh hapa tuwasubiri akina dada wanasemaje maana ukisema wewe mwanaume utaambiwa unavutia kwako
   
 4. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135

  Hapana, ni bora kupata mawazo ya both sides; je wanaume wanakubalina na hili, wengi wanaona kuwa jukumu linakwisha pale wanapomweka mwali ndani?
   
 5. huzayma

  huzayma Senior Member

  #5
  Jan 4, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 127
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mie hii ndo kwanza nisikie, mana kule kwetu ukiolewa tu hilo ni jambo la kwanza unaloambiwa, kama mume alikuwa akila, akisafishiwa nyumba hata na ndugu zake na akitandikiwa kitanda, kilichomfanya aje kukuoa hapa ni kushughulika yale ya kitandani kisha hayo mengine yanafata baadae, sasa hao wanaume wa kuoa kwa ajili ya kukulisha ndo nawasikia hapa, ndoa ni kupigwa nao mengine yanafatia , kama mwanaume hakupi vitu hakuna cha kukuweka hapo na hiyo sio ndoa ni ndoano.:embarassed2:
   
 6. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Kwa nini halieleweki Mkuu?
   
 7. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #7
  Jan 4, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Kwangu mimi yote yanatakiw ana yana nafasi yake
  Kuhakikisha kuwa mkeo anapata huduma zote za kifamilia na kindoa maana ndoa haikamiliki bila yale mambo na huwezi kusema ni ndoa kama hakuna yale mambo
  So timiza jukumu kama mwanaume na kama mume na then njoo kwenye familia timiza wajibu kama baba
  Unaona tofauti yake
  Kwenye familia timiza kama baba wa familia na kwenye ndoa timiza kama mume wa mwanamke
   
 8. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #8
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
   
 9. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #9
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mimi nina hakika kama hili lingefanyika, basi wanandoa wengi sana wangepunguza kuwa na sleep less nights.
  Hata idadi ya vimada/mahawara kwa pande zote mbili ingepungua.

  Wakina dada wengi wanadai kuwa waume zao ndio wanaowasababishia kutoka nje: kwa kusahau wajibu wao wa unyumba!
   
 10. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #10
  Jan 4, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  tatizo letu wanaume tunaoa na then tukishawafikisha wake zetu nyumbani tunaona ndo tumemaliza kila kitu
  Kumbe yapo majukumu ambayo yanatakiwa kutekelezwa na kila upande kuhakikisha kuwa ndoa inadumu
  Kuwa na mke si kumpa tuu chakula na nguo na matumizi yake
  Ni zaidi ya hayo na zaidi ni ile haki yake ya kuwa mke wako
  Timiza jukumu lako kama mume na sio mwanaume ndani ya nyumba
   
 11. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #11
  Jan 4, 2012
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Majukumu ya mwanaume/mwanamke kwenye familia yanajulikana vizuri hizo zilizobaki ni sababu zisizo na miguu wa kichwa
   
 12. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #12
  Jan 4, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
   
 13. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #13
  Jan 4, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Nitatoka kwa wazazi wangu na kuambatana na mme wangu kwa 7bu:kupeana raha ya tendo la ndoa kihalali na mtu tunayependana na kuanzisha na kujenga familia yetu kwa ushirikiano na mme wangu.km itashindikana kutimiziana hayo kwa namna zote bac nitafungasha mabegi maana hapo hata upendo hautakuwepo tena,hayo ya vimada na serenget boy ni kujiendekeza tu ila mkitimiziana hayana nafac.
   
 14. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #14
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135


  Yaani, I wish wanaume wenye tabia kama hii wangesikia na kutekeleza haya. Kwa kiasi kikubwa, migogoro ya ndoa ingepungua sana.
  Ndio maana kuna baadhi ya watu watu walikuwa wanadai kwamba WANAUME HAWAPEWI DARASA HASA WAJIBU WAO KWENYE NDOA KABLA YA KUOA.... JAMII INA ASSUME KWAMBA WANAJUA KILA KITU...
   
 15. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #15
  Jan 4, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Umejuaje TF?

  Ukweli ni kwamba kila mtu kwenye ndoa ana majukumu yake...Watu wakubaliane na wayatimize....

  Suala la unyumba ndiyo nguzo ya ndoa...kama haupo au unatolewa kwa kusua sua kama mishahara ya watumishi wa umma basi ndoa inakuwa ikielekea ICU na baadaye kule mortuary!!

  Hilo la samaki...ni kweli na linahusu pande zote mbili...Ukikaa na mtu muda mrefu una-saturate...Ni jukumu la wanandoa ku-revive mahusiano yao kwa mbinu zozote zile...

  Wale wanaojikuta wameanguka na kucheat...basi wawe responsible na wafuate ma ushauri ya wataalamu ikiwemo ile dossier maarufu ya The Boss!!
   
 16. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #16
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Sasa ni kwa nini hayatekelezwi? kwa nini kuna migogoro?
   
 17. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #17
  Jan 4, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180


  :ranger:
   
 18. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #18
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135

  Mmh, nadhani ni rahisi sana kusema kwamba utafunga mabag na kuondoka. Ingakuwa ulaya na America, ningekuelewa kirahisi sana. Ndoa nyingi sana hazina furaha na bado watu wamekaa pamoja. Kama tutafanya sensa ya ndoa zenye furaha hapa JF, na watu wakakubali kusema ukweli wao, we will be shocked.

  Sometime kwenye ndoa, watu wanaishi pamoja kwa mambo mengi zaidi ya kupeana raha.
   
 19. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #19
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Dark City:
  Nimekupata, na nina amini kama kuna watu wamejisahau kidogo, basi watarudi kwenye mstari!
  Hiyo dossier ya the Boss ni ipi hiyo? Tukumbushe tafadhari
   
 20. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #20
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Asha Di: fungua mdomo:biggrin:
   
Loading...