Samahani kwa picha hizi sio nzuri, Tumuonee huruma

Samahani kwa picha hizi sio nzuri, Tumuonee huruma

Pole yake Mwanaidi.
Ila wangewahi na mitishamba hali yake isingefikia level hii.
Asali mbichi ya ukweli sio makangaja ya mjini ukichangaya na Unga wa Kasha la Konokono sio wa Baharini na wala sio aliye hai ,lazima iwe ya Muda.
Amini usi amini ukipaka kwenye kidonda Ndani ya siku 3-5 unaanza kupata majibu kidonda!



Ama kweli watu wengine kweli mkuu habari kama hii kuchanganywa na stori kama hii inaumiza.
https://twitter.com/TzNews70


YAANI ndugu nilivyoona hiyo picha ya MWANAIDI na story waliyoitungia ktk huo mtandao hadi machozi yalinitoka,kwanini binadamu tunakosa busara kiasi hiki
 
Taarifa:leo Trh 29/06/2014.
1.Habari zakutia moyo Ni kwamba kuna msamaria amejitokeza wa kugharamia tiketi za mama yake na nesi mmoja kwenda na kurudi India.

2.Za kusikitisha ni kwamba kuna mtandao mmoja(tznews 70) Kupitia Ukurasa wao wa facebook walitoa picha hizo za MWANAIDI na kuzitungia story kwamba huyo ni mwanachuo wa chuo Mkoani Iringa amechomwa moto kwa tuhuma za wizi.
Jamani hawa wenzetu walichokifanya si jambo jema hata kidogo.

3.Kwa Mara nyingine niwashkuruni nyote mnaondelea kujitolea kwa moyo kutokana kuguswa na shida ya ndugu yetu Mwanaidi.

mkuu hiyo ni 'simple defamation case' , wakati mnashughulikia matibabu nashauri mzungumze na mwanasheria ili kuona kama kuna kesi na jinsi gani Mwanaidi atakua adequately compensated.
 
Pole sana..Naamini Mungu uneyemwamini atakuponya hapo itachukua mda ila usivunjike moyo
 
Inatia huruma, hivi serikali mambo kama haya hayana kitengo?

mkuu serkal yetu ione hivihivi, yaan ni bora hata ukipata tatizo bora uombe msaada kwa watanzania,kuliko system pole sana B mwanaid
 
Mkuu SPANISH CP angalia pm kuna maagizo nimekupa.
 
mkuu serkal yetu ione hivihivi, yaan ni bora hata ukipata tatizo bora uombe msaada kwa watanzania,kuliko system pole sana B mwanaid


Yaani haki ya nani vile haya mambulula yanaona bora kutibu wanaojidunga madawa ya kulevya kwa starehe zao, lakini mtu kama huyu ambae ni ajali (bahati mbaya) haya habari hayana kazi kugawana mafungu tu,,,

Na walaaniwe wote

Pole sana mama yangu!
 
Habari nimechelewa kuiona leo 1/07 bado ipo valid?
 
Habari nimechelewa kuiona leo 1/07 bado ipo valid?

Ndio habari iko hivyo,mpaka leo ndugu yetu mtanzania mwenzetu ana miezi minne sasa yupo hospital,wataalam wamempa rufaa apelekwe India tatizo lililopo upatikanaji wa pesa hizo milion 15.
kuna wasamalia wamejitolea tiketi 3 kwa ajili ya mgonjwa,mama yake,na nesi atakaewasindikiza kwenda na kurudi huko India.
Kama umeguswa na una chochote ndugu basi changia kwa
tigopesa-0715424152(Othman Maulid-mwandishi na mpiga picha wa gazeti la Zanzibar Leo.
 
TAARIFA;
Leo Tarehe 15 july 2014
Ndugu zangu,kwanza tumshkuru Mwenyezimungu kwa kila jambo maana yeye ndiye mpangaji.

Pili naomba niwape taarifa kwamba Mwenyezimungu ameejaalia kupitia michango yenu nyinyi members na msio members wa mtandao huu leo hii ndugu yetu MWANAIDI atasafiri kuelekea India Kupata matibabu.

Tatu,naomba kwa heshma kubwa niwashkuru na niseme ahsante kwa wote mlioguswa na tatizo hili na mkajitolea kwa kadri mlichojaaliwa,ni vigumu kuwataja mmoja mmoja lakini mniwe radhi kwa ujumla wenu nasema AHSANTENI SANA na Mwenyezimungu pekee ndie atawalipa kwa wema huu mlioutenda.

Mwisho,mgonjwa atasafiri leo na ndege ya Oman Air atasindikizwa na mama yake mzazi,pamoja na nesi mmoja kwenda India, Tumuombee dua akapate matibabu yenye kumfaa ili arudi akiwa na afya na siha njema.
"AHSANTENI"
 
samahanini lakin hii picha inafanana na yayule mvulana wa RUCO aliyechomwa moto plz sina nia mbaya
 
Nimetuma kiasi kidogo, Mungu amfanyie wepesi.

CC: SPANISH CP
 
Last edited by a moderator:
samahanini lakin hii picha inafanana na yayule mvulana wa RUCO aliyechomwa moto plz sina nia mbaya

Kwania njema kabisa naomba ufanye hesabu ifuatayo,
thread hii nimeiandika na kuambatanisha na picha ya Mwanaidi trh 9june 2014,
Tukio La kuchomwa moto mwanachuo lilitokea nadhani kati ya trh 27 au 28 June sasa jiulize kipi ktk matukio hayo mawili kilitangulia?

Kiufupi ni kwamba watanzania wanaopenda kuchukulia matatizo ya wenzao kama sherehe kwao, Mtandao Wa Tznews ulitoa habari ya kuchomwa moto mwanachuo huko Iringa,ni Kweli tukio lilitokea ila wakaona ili wanogeshe habari yao na ivutie kwa wasomaji ndipo wakaingia jf na kuichukua picha hiyo ya Mwanaidi Na kuiambatanisha na habari yako.

Nilisikitika sana kwa kitendo walichofanya mtandao huo.
 
Serikali sikivu taf sikiliza okoa maisha ya mpiga kura.
 
Back
Top Bottom