Sam Mahela leo dakika 45 umeshindwa kabisa kuongoza kipindi

Sam Mahela leo dakika 45 umeshindwa kabisa kuongoza kipindi

Msigwa ameulizwa maswali yakaiwada kabisa anashindwa kujibu.Ni aibu kwa mbunge kutopenda kusoma kichwani mweupe
Ukweli unaujua ila umeona bora uwe mnafiki ili watoto wako waende chooni kama wewe ni mkweli ebu sema swali gani ameulizwa na ameshindwa kulijibu na kila mwenye macho ameona wapinzani walivyo na uwezo wa kujenga hoja
 
Waandishi wa habari wa hapa nyumbani wana upungufu/udhaifu mkubwa sana kwenye mahojiano ya ana kwa ana.

Huwa naangalia namna ambavyo jirani zetu (kenya) wanavyofanya kama kwenye kipindi cha "Big Question" huwa wanahoji vizuri sana bila kujali anayehojiwa ni nani.

pata muda angalia KTN au Citizen TV utaona namba ambavyo wanahoji kwa wererdi huku wakiweka hisia zao pembeni.
 
nimemshangaa sana msigwa kubeza uwepo wa majeshi yetu DRC! yaani hajui manufaa ya jeshi letu kuwepo DRC kweli? au aliamua kujitoa ufahamu! basi kama hajui nchi hii tunawabunge wa ajabu sana.
Of what economic gain to us? Ndiyo ilikuwa concern us Msigwa. Tupe jibu
 
Hiki kipindi kilitakiwa kipate presenter aina ya STEPHEN JOHN SACKUR wa BBC hardtalk.Hawa waliopo wanakiendesha chini ya kiwango,hiki kinatakiwa kuwa kipindi cha kuongelea serious issues kinyume na inavyofanyika sasa hivi.
Perfect vyuo vyenyewe vya waandishi ndio hivyo
 
Hata mimi alinishangaza sana! Hii si kawaida yake - lakini kwa mahojiano na Mh.Msigwa nimeona kuna mambo fulani alikuwa hataki ayaseme - sasa alimkaribisha Mh.Msigwa studio akiwa na lengo gani - mbona viongozi wa chama tawala wakija kwenye studio za ITV uzungumza freely bila ya kuwa interrupted unnecessarily.

Safari hii SAM ameonekana alipania kumbana bana Msigwa - a proffessional journalist kama SAM hapashwi kuwa mwoga au kuogopa lawama hicho ndicho nilicho kiona kwenye mahojiano yake na Msigwa - SAM was visibly jumpy!!

Watanzania wana uwezo mkubwa wa kutambua kama wanao karibishwa kwenye Studio kwa mahojiano ni wakweli au wababaishaji, hivyo SAM hana sababu yakuwa na wasi wasi kwamba labda jamaa akijibu ndiyo sivyo hiyo inaweza kumwingiza matatani yeye kama host wa kipindi, cha muhimu hapa muhusika aonywe mapema kwamba hasitukane watu au kutumia lugha hisiyo ya kistaarabu wakati wa mahojiano basi.
Amesoma kiwango gani na wapi chuo gani
 
Nimekua nikifuatilia kipindi hiki kinachorishwa na ITV maarufu Dakika 45. Huyu jamaa Sam Mahela wakati akifanya mahojiano na mwaalikwa asilimia 50% mzungumzaji ni Sam Mahela mwenyewe.

Katika maadili ya habari, hurubusiwi kutoa maoni yako hasa wakati wa kufanya mahojiano (un-opinionated). Huyu Mahela akiguswa tu Mfano Magufuli, utamsikia akimtetea kwa nguvu zote eti huyu Rais kaleta mabadiliko makubwa sana na mm nimefanya utafiti mikoa saba Tanzania na kwamba magufuli anakubalika.

Mfano katika kipindi cha leo akihojiana na Msigwa, huyu Mahela, alizungumza zaidi kuliko mualikwa, alijibizana nae kana kwamba yeye ni msemaji wa CCM au wa serikali ya Magufuli. Alimhakikishia kuwa Magufuli anakubalika sana na yeye alifanya tafiti na viongozi wa dini na vyama vya siasa vinamkubali. Pathetic.

Alienda mbali zaidi kwamba kila alichokua anasema Msigwa yeye humjibu "Wasema wewe, Mimi sijasema"! Sasa najiuliza huyu KANJANJA vipi, ama ni wakala wa CCM ndani ya DK 45 au anamfurahisha mfalme....

Wadau mtakumbuka aliekua anaendesha kipindi hiki huko nyuma ni Buhohela, na kwasasa amepata ugali wake (kazi) magogoni (Ikulu). Huyu Mahela naona nae amepatamani huko na sharti amfurahishe mfalme!

Huo ni Ukanjanja na njaa Kali...Aibu! Shame on you MAHELA.
Well said. Binafsi nina wasiwasi na mtangazaji huyu kama ana kiwango cha kutosha cha elimu ya uandishi wa habari (broadcasting). Nilimsikiliza akifanya mahojiano na waziri wa elimu prof. Joyce Ndalichako kwa kweli nilisikitika sana. Kwa kifupi anaaibisha taaluma. Huo ndio ukweli. Mimi ninashauri ITV wamsaidie ama kwa mafunzo ya ndani (in house training) au wampeleke chuoni akajiendeleze. Na kama amesoma lakini bado anafanya kazi zake kwa namna hiyo, basi, wamwache tu abaki kusoma taarifa ya habari na si kuendesha kipindi kama hicho cha Dakika 45!
 
Huyu jamaa sijui vp sijui mi namuonaga anajiuliza na kujijibu mwenyewe
Na kucheka cheka ovyo Kama jemsi delicious aisee
Me simuelewagi kabisa huyu jamaa
 
sasa kama umeangalia kipindi kwa dakika 45 ukashindwa kuona udhaifu wa mahela, hapa hata uelekezwe htaelewa(......)ungekuwa mjinga ingekuwa rahisi ufundishwe mpk uelewe!hata ile chekacheka ya kienyeji huku muarikwa akiwa katikati ya mazungumzo nayo inahtaji kwenda darasani!?
 
Acha tumwambie aliboa sana hasa mimi kwan.ukimuuliza mtu swali acha ajibu.siyo kuuliza maswali ukitarajia jibu unalolipenda wewe.
 
Huyu mtangazaji wa hiki kipindi kwa kweli ni kero sana, anachekacheka kinafiki, anaonyesha upande katika mahojiano, nashauri abadilishwe pia yupo the yule Ufosaro kwny malumbano ya hoja, wanakera mpaka tunaacha kuangalia vipindi vyao, kila mara wanawaingilia wachangiaji wa mada ambao wanajaribu kuikosoa serikali, pia muda wa wachangiaji hautoshi (malumbano).SAM MAHELA amekeraa kipindiki hakina mvuto tena.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom