BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,831
- 287,784
Saluni' za kuchua zashamiri Dar
Waandishi Wetu
Daily News; Sunday,March 16, 2008 @00:02
*Yadaiwa mabalozi na mawaziri ni wateja wakubwa
*Zimeweka mabinti kwa ajili ya ngono
*Gharama kwa huduma ni kati ya 10,000/- na 50,000/-
BAADHI ya saluni zinazotoa huduma za kuchua na kukanda mwili maarufu kama ‘massage salon' zimegeuka madanguro, imefahamika. Saluni za aina hiyo zimekuwa zikiruhusu huduma ya kukanda hata maeneo ya siri huku wahudumu wake wakiwa tayari kufanya ngono na mteja yeyote kwa muda unaolingana na fedha inayotolewa na mteja.
Uchunguzi uliofanywa na HabariLeo Jumapili kwa wiki kadhaa umegundua kuwa baadhi ya saluni hizo ambazo awali zilikuwa zinaendesha huduma za kunyoa nywele na kusafisha uso maalumu kwa wanaume, nyingi sasa zimejikita katika kutoa huduma ya masaji katika eneo lolote la mwili analotaka mteja. Lakini pia kuna saluni nyingine ambazo ni maalumu kwa ajili ya kuchua na kukanda mwili tu.
Zote hizo zinatoa huduma zinazofanana katika kufanya masaji, huduma inayoonekana kupendwa na watu wa rika zote katika Dar es Salaam wakiwamo watu wenye fedha na watu wanaoheshimika katika jamii.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo, saluni za namna hiyo nyingi ziko Sinza, Kijitonyama na Kinondoni. Baadhi ya wahudumu wa saluni hizo wamethibitisha kuwa wana wateja wengi wa rika mbalimbali wakiwamo watu wenye nyadhifa kubwa katika mashirika na taasisi za serikali wakiwamo mawaziri.
Waandishi wetu wamegundua kuwa huduma za masaji zinazofanywa katika saluni hizo zinaenda mbali zaidi na mara nyingi huishia katika kufanya tendo la ngono.
Katika saluni moja iliyoko Kinondoni mhudumu alimweleza mwandishi kuwa kuna aina tatu za masaji zinazofanywa katika saluni hiyo.
Ambazo ni hard massage, medium massage na soft massage. Kwenye saluni hiyo huduma zinatofautiana. Kwa mteja anayetaka kufanyiwa masaji kwa nusu saa atachajiwa Sh 5,000, saa moja Sh 10,000 na huduma hiyo itakuwa ni kwa mwili mzima isipokuwa sehemu za siri. Lakini mteja ambaye anahitaji huduma ya kufanyiwa masaji sehemu za siri baada ya masaji ya mwili mzima anatozwa Sh 5,000 zaidi.
Pia kuna huduma ya ngono kwa mteja ambaye anaona anashindwa kujizuia wakati anafanyiwa masaji hiyo na gharama zake katika saluni hiyo inaanzia Sh 20,000. Katika suluni nyingine ambayo huduma ya kufanyiwa masaji saa moja gharama zake ni Sh 10,000. Lakini kwa mteja anayetaka kufanyiwa masaji ya sehemu za siri atalazimika kulipa tena Sh 10,000 aweze kufurahia huduma hiyo.
"Kuna huduma nyingine kaka kama utashindwa kujizuia ni ya kufanya mapenzi. Usijali gharama yake ni maelewano tu lakini kiasi cha chini ni Sh 30,000," alisema dada mmoja mrembo wakati anatoa maelezo kwa HabariLeo Jumapili.
Mwandishi wetu mmoja alionyesha kushtuka baada ya kutajiwa kiasi hicho kwa kufanya ngono na ndipo akajibiwa na mhudumu huyo kuwa: "Kaka hicho ni kiasi cha chini hapa watu wanatoa hadi Sh 50,000 kwa tendo moja tu la ngono kulingana na uwezo wa mtu."
Saluni zilizoko Sinza zinaonekana za gharama kidogo maana masaji zinazofanywa huko zimegawanywa tofauti tofauti. Mteja anayetaka kufanyiwa masaji ya mwili mzima kwa saa moja anatozwa Sh 20, 000. Mmoja wa wahudumu wa saluni moja iliyoko Sinza alimweleza mwandishi wetu kuwa huduma kwa masaji ya mgongo ni Sh 10,000.
Masaji ya miguu Sh 10,000 wakati masaji ya sehemu za siri ni Sh 15,000. Mhudumu huyo alithibitisha kuwa kwa vile masaji zinafanywa kwenye maeneo ya siri kati ya msichana na mwanaume, wakati mwingine huduma hiyo inaishia kwenye kufanya ngono kutokana na wanaume wengi kushindwa kuvumilia.
"Mteja akitaka kufanya tendo la ndoa niko tayari, inategemea na yeye atalipa kiasi gani cha fedha na kama nitaridhika nacho sina jinsi…hayo ndiyo maisha yetu," alisema mhudumu huyo. Labda cha kufurahisha ni kwamba wasichana wengi wanaofanya kazi kwenye saluni hizo wanatambua udhaifu wa wateja wao na wengi wao huwa wana kondomu ili mteja anayetaka huduma ya ngono aridhishwe.
"Kaka tunazo kondomu humu ndani kwa hiyo usihofu kama unataka wewe tuelewane tu," alisema mhudumu mmoja kwa mwandishi wetu.
Saluni za namna hiyo pia ziko katika baadhi ya maeneo ya Kijitonyama ambako huduma zake zinafanana na saluni za Kinondoni ambako bei yake si ya juu kama ilivyo kwa Sinza.
Gazeti hili limegundua kuwa mteja anayeenda kufanyiwa masaji kwa muda mfupi anazoeana na mhudumu kutokana na mteja kuvua nguo zote na kubaki uchi wa mnyama kusubiri huduma hiyo. Katika saluni moja kunakuwa na vyumba vidogo vidogo kwani kila mteja anakuwa katika chumba chake na mhudumu, na mlango hufungwa hadi mteja anaporidhika na huduma aliyopewa.
Mhudumu mmoja alipoulizwa kama wanapata wateja wa kutosha alijibu: "Wateja ni wengi na wengi wao ni mabalozi, mawaziri, watu wazito na wafanyabiashara maarufu".
Alisema kuwa vigogo wengi wanakwenda kwenye saluni hizo kwa siri kubwa ili familia zao zisijue kama wanaenda kufanyiwa masaji.
"Lakini mabalozi wao wako huru wakati wowote wanakuja. Si unajua mambo haya katika nchi zao sio mageni kama ilivyo hapa kwetu?" alisema mhudumu mwingine wa saluni ya Kinondoni.
Mmoja wa wahudumu wa Sinza alisema wateja wao wengi ni vijana wa kiume ambao wanaonekana kupenda huduma hiyo. Alisema wanawake ni wachache. Kwa ujumla wahudumu wengi waliohojiwa na waandishi wetu walikiri kuwa wateja wao wengi ni wanaume ambao wanaonekana kufurahia huduma ya kufanyiwa masaji katika maeneo hayo.
Mhudumu mmoja alisema kwa wateja ambao hawataki kwenda kwenye saluni hizo wana huduma maalumu za kumfuata mteja nyumbani kwake ili mradi mteja huyo awahakikishie kuwa atalipa zaidi.
"Ni lazima malipo yake yawe zaidi kwani kwenda kwake unatumia usafiri, hivyo ni lazima na yeye alipe zaidi," alisema mhudumu huyo. Aliongeza kuwa huduma ya Sh 10,000 katika saluni kwa mteja anayetaka akafanyiwe nyumbani kwake atalipa Sh 30,000.
Huduma za masaji zimekuwa zinafanywa katika hoteli kubwa maarufu kwenye vitengo vya Casino, lakini kwa sasa huduma hizo zimetapakaa katika saluni nyingi za Dar es Salaam.
Baadhi ya watu waliohojiwa na HabariLeo Jumapili walisema kuwa ingawa huduma hiyo imeongeza ajira kwa wasichana wengi, lakini pia inakiuka maadili katika jamii ya Mtanzania.