Samahani kwa picha hizi sio nzuri, Tumuonee huruma

Samahani kwa picha hizi sio nzuri, Tumuonee huruma

SPANISH CP

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2014
Posts
465
Reaction score
230
Binti Mwanaidi Vuai Salehe amelazwa ktk Hospitali ya jeshi Bububu Zanzibar kwa miezi minne sasa anauguza majeraha ya ajali ya moto.
Hali yake inazidi kua mbaya na anahitajika Tsh Milion 15 aweze kupelekwa India.

attachment.php


Kama uko tayari kumsaidia
A/c 051206007686 PBZ-Malindi.
0773599466-mama yake mzazi-kwa mawasiliano tu.
KUCHANGIA.
TUMA kwa Tigopesa 0715424152-Mwandishi wa habari gazeti la Zanzibar Leo(Othman Maulidi
Ni binti mwenye miaka 26 tuungane kumsaidia.

UPDATES:
Leo jioni Mwanaidi amehamishiwa ktk hospitali ya Mnazi mmoja. Zanzibar

TAARIFA YA MICHANGO:
Mpaka kufikia leo trh 10 jun 14,Michango ya pesa zilizopokelewa ni Tsh 1,900,000/=(milion moja na laki tisa).
Tunashkuru kwa moyo wenu wale waliojitolea kwa hali walichonacho.

Bado tunaendelea na michango tuone wapi tutafikia.
Mwenyezimungu awalipe kwa wema wenu.

LEO TAREHE 15 JUN 14:
Mwanaidi bado yupo Mnazi mmoja hospital kwa wale waliopo Zanzibar tunaomba hata mkafariji na muione hali halisi ya mgonjwa.

Michango inaendelea na huenda wiki ijayo akahamishiwa hospitali ya taifa Muhimbili.

Tunashkuru kwa wanaotuunga mkono ktk harakati hizi za kumsaidia Mwanaidi.

Updates

TAARIFA;
Leo Tarehe 15 july 2014
Ndugu zangu,kwanza tumshkuru Mwenyezimungu kwa kila jambo maana yeye ndiye mpangaji.

Pili naomba niwape taarifa kwamba Mwenyezimungu ameejaalia kupitia michango yenu nyinyi members na msio members wa mtandao huu leo hii ndugu yetu MWANAIDI atasafiri kuelekea India Kupata matibabu.

Tatu,naomba kwa heshma kubwa niwashkuru na niseme ahsante kwa wote mlioguswa na tatizo hili na mkajitolea kwa kadri mlichojaaliwa,ni vigumu kuwataja mmoja mmoja lakini mniwe radhi kwa ujumla wenu nasema AHSANTENI SANA na Mwenyezimungu pekee ndie atawalipa kwa wema huu mlioutenda.

Mwisho,mgonjwa atasafiri leo na ndege ya Oman Air atasindikizwa na mama yake mzazi,pamoja na nesi mmoja kwenda India, Tumuombee dua akapate matibabu yenye kumfaa ili arudi akiwa na afya na siha njema.
"AHSANTENI"

TAARIFA: Leo trh 09 Aug 2014.
Dada yetu Mwanaidi Amerejea kutoka India alikokua anapatiwa matibabu ya majeraha ya moto.
HALI YAKE KWA SASA:
Kwakweli tunamshukuru Mwenyezimungu baada ya operation kadhaa kwa sasa hali yake inaendelea vyema kwa kiasi kikubwa.
Alipo ni Mnazi Mmoja hospital yupo katika uangalizi wa daktari kwa muda kabla ya kuruhusiwa kwenda nyumbani.
Nimeongea na mama yake Mzazi anawashkuru woote kwa ushirikiano wenu wa kufanikisha safari hii na Mwenyezimungu atawailipa.

Nb: ikiwezakana kesho nitaweka picha
 
Picha hiyo
 

Attachments

  • Mwanaid 1.JPG
    Mwanaid 1.JPG
    87.8 KB · Views: 3,714
Picha zingine hizi hapa
 

Attachments

  • Mwanaid 2.JPG
    Mwanaid 2.JPG
    124.6 KB · Views: 3,402
  • Mwanaid 3.JPG
    Mwanaid 3.JPG
    112.1 KB · Views: 15,655
Pole sana mwanaid mungu akupunguzie maumivu na upone haraka
Pia akujalie upate msaada wa mapema kwa matibabu
Inatia huruma!
 
Inatia huruma, hivi serikali mambo kama haya hayana kitengo?
 
Pole sana mhanga wa ajali hiyo ya moto, Mwenyezi Mungu akupe nafuu zaidi. Kwa mara nyingine pole.
 
Pole sana samahani kwa kuuliza ivi chanzo cha ajari ni kipi?wadau mara nyingi wanapenda kupata taarifa ya kina na ndiyo wanashawishika kutoa msaada, kimsingi pole
 
SPANISH CP hana namba ya Tigo.., kuna vijisenti nataka nitume kidogo daaaa!

Namba ya tigo ni hii
0715424152(Huyu ni mwandishi wa habari gazeti la Zanzibar leo) naye amejitolea kuendeleza michango kwa watu mbalimbali naomba umpigie atakupa maelezo ya kina.
AHSANTE KWA KUGUSWA NA HILI NDUGU Yangu.
 
Namba ya tigo ni hii
0715424152(Huyu ni mwandishi wa habari gazeti la Zanzibar leo) naye amejitolea kuendeleza michango kwa watu mbalimbali naomba umpigie atakupa maelezo ya kina.
AHSANTE KWA KUGUSWA NA HILI NDUGU Yangu.

Ngoja namrushia tu.., asipofikisha kivyake coz laana itamfuata.., jina limekuja Othman maulid.., i hope ndo yeye.., tutume chochote tulichonacho jamani.., hata buku itasaidia coz si tupo wengi..
(Update: Amenipigia kwamba kaipata na ataifikisha)
 
Dah..pole yake na kwa wanaomuuguza! tunashukuru kwa namba mkuu!
 
Ngoja namrushia tu.., asipofikisha kivyake coz laana itamfuata.., jina limekuja Othman maulid.., i hope ndo yeye.., tutume chochote tulichonacho jamani.., hata buku itasaidia coz si tupo wengi..

Ndio huyohuyo mtumie tu Othman Maulidi naamini atafikisha,
Shukran Ndugu chochote ulichotoa Mwenyezimungu akupe zaidi.
 
Hivi UKAWA hawawezi kulibeba hili jamani?
cc Dr.Wilbroad Slaa, Kurugenzi ya Habari

Samahani ndugu hili jambo sikulileta hapa ktk misingi ya siasa,dini wala ukanda.
Huyu binti ni binadamu mwenzetu anamatatizo magubwa na umaskini ndo unamtesa kitandani kwa miezi minne sasa.
Kama umeguswa na maradhi yake toa chochote kama huna basi hata kauli nzuri ingefaa.
Samahani tuungane kumsaidia
 
Last edited by a moderator:
Pole sana Binti Nitakuweka kwenye Maombi yangu leo
 
Back
Top Bottom