Uchaguzi 2020 Salumu Mwalimu: Biashara zote za Serikali kubinafsishwa

Ukiwa na sera nzuri mashirika yataendeshwa kwa ufanisi mkubwa sana! Na hapo kwenye sera ndipo serikali ya CCM imefeli vibaya
Acha ujinga, mngekuwa na sera basi mngeshajenga ofisi ya makao makuu. Mbona mlishindwa kusimamia pesa za visima zilizotolewa na Sabodo hadi akakatisha na kuwanyima jengo la CINEMAX pale ITV Mwenge. Mmesgindwa kusimamia ruzuku ndio maana wabunge wengi wamewakimbia.
 
Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi amemnukuu Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais Chadema akieleza sera ya Chama chao kuwa ni kubinafsisha biashara zote ili ziendeshwe na sekta binafsi.
Amesema Serikali itabaki na jukumu la kutunga Sera tu.

My Take:
Nadhani upo umuhimu wa wataalamu kuwasaidia vyama vya siasa na wagombea mambo muhimu na yaliyotafitiwa ya kuyaongelea kwenye kampeni.
Kodi waliahidi hawatakusanya, na sasa wanaahidi kubinafsisha biashara za serikali, matapeli hawa
 
Acha ujinga, mngekuwa na sera basi mngeshajenga ofisi ya makao makuu. Mbona mlishindwa kusimamia pesa za visima zilizotolewa na Sabodo hadi akakatisha na kuwanyima jengo la CINEMAX pale ITV Mwenge. Mmesgindwa kusimamia ruzuku ndio maana wabunge wengi wamewakimbia.
Sera siyo ofisi wala majengo!
 
Wanasiasa huwa mara nyingi wanaongea vitu katika mtazamo wa kisiasa na sio katika uhalisia Kuna vitu wanavozungumza havina uhalisia kabisa
Hili suala linamtatiza sana hata Faroukh Karim wa ITV, Zanzibar. Jana alilazimika kuliuliza kwenye press conferences.
 
Wewe upo juu sisi tupo juu katikati na chini.
Hivi TTCL ilikuwa hoi kwa sababu gani na imerudi kuwa hai kwa sababu gani?
Hiyo TTCL bado iko hoi taaban. Kinachosemwa sicho unachokijua kwa undani. Na uongo ndiyo imekuwa nguzo muhimu kwa awamu hii. Subiri nitaweka humu jamvini taarifa muhimu kuanzia wiki ijayo ndipo utagundua kuwa una serikali ya aina gani
 
Hapo ndio mashirika yote nyeti yataangukia mikononi mwa mabeberu, na kutuendesha yanavyotaka!

Tutapiga magoti, watatuendesha, na watapata kila wanachokitaka, maana wao ndio watakuwa wameshikilia mpini!.

Wanaowashangilia hawa wanasiasa nakuwaona ndio wakombozi wao, binafsi huwa nawaona, somewhere kumkichwa hakuko vizuri!.
 
Ukiwa na sera nzuri mashirika yataendeshwa kwa ufanisi mkubwa sana! Na hapo kwenye sera ndipo serikali ya CCM imefeli vibaya
Ha ha ha wenye Sera nzuri nani?. Hiki Chama cha Mbowe?. I see, haupo serious kabisa. Wao wenyewe wanashindwa kuweka Sera nzuri, juu ya mapato na matumizi ya saccos yao itakuwa ya mashirika ya umma?. Hawa watu ni watafunaji, watanzania tusikubali hata nukta ulaghai wao.
 
Hiyo TTCL bado iko hoi taaban. Kinachosemwa sicho unachokijua kwa undani. Na uongo ndiyo imekuwa nguzo muhimu kwa awamu hii. Subiri nitaweka humu jamvini taarifa muhimu kuanzia wiki ijayo ndipo utagundua kuwa una serikali ya aina gani
Ipo hoi wakati mimi najiunga JF kupitia TTCL?
Mitandao yote inachukua bando TTCL.
 
Hapo ndio mashirika yote nyeti yataangukia mikononi mwa mabeberu, na kutuendesha yanavyotaka!

Tutapiga magoti, watatuendesha, na watapata kila wanachokitaka, maana wao ndio watakuwa wameshikilia mpini!.

Wanaowashangilia hawa wanasiasa nakuwaona ndio wakombozi wao, binafsi huwa nawaona, somewhere kumkichwa hakuko vizuri!.
Wote wanao ona wamepata Mkombozi ni kama vipofu vile. Wengi hawaoni mbali, na huendeshwa kwa matumbo yao tu. Kwa mustakabali wa ustawi wa mama Tanzania, Sera za chama cha Mbowe ni sumu kwa taifa wala sio mbolea.
 
Hatuwezi kufanya majaribio kwa nchi nzima. Watanzania ni waelewa sana!
====
Kwamba Tanesco itabinafsishwa, TTCL, ATCL, TRC, nakadhalika....! Vyote watapewa " wakwepuaji" wa chama cha Mbowe,Chadema! Maajabu hayeshi!
Hizi ndo unaita akili kweli? Shirika la Umeme siyo business oriented, ni service oriented. Kwa nini hukumpigia hata simu Mh. Mwalimu akakufafanulia alichosema kuliko kujidhalilisha hivi?
 
Ipo hoi wakati mimi najiunga JF kupitia TTCL?
Mitandao yote inachukua bando TTCL.
Kweli TTCL ni ma-genius.

TTCL wanatoa gawio la 2.1bil huku hapohapo wanaomba mtaji wa trilion 1.7,hizi ni hesabu za Trigonometric ratios
nadhani.
Screenshot_2020-10-03-08-25-57-1.jpg
Screenshot_2020-10-03-08-26-42-1.jpg
 
Kodi waliahidi hawatakusanya, na sasa wanaahidi kubinafsisha biashara za serikali, matapeli hawa
Wote wanao ona wamepata Mkombozi ni kama vipofu vile. Wengi hawaoni mbali, na huendeshwa kwa matumbo yao tu. Kwa mustakabali wa ustawi wa mama Tanzania, Sera za chama cha Mbowe ni sumu kwa taifa wala sio mbolea.
Sera ya Chadema ni wazi haikuandaliwa Tanzania wala na watanzania iliandaliwa nje ya nchi na wazungu akina Amsterdam imejaa maslahi yao tu sera yote ona hadi madii wataweka rehani kwa wazungu!!! Hiyo sera haikuandaliwa Tanzania
 
Back
Top Bottom