Dakika 45 ITV, Sam Mahela haiwezi

kipuyo

JF-Expert Member
Jul 30, 2009
1,785
1,464
Kipindi hiki huwa hewani kila jumatatu baada ya taarifa ya habari mpaka mida ya saa nne usiku.
Kipindi hiki kilipata umaarufu zaidi enzi za mtangazaji mmoja aliyekuwa kwenye timu ya kampeni za Magufuli kipindi kile cha uchaguzi Mkuu wa 2015.
Kwa sasa kipindi kinaongozwa na jamaa mmoja anayeitwa Sam Mahela,kusema ukweli kipindi kwa sasa hakina mvuto.
Maswali anayauliza yeye na maelezo anayatoa yeye,sasa najiuliza kuna haja ya kumuita MTU?
Yaani mara nyingine anaboa mbaya,swali lina maelezo kibao,unafikiri insha.
Anauliza swali,kabla ya kujibiwa anajijibu mwenyewe
Yapaswa abadilike kurudisha heshima ya kipindi.
 
Kwahiyo unataka tumpe nani hiki kipindi?

kwanza tangu kilivyokua ni recorded sio mubashara tena nikaachana nacho mazima nimewaachia wengine
 
Angalau buhohela kuliko mahela

Nakubali, Mahela anapwaya zaidi, ni mnazi sana. Mara nyingi huegamia kwenye itikadi kumsaidia mgeni kujibu kipropaganda. Semenyu alikuwa anauliza maswali yanayolenga jamii nzima ya watazamaji. HAKUWA NA UVYAMA, HAKUWA MUONYESHA KUTAKA KITU KWA WAGENI NA UTAWALA...!! Nasikitika kuseam tangu aondoke Semunyu sina furaha sana na kipindi hicho...!!

Tafakari...!!
 
kwanza tangu kilivyokua ni recorded sio mubashara tena nikaachana nacho mazima nimewaachia wengine
Hata Mimi nilipoona kimeanza kuwa recorded sijawai umiza kichwa shida nyingine wanaitwa wanasiasa nikimaanisha mawaziri most of the time kwanini asiitwe headmaster wa shule iliyokuwa ya mwisho kitaifa na Afisa elimu wake
Au madawa kwa sasa hospital ni janga la kitaifa aitwe DMO moja na katibu mkuu wizara hayo ni mapendekezo na kipindi kiwe live
 
Watangazaji wengi Elimu SIFURI, UPEO Hafifu, Mishahara duni, Ubunifu Dhaaifu = MAJANGA PLUS.
 
Yaani kipindi cha Jana ndo kaniboa kabisa Sam Mahela anafaa kuwa repota tu sio kukaa studio
 
Anajikunja kama vile studio kuna baridi, nadhani hata studio hawapo huru...

studio inatakiwa iwe na library ya maana, iwe kama ofisi, maswali yawe machache ila very heavy, pia waulizwaji waruhusiwe kujibu kwa ushahidi wa namna yeyote sio kama jana, NW alikuwa kama vile anafanyiwa usaili wa kazi au ngazi na Huyo mtangazaji mwenyewe alikuwa hayupo comfortable yaani ni kama alikuwa anajiangalia kwenye kioo.

ITV ni nzuri, boresheni mazingira ,umaridadi huficha umaskini
 
Tangu aondoke SEMUNYU hicho kipindi kilipoteza mtu muhimu na aliyekuwa anajua kuuliza maswali kulingana na mgeni wa siku hiyo. Hata Buhohela alipwaya sana...!! SEMUNYU WAS THE BEST...!!

Tafakari...!!

Selemani Semunyu alikuwa hovyo kuliko wote,Buhohela ndo alikuwa alikuwa afadhali kuliko wote waliowahi kuendesha hicho kipindi.
Hicho kipindi kilikuwa kinamfaa mtu kama Jerry Murro ama Rainfred Masako
 
Back
Top Bottom