Salma Kikwete ni first lady, ana haki ya kikatiba ya kupewa ulinzi kwa nafasi yake. Hata waliotangulia walikuwa wakipewa ulinzi. Ila hilo la kupewa taarifa za maendeleo ya mkoa/wilaya si sahihi, kwani yeye hana MAMLAKA ya kutoa maamuzi. Taarifa za maendeleo hazitolewi kama hadithi, lakini kwa kumsomea huyo mama ni sawa na kusoma hadithi. Anachokifanya sasa hivi ni kampeni ya kumsaidia mumewe.
haki ya nani ipo siku mtasikia au kuona laivu anakagua gwaride. na hao wakuu wa mikoa in maana hawajui itifaki? risala anasomewa ili atoe taarifa gani kwa nani? nijuacho mimi hatima ya risala ni kufikisha ujumbe kunakotakiwa na penye uwezekano majibu au ahadi zitolewe. sasa mwalimu wangu salma, ana majibu gani juu ya mambo mazito ya nchi? kaaaazi kweli kweli, hata mimi sijui anpokwenda mikoani ankwenda kwa nafasi ipi. may be ankuwa amemwakilisha mkuu wa nchi. vinginevyo nadhani si sahihi kufanyiwa afanyiwavyo. kama ingekuwa kukagua maendeleo ya ka epa kake ka wama binafsi sioni tatizo.
vipi wewe bana!!! Michele Obama huwa hapati hivyo ulivyouliza?
First lady yoyote duniani ana haki zake na nafasi yake katika nchi ikiwamo hizo hadhi na nafasi... hiyo hadhi ina-extend hadi watoto wa marais
Kuna haja ya kujua protocols za viongozi ili jamii ielewe zaidi
Hapa ndugu inabidi upewe elimu ya uraia yaani 'civics' Kwani hufahamu wewe kuwa ulipompigia kura Kikwete kuwa Rais ndipo ulipompigia kura Mama Salma Kikwete kuwa 'First Lady'. Au unafikiri ni suala la utashi wa mtu binafsi kuamua majukumu na haki za mke wa Rais?
Kama wataalam wa 'political science' humu jamvini na wataalam wa sheria wana wakati watakusaidia kielimu. Lakini inategemea na makusudi uliyo nayo katika kuuliza swali, kama lengo ni kujifunza ninaamini utafundishwa tu.
Nadhani huyu mama kwao ni Singida kama sikosei!
FLs wahahaki kikatiba kwa sababu tu waume zao ndio viongozi wakuu wa nchi..Maamuzi mengine ya nchi yanaweza yakafanywa na mke wa kiongozi indirectly. Hii unaweza kuona hata katika enzi za simulizi za BIBLIA jinsi ma Malkia walivyo kuwa wakiwaendesha waume zao kufanya maamuzi yaliyo nje ya utashi wao. Kusomewa risala ya maendeleo ya nchi mmmmhh!!!!...Labda alitumwa na mzee!!!
Wakuu Heshima Mbele,
Kiukweli Mke wa Rais anazohaki zake, Mfano haki ya kuwa na usafiri, haki ya kuwa na ulinzi , Kama ambavyo watoto wa Rais wana haki ya kupewa ulinzi pale inapobidi. Kule Marekani shule wanazosoma watoto wa Marais ni eneo maalum la ulinzi, na wale watoto wamepewa secret code za Ulinzi na C.I.A. ,Mfano Obama ni Renegade, Michele ni "Renaissance",Malia Obama's ni "Radiance," na Sasha Obama's ni "Rosebud." ili tu kuimarisha mawasiliano ya kiulinzi kwa emeregence.
Tatizo lililopo ni kwenye mipaka ya kazi, Mke wa Rais anaweza kushiriki kwenye shughuli za kijamii, lakini hii haiko kikatiba kwamba mke wa rais atafanya nini KATIKA KIPINDI CHA URAIS WA MUMEWE, mfano wakati Mkapa anaingia Ikulu Anna alikuwa afisa pale UNICEF, Aliacha shughuli zake na kuanzisha NGO yake ya EOTF.Huyu mama yetu sasa na yeye ana WAMA. Sijui huyo atakayekuja atakuja na kitu gani? Lakini iwepo mipaka Kisheria inayompa mke wa Rais kazi za Kufanya. kama ni Taasisi ijulikane na kila mke wa Rais anayeondoka madarakani aiache ili yule anayeingia aitumie ,Lakini pia ifahamike source ya Funds.
Huyu ni co-president. That is why.Mie nataka kujua pia hapa jana nimeona Mkuu wa Mkoa wa Mara akisoma Risala mbele ya mama Salma nikajiuliza maswali mengi kichwani bila majibu
Kwani anakazi gani katika nchi mpaka asomewe hiyo Risala ?
...Tz jamhuri ya MABWEGE!!!! wachache sana wana akili timamu, waandishi wote wa habari ni mabwege!!