mngony
JF-Expert Member
- Jul 27, 2012
- 5,553
- 6,966
Habarini wanajamvi, kwanza kabisa niwapongeze wale ambao hawalali usiku na mchana kwa kazi kubwa na nzito ya kizalendo kuhakikisha Taifa letu lipo Salama kabisa.
Siku za karibuni kumetokea utenguzi wa teuzi mda mchache sana baada ya mhusika kuteuliwa, mpaka sasa yameshatokea kama matukio 3 au 4 hivi. Sababu ni kinachoonekana ni makosa katika uteuzi, lakini kwa uelewa wangu mdogo teuzi serikalini huwa kuna utaratibu unaojulikana kama Vetting ambao kwa ufupi ni kuangalia kama mhusika anafaa kwa hiyo nafasi, na utaratibu huo hufanywa na Usalama. Sasa ninachoshangaa inakuaje ndani ya mda mfupi teuzi hizo 3 zinaonekana kama hazikufanyiwa huo utaraibu au haikuanyika vizuri au sijui ilikuwaje. Nakubali kuna nafasi ya makosa ya kibinadamu lakini mara 3 ni nyingi ndani ya kipindi cha miezi 6, na hili tukio la mwisho mtu kaingia mpaka Ikulu kimakosa, jambo ambalo kwa uelewa wangu mdogo ni Hatari Kiusalama