1. Unaenda saluni kuongea ama kutengeneza unachotaka kutengeneza? Mi hua nashangaa sana watu wanavyopayuka hovyo badala ya kutulia wakimaliza kilichowapeleka warudi majumbani kwao.
Ila bado sijui hiyo inaweza ikavunja vipi mahusiano ya mtu mwenye akili zake timamu.
2. Matokeo ni kucha zinapendeza, yakiwepo mengine basi yanatokana na hulka ya mtu na sio kwasababu tu kapakwa rangi na mkaka.
3. Again, kama mtu anaongozwa na mawazo ya ngono hata anaebahatisha kukaa nae kwenye daladala anaweza akamtaka na akimpata anamchukua. Pili, kwa wanaume ambao wameoa nadhani vitu vingine ni vizuri wakawaomba wake zao wawafanyie. Itaongeza ukaribu kati yao, na akinogewa na kuoshwa kichwa anamalizia mahitaji yake kihalali.
4.Kupigwa sound kuna tatizo gani? Sound zinapigwa na vinyozi tu? Mdada ambae yuko avarage (muonekano na umbo) lazima apigwe sound sehemu na watu tofauti tofauti, hamna anaeweza kuzuia hilo. Ishu ipo kwenye mhusika kukubali ama kukataa, na kama atamkubali kinyozi jua fika angeweza akamkubali yeyote yule kati ya wanaomfuata hivyo ishu sio kuwa kinyozi bali ni mtu kuwa 'anapatikana'.
NB. Kama mtu anahitaji kuona/kuhisi mwenzake anamjali na hali ikawa tofauti na hivyo ni rahisi sana(japo sio haki) kuanguka kwa anaeonyesha kujali hata kama wewe hapo utaona hana hadhi sijui. Hivyo muhimu ni watu kutimiza majukumu yao. . . sio wanabweteka alafu wanabaki kulia lka baadae.
Kwanza sipendelei kwenda saluni hizo, Pili, sijui kwenu wanaume, for me as woman. Mwanaume wa anyefanya kazi saluni ya wanawake yaani hanitii tamaa hata siku moja, namwona kama ******/hanisi au mwanamke mwenzangu vile.
Yaani nahisi walost their masculine part....sorry thats me.
Kinachotokea hapo ni effects za continuous service. Huyo wa daladala ni one time and may not have
any effect. lakini wewe fikiri kwamba mumeo kila siku ankwenda saluni flani na anaoshwa na
mwanadada flani! Uwezekano wakutegwa kutokana na ukaribu unaojengwa kwa huduma
inayotolewa ni mkubwa sana. Hulka ya mtu inachangia lakini mazingira pia yanahusika kubadilisha
mtizamo wa mtu. . . .
Hulka ya mtu ndio kila kitu. . .hata kuwe na continuity sijui kitu gani kama mtu hulka yake sio kuruka ruka kila kona hatofanya hivyo. Wanaofanya hivyo hata wasingekuwa na hao wanaowapa huduma wangechukuana na watu wengine huko mitaani bila kujali hayo uliyoongelea mwanzo.
Kuaminiana ni vyema! Sasa hutakiwi uamini tuu blindly hata pale ambapo kuna factors zinazoweza
kukushawishi otherwise.
duh, na maofisini je?
Kuna clients ambao kila siku waongea nao
kuna msekretaru ambao kila siku wanakuandalia chai, cha mchana, kupanga ratiba, kuhakikisha uko proper kimwonekano
utakuwa na wa ngapi?
Hiyo ni hulka tu, hata ufungiwe ndani utaangua hata tango kwenye friji.
Nikuulize, utamruhusu mmeo/mkeo kufanya kazi saloon majukumu yake yakiwa ni kuwapatia massage
wateja?