Saluni za "kuchua" zashamiri Dar

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,005
Saluni' za kuchua zashamiri Dar
Waandishi Wetu
Daily News; Sunday,March 16, 2008 @00:02

*Yadaiwa mabalozi na mawaziri ni wateja wakubwa
*Zimeweka mabinti kwa ajili ya ngono
*Gharama kwa huduma ni kati ya 10,000/- na 50,000/-

BAADHI ya saluni zinazotoa huduma za kuchua na kukanda mwili maarufu kama ‘massage salon' zimegeuka madanguro, imefahamika. Saluni za aina hiyo zimekuwa zikiruhusu huduma ya kukanda hata maeneo ya siri huku wahudumu wake wakiwa tayari kufanya ngono na mteja yeyote kwa muda unaolingana na fedha inayotolewa na mteja.

Uchunguzi uliofanywa na HabariLeo Jumapili kwa wiki kadhaa umegundua kuwa baadhi ya saluni hizo ambazo awali zilikuwa zinaendesha huduma za kunyoa nywele na kusafisha uso maalumu kwa wanaume, nyingi sasa zimejikita katika kutoa huduma ya masaji katika eneo lolote la mwili analotaka mteja. Lakini pia kuna saluni nyingine ambazo ni maalumu kwa ajili ya kuchua na kukanda mwili tu.

Zote hizo zinatoa huduma zinazofanana katika kufanya masaji, huduma inayoonekana kupendwa na watu wa rika zote katika Dar es Salaam wakiwamo watu wenye fedha na watu wanaoheshimika katika jamii.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, saluni za namna hiyo nyingi ziko Sinza, Kijitonyama na Kinondoni. Baadhi ya wahudumu wa saluni hizo wamethibitisha kuwa wana wateja wengi wa rika mbalimbali wakiwamo watu wenye nyadhifa kubwa katika mashirika na taasisi za serikali wakiwamo mawaziri.

Waandishi wetu wamegundua kuwa huduma za masaji zinazofanywa katika saluni hizo zinaenda mbali zaidi na mara nyingi huishia katika kufanya tendo la ngono.

Katika saluni moja iliyoko Kinondoni mhudumu alimweleza mwandishi kuwa kuna aina tatu za masaji zinazofanywa katika saluni hiyo.

Ambazo ni hard massage, medium massage na soft massage. Kwenye saluni hiyo huduma zinatofautiana. Kwa mteja anayetaka kufanyiwa masaji kwa nusu saa atachajiwa Sh 5,000, saa moja Sh 10,000 na huduma hiyo itakuwa ni kwa mwili mzima isipokuwa sehemu za siri. Lakini mteja ambaye anahitaji huduma ya kufanyiwa masaji sehemu za siri baada ya masaji ya mwili mzima anatozwa Sh 5,000 zaidi.

Pia kuna huduma ya ngono kwa mteja ambaye anaona anashindwa kujizuia wakati anafanyiwa masaji hiyo na gharama zake katika saluni hiyo inaanzia Sh 20,000. Katika suluni nyingine ambayo huduma ya kufanyiwa masaji saa moja gharama zake ni Sh 10,000. Lakini kwa mteja anayetaka kufanyiwa masaji ya sehemu za siri atalazimika kulipa tena Sh 10,000 aweze kufurahia huduma hiyo.

"Kuna huduma nyingine kaka kama utashindwa kujizuia ni ya kufanya mapenzi. Usijali gharama yake ni maelewano tu lakini kiasi cha chini ni Sh 30,000," alisema dada mmoja mrembo wakati anatoa maelezo kwa HabariLeo Jumapili.

Mwandishi wetu mmoja alionyesha kushtuka baada ya kutajiwa kiasi hicho kwa kufanya ngono na ndipo akajibiwa na mhudumu huyo kuwa: "Kaka hicho ni kiasi cha chini hapa watu wanatoa hadi Sh 50,000 kwa tendo moja tu la ngono kulingana na uwezo wa mtu."

Saluni zilizoko Sinza zinaonekana za gharama kidogo maana masaji zinazofanywa huko zimegawanywa tofauti tofauti. Mteja anayetaka kufanyiwa masaji ya mwili mzima kwa saa moja anatozwa Sh 20, 000. Mmoja wa wahudumu wa saluni moja iliyoko Sinza alimweleza mwandishi wetu kuwa huduma kwa masaji ya mgongo ni Sh 10,000.

Masaji ya miguu Sh 10,000 wakati masaji ya sehemu za siri ni Sh 15,000. Mhudumu huyo alithibitisha kuwa kwa vile masaji zinafanywa kwenye maeneo ya siri kati ya msichana na mwanaume, wakati mwingine huduma hiyo inaishia kwenye kufanya ngono kutokana na wanaume wengi kushindwa kuvumilia.

"Mteja akitaka kufanya tendo la ndoa niko tayari, inategemea na yeye atalipa kiasi gani cha fedha na kama nitaridhika nacho sina jinsi…hayo ndiyo maisha yetu," alisema mhudumu huyo. Labda cha kufurahisha ni kwamba wasichana wengi wanaofanya kazi kwenye saluni hizo wanatambua udhaifu wa wateja wao na wengi wao huwa wana kondomu ili mteja anayetaka huduma ya ngono aridhishwe.

"Kaka tunazo kondomu humu ndani kwa hiyo usihofu kama unataka wewe tuelewane tu," alisema mhudumu mmoja kwa mwandishi wetu.

Saluni za namna hiyo pia ziko katika baadhi ya maeneo ya Kijitonyama ambako huduma zake zinafanana na saluni za Kinondoni ambako bei yake si ya juu kama ilivyo kwa Sinza.

Gazeti hili limegundua kuwa mteja anayeenda kufanyiwa masaji kwa muda mfupi anazoeana na mhudumu kutokana na mteja kuvua nguo zote na kubaki uchi wa mnyama kusubiri huduma hiyo. Katika saluni moja kunakuwa na vyumba vidogo vidogo kwani kila mteja anakuwa katika chumba chake na mhudumu, na mlango hufungwa hadi mteja anaporidhika na huduma aliyopewa.

Mhudumu mmoja alipoulizwa kama wanapata wateja wa kutosha alijibu: "Wateja ni wengi na wengi wao ni mabalozi, mawaziri, watu wazito na wafanyabiashara maarufu".

Alisema kuwa vigogo wengi wanakwenda kwenye saluni hizo kwa siri kubwa ili familia zao zisijue kama wanaenda kufanyiwa masaji.

"Lakini mabalozi wao wako huru wakati wowote wanakuja. Si unajua mambo haya katika nchi zao sio mageni kama ilivyo hapa kwetu?" alisema mhudumu mwingine wa saluni ya Kinondoni.

Mmoja wa wahudumu wa Sinza alisema wateja wao wengi ni vijana wa kiume ambao wanaonekana kupenda huduma hiyo. Alisema wanawake ni wachache. Kwa ujumla wahudumu wengi waliohojiwa na waandishi wetu walikiri kuwa wateja wao wengi ni wanaume ambao wanaonekana kufurahia huduma ya kufanyiwa masaji katika maeneo hayo.

Mhudumu mmoja alisema kwa wateja ambao hawataki kwenda kwenye saluni hizo wana huduma maalumu za kumfuata mteja nyumbani kwake ili mradi mteja huyo awahakikishie kuwa atalipa zaidi.

"Ni lazima malipo yake yawe zaidi kwani kwenda kwake unatumia usafiri, hivyo ni lazima na yeye alipe zaidi," alisema mhudumu huyo. Aliongeza kuwa huduma ya Sh 10,000 katika saluni kwa mteja anayetaka akafanyiwe nyumbani kwake atalipa Sh 30,000.
Huduma za masaji zimekuwa zinafanywa katika hoteli kubwa maarufu kwenye vitengo vya Casino, lakini kwa sasa huduma hizo zimetapakaa katika saluni nyingi za Dar es Salaam.

Baadhi ya watu waliohojiwa na HabariLeo Jumapili walisema kuwa ingawa huduma hiyo imeongeza ajira kwa wasichana wengi, lakini pia inakiuka maadili katika jamii ya Mtanzania.
 
Hii inabidi isomeke "UWANJA WA FISI WAHAMIA MAENEO RASMI- KTK MASALUNI"
Nina swali, hizo huduma za ziada ziko formally arranged na wenye salon au ni kabiashara ka hao wahudumu 'on the side'?
Ushauri wa bure kwa wanawake wenye waume/wachumba, mjifunze kufanya massage kwani hata hao wasichana si professional masseuse
 
Hii inabidi isomeke "UWANJA WA FISI WAHAMIA MAENEO RASMI- KTK MASALUNI"
Nina swali, hizo huduma za ziada ziko formally arranged na wenye salon au ni kabiashara ka hao wahudumu 'on the side'?
Ushauri wa bure kwa wanawake wenye waume/wachumba, mjifunze kufanya massage kwani hata hao wasichana si professional masseuse

Kwi kwi kwi!

Hata wakijifunza kuchua na kutomasa Haitasaidia kitu.

Tabisa ya wanaume malaya ni sawa na mpishi mwenye tabia ya kununua 20kg ya nyama kwa mtindo wa kunua 1/2 kilo kila Bucha.

Pamoja na ukweli kwamba nyama ni ileile kila bucha ina vimbwanga vyake vya kukata nyama na kuipackage.

Sasa sijui wake zetu nao wakienda huko wanapata wana serengeti wa kuwapa huduma hiyo kipimo cha uvumilivu kikivunjika?
 
Kwi kwi kwi!

Hata wakijifunza kuchua na kutomasa Haitasaidia kitu.

Tabisa ya wanaume malaya ni sawa na mpishi mwenye tabia ya kununua 20kg ya nyama kwa mtindo wa kunua 1/2 kilo kila Bucha.

Pamoja na ukweli kwamba nyama ni ileile kila bucha ina vimbwanga vyake vya kukata nyama na kuipackage.

Sasa sijui wake zetu nao wakienda huko wanapata wana serengeti wa kuwapa huduma hiyo kipimo cha uvumilivu kikivunjika?

You never know inawezakana kabisa kukawa na wanaserengeti wanaojua kuifanyia massage nanino....:) Wewe utaona safari za kwenda saloni kuchuliwa zinaongezeka. Baba nanihii, mimi naenda saluni kuchuliwa maana nasikia mwili wote unauma...:) nitakawia kurudi maana kunakuwa na wateja wengi
 
Woooh, good news. Kuna watu na heshima zetu tulikuwa hatuwezi kwenda 'kuchuliwa' Kinondoni makaburini. Na kama hizi sehemu zinaongezeka ina maana competition itaongeza ubora wa huduma na kushusha bei kwa wateja which is a good thing. Na hii ni hatua kubwa kuelekea kwenye uhalalishwaji wa biashara ya mwili na madanguro, at the moment the government is losing lots of tax on this business kwa kuwa income wanayopata dada zetu ni kubwa sana.
Maendeleo sio ujenzi wa barabara na zahanati tu!
 
Tunalilia amendeleo, lakini inaelekea maendeleo yatatuletea mengi hata yale tusiyo yataka.

Kwa hiyo nikisikia dada shangazi au mama yangu mdogo kafungua au anafanya kazi ya kuchua natakiwa kuelewa ni nini hasa anaongelea?

Siyo nakwenda kwenye hadhara na kutamba "Tangu mama yangu mzazi aanze kazi ya kuchua hali ya famila yetu kifedha imekua. Nisijue namdharirisha mama yangu na mimi mwenyewe vilevile.

Na zile club za kunengua na kusaula viwalo bado hazijaanza?
 
Woooh, good news. Kuna watu na heshima zetu tulikuwa hatuwezi kwenda 'kuchuliwa' Kinondoni makaburini. Na kama hizi sehemu zinaongezeka ina maana competition itaongeza ubora wa huduma na kushusha bei kwa wateja which is a good thing. Na hii ni hatua kubwa kuelekea kwenye uhalalishwaji wa biashara ya mwili na madanguro, at the moment the government is losing lots of tax on this business kwa kuwa income wanayopata dada zetu ni kubwa sana.
Maendeleo sio ujenzi wa barabara na zahanati tu!
Sana...
Tatizo letu ni kuwa mambo haya tunayaepanda lakini tunaogopa kuyaweka wazi. Kwa wanasiasa imekuwa ni sehemu yao ya kupata ujiko kwa kupiga marufuku nyingi, na hata kuwafunga wakinadada zetu ili tu waonekanae ni watu wenye maadili
 
.....maendeleo yana raha na karaha...ni kweli hizi huduma zipo ......na there you find WHO IS WHO IN THIS COUNTRY....NIMESHUHUDIA..lakini uzuri ni kuwa wanaume wengi wana siri ..kwa hiyo unayoyakuta hapo unayaacha hapo hapo ...siri za jandoni...ndio maana ..na offcourse si jambo la ajabu......tatizo linaza pale massage inapofanywa hata kwa shilingi 5,000...ni bei ndogo mno hii itasababisha hata watoto wadogo waanze kwenda massage...ndio maana hawawezi kuvumilia...hata haitoshi kununua mafuta maaalum i guess wanatumia lotion za kawaida....

massage ni moja ya taaluma za heshima na muda mrefu duniani......na isichukuliwe kila anayeenda massage anafuata ngono..nataka tu kusema wengi wa watu wazima wanaoenda massage wanafuata hilo tu!!!!......na ukienda kwenye hotel kubwa usije ukadhubutu kumtamkia binti anayefanya massage upuuzi wa sex ..she can sue you!.....ile ni kazi kama kazi nyingine....
 
Ni kweli massage parlours katika nchi zilizoendelea wanafanya massage kama professionals, na ukimtamkia mhudumu mambo ya ngono hamtaelewana na atatafsiri kuwa umemdharau. Lakini nchi hizo hizo ambazo umalaya ni marufuku, wameruhusu wasichana warembo wanaojiita "professional escorts" (wapo pia wanaume mabaunsa katika biashara hiyo) ambao hutoa huduma za "company" kwa wageni, wafanyabiashara au mtu yeyote anayehitaji kusindikizwa mahali au kwenye social event. Kwenye matangazo yao wanaandika wazi kuwa hawafanyi biashara ya ngono, lakini wanaongeza kuwa kwa kuwa escort na mteja wake ni "consenting adults", basi lolote la ziada likitokea baina yao ni hiari yao na si sehemu ya malipo aliyotoa mteja kwa huduma ya "escort".

Hayohayo ya "consenting adults" yanatokea katika massage parlours hasa za nchi kama Thailand na Singapore ambako pia wanadai wamepiga marufuku umalaya. Ukiingia unaambiwa hapa ni massage parlour na sio danguro, huna haki ya kudai ngono kutokana na malipo uliyotoa ya kufanyiwa massage, lakini mkielewana vyovyote vingine na mhudumu wako ni juu yenu kwa kuwa ninyi ni consenting adults. Basi watu wameutumia mwanya huohuo kugeuza massage parlour karibu zote kwenye nchi hizo kuwa danguro, na massage parlour ni biashara inayolipa sana kule. Mwanaume anayeingia anakuja na hela fungu mbili, ya kwanza analipa kwa cashier kwa ajili ya huduma ya massage, akifika chumbani anaelewana na mhudumu kuwa anahitaji ngono kwa hiyo anamlipa lile fungu lingine. Wahudumu wa hizo massage parlours wanalipwa mishahara kidogo sana na waajiri wao, wengine hawalipwi kabisa, kwa kuwa hela wanayopata toka kwa wateja ni nyingi sana.

Hiyo kama imeingia bongo, basi tayari ni umalaya umehalalishwa "kiaina" kama uzoefu ulivyoonesha katika nchi nilizotaja. Sijui kama "professional escorts" nao wameshaingia bongo, lakini nilikwenda Uganda mwaka jana nikawakuta Kampala, tena ofisi zao ziko ndani ya jengo linalomilikiwa na chama tawala cha NRM, karibu na geti la kuingilia Mengo hospital. Wanasema ni biashara halali kabisa, na wanadai hawajihusishi na biashara ya ngono, lakini wanakuambia ukielewana hivyo na escort ni juu yenu. Ukiingia ofisini unapewa fomu ujaze details zako, anwani na namba ya simu, na aina ya escort unayemtaka (umri, jinsia, mwonekano wake, tabia nk), halafu unalipa ada shilingi 20,000 za Uganda (kama USD 11 hivi). Itategemea sifa ulizotaja, wakipitia katika data base yao wakimuona mtu anayeendana nazo wanakupigia simu uje ofisini wawakutanishe, ukiridhika nae, naye pia akiridhika nawe, wanawasainisha, unalipa 20,000 nyingine unaondoka na mtu wako, biashara na hao agents imekwisha, yatakayobaki utajuana na mtu wako sasa. Nilifika kwenye hiyo ofisi nikakuta waheshimiwa waliokuja kwenye conference ya wiki nzima wako pale wanatafuta escorts za kudumu nazo wakati wa conference, wengine walikuwa watalii nk, na wanadai ni salama sana mtu huyo hawezi kukufanyia ubaya maana ni traceable. Mie nilikuwako for 2 weeks, nilipata escort pia na alinisaidia sana kuujua mji. Alikuwa mwalimu wa shule ya sekondari, na ile alikuwa anafanya kama starehe yake, kwa hiyo jioni akitoka shule ananifuata hotelini nilikofikia tunapanga pa kutembelea siku hiyo na kadhalika, lakini gharama zote kwa mujibu wa makubaliano ni juu yangu (hatukufanya ngono, wala sikuonesha dalili za kuhitaji, nae wala hakunishawishi, ingawa nilivyomwona kwa muda niliokaa nae ingekuwa rahisi sana kupata hiyo kama ningehitaji). Ilikuwa wajibu wangu kumlipia usafiri wa kurudi nyumbani kwake na kuja tena kesho yake, na kila siku nilikuwa nampa USh 10,000 kwa ajili ya kukodi "special" (ndivyo taxi zinavyoitwa kule Kampala), lakini mwenyewe akishazichukua alikuwa anadandia "bodaboda" (pikipiki) ambayo gharama si zaidi ya 1,000. Akili kumkichwa!

Utandawazi unatuvamia kwa kasi na namnukuu mwalimu wangu mmoja: "we have opened up too wide" (yaani "tumepanua" mno!)
 
kithuku umenifurahisha..we have opened too wide really..na rais mstaafu mzee mwinyi anakuambia yeye alifungulia madirisha yoote ..sasa waliingia inzi ,nyuki,mbu,ndege wazuri wacheche......sasa ni jukumu la tawala zinazofuata kuondoa hizo inzi..kila zama na kitabu chake"""

massage za bongo nyingi hata zile exclussive kiasi wanapigwa mkwara wa sex na ukimujaribu anakupa anwani ya nyumbani kwake sanasana ...atakupigisha punyeto...

ila zile za hood kila kitu kweli ni poa ...uzuri wana kondomu..lakini kwa kuwa sasa zimeingia hood na bei ni ndogo ..hofu yangu ni hawa watoto wetu wanaobalee..si unajua stage hiyo wengi tunakuwa domo zege..na zamani tuliponea kwenye ma housegirl au mama hurumas.hadi tukajua kutongoza..siku hizi itakuwa terrible maaana vijana wa kiume hawajifunzi kutongoza wanaishia kuchukua changudoas na sasa hii huduma imekuwa cheap ni hatari vijana wadogo wakianza kwenda massage..nashauri serikali idhibiti ..huduma hii ibakie kwenye specified clubs,au gyms au casino ambazo zina memberships na watoto wadogo hawaruhusiwi...
 
Tatizo ya hizo saluni za kuchua maowner wanaajili machangudoa na si wajuzi wa kazi hiyo, kwa hiyo wanakuwa pale kwa nia ya kutafuta customer, we jaribu kuuliza wamepatia wapi ujuzi wa kuchua usikie! Na pia hawa wanaume wanaotaka ngono mi naona hawaendi kwa nia ya kuchua ila wana lao jambo!

Mi naona TZ tuige sheria za sweden/Nerthaland kwamba kuwa changudoa si kosa, bali kosa ni kwa yule anayelipa pesa ili kupata sex kwa kuwa amemfanya binadamu kama commodity kwa kumnunua ili apate kiburudisho, kwa hiyo tukiweza kuwakamata hawa wanaume wanaonunua sex hopefuly hawa wanaojiuza watakosa customer na wataamua kujihusisha na shughuli za maendeleo zaidi na kuacha kukaa kwenye saluni kusubiri wateja.
 
Kithuku kweli hukuomba huduma hata kidogo? Joke

Lakini jamani lazima tukubali, dunia imebadilika mnooo. hatuwezi kutegemea serikali idhibiti kila kitu. Hivi tunafikiria serikali ni nani? si ndo hawa hawa watu wa utandawazi wamesoma na kuyaishi haya maisha? au tunadhani kwamba ukishakuwa waziri basi unakuwa mtu tofauti.

My point is, the world has changed the best we can do is to regulate the regulatables! kitu kama massage utakicontrol vipi? labda sema upitishe sheria ya kuregulate hiyo industry na maadili ya kufuata kama alivyoeleza muungwana Kithuku na wengine..such as escort.....

Anyway all in all mambo siku hizi yanaenda faster sana.

Kingine inabidi wanawake huko manyumbani wawajibike kuwafanyia wazee wao haya mambo..maana wasipokuwa watundu, mzee ataogopa kuuliza kwa kuogopa kuitwa muhuni na badala yake ataenda kwa vibinti vidogo kufanya mambo! Well sijui kama wanawake nao wanafanyiawa!

Jamani things are changing....we live in interesting times!
 
Tatizo ya hizo saluni za kuchua maowner wanaajili machangudoa na si wajuzi wa kazi hiyo, kwa hiyo wanakuwa pale kwa nia ya kutafuta customer, we jaribu kuuliza wamepatia wapi ujuzi wa kuchua usikie! Na pia hawa wanaume wanaotaka ngono mi naona hawaendi kwa nia ya kuchua ila wana lao jambo!

Mi naona TZ tuige sheria za sweden/Nerthaland kwamba kuwa changudoa si kosa, bali kosa ni kwa yule anayelipa pesa ili kupata sex kwa kuwa amemfanya binadamu kama commodity kwa kumnunua ili apate kiburudisho, kwa hiyo tukiweza kuwakamata hawa wanaume wanaonunua sex hopefuly hawa wanaojiuza watakosa customer na wataamua kujihusisha na shughuli za maendeleo zaidi na kuacha kukaa kwenye saluni kusubiri wateja.
THIS SOUNDS PRACTICAL....! JANA USIKU I SAW CITY AUXILLIARY POLICE WAKIKAMATA MACHANGUDOA PAMOJA NA WATEJA WAO (kona baa,kili muda,machenii,k/ndn etc)......!PUNGUFU NILILOLIONA NI KUWA WANAOKAMATWA NI WALE WASIOWEZA KUTOA CHOCHOTE....WALIOKUWA WAKITOA WALIACHIWA.......!(I eyewitnessed this) HIVYO BADO MULE MULE KUNA MAFISADI WAKUBWA NA WADOGO HATA KATIKA KUJENGA MAADILI....!
 
Hii inabidi isomeke "UWANJA WA FISI WAHAMIA MAENEO RASMI- KTK MASALUNI"
Nina swali, hizo huduma za ziada ziko formally arranged na wenye salon au ni kabiashara ka hao wahudumu 'on the side'?
Ushauri wa bure kwa wanawake wenye waume/wachumba, mjifunze kufanya massage kwani hata hao wasichana si professional masseuse
Hiyo ni 2008 sijui siku hizi hali itakuwa vp?!
 
Back
Top Bottom