Salma Kikwete na kampeni za urais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Salma Kikwete na kampeni za urais

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Jan 9, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280  [​IMG]

  JE, Salma Kikwete ameanza kampeni kwa ajili ya mumewe hata kabla ya kipenga kupulizwa? Uchaguzi mkuu ni Oktoba 2010 na vita vya maneno vimeanza.

  Kama si hivyo, kwa nini sasa anaonekana zaidi katika vyombo vya habari na kutembelea mikoani, tofauti na ilivyokuwa mumewe alipoingia ikulu?

  Watetezi wa anachofanya wanasema anafanya kazi ya shirika lake lisilo la kiserikali la Wanawake Maendeleo (WAMA). Hili nalo linahitaji mjadala kwani linaweza kumuingiza rais, na hata yeye binafsi, katika mgogoro.

  Haiwezekani mumewe akawa mkuu wa serikali naye akawa na shirika lisilo la kiserikali, halafu kukawa salama. Ni lazima kutakuwa na mgongano wa kimaslahi na hata kisheria.

  Uzoefu tulioupata kutoka kwa Anne Mkapa, mke wa rais mstaafu, Benjamin Mkapa unatosha kumsaidia Kikwete kuondokana na aina hii ya mashirika binafsi.

  Salma hawezi kutoa majibu kwa nini aanzishe NGO baada ya mumewe kuwa rais. Hawezi kujibu kwa nini hatuoni wake za viongozi wengine wa vyama vya siasa wakimiliki NGO. Hawezi.

  Kwani hata hawa wakiwa nazo hakuna wa kuzichangia. NGO zinazochangiwa ni za wake wa marais; huko ndiko wachangiaji wanatafuta kuwa karibu na ikulu ili waweze kufanikisha malengo yao.

  Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa NGO ya mama Mkapa EOTF. Wengi waliokuwa wakiichangia walikuwa na malengo binafsi.

  Imeandikwa na kuhubiriwa: Mke wa Kaizari hapaswi kutenda tendo lenye kuweza kutilia shaka utawala wa mumewe. Tuliishi na kumuona Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Tuliona jinsi mkewe, Maria Nyerere alivyokaa mbali na utawala wa mumewe.

  Mama Maria hakuwahi kujihusisha na “uchuuzi” wakati mumewe akiwa ikulu.

  Lakini taasisi ya mke wa rais – WAMA imefanya jambo moja la maana. Imeondoa maneno yasemayo WAMA Foundation, The Office of The First Lady of the United Republic of Tanzania kwenye tovuti yao.

  Hata neno Jamhuri ya Muungano, kisheria halipaswi kutumiwa na mtu au taasisi yoyote isipokuwa mihimili mitatu ya dola – Bunge, Mahakama na Utawala. Cheo cha mke wa rais (First lady) hakimo katika katiba yetu.

  Kama mzalendo, nimejaribu kukusanya baadhi ya maoni kuhusiana jinsi ufisadi unavyoingia ikulu kiasi cha kututatiza.

  Ukiangalia kinachofanywa na WAMA hakina tofauti na kile kinachofanywa na EOTF. Ni vema mama Salma akajifunza kutoka kwa wengine. Ajifunze kwa kilichompata Regina Chiluba, mke wa zamani wa rais wa Zambia, Fredrick Chiluba.

  Bahati mbaya sana, hata wavuti wa Kurungenzi ya Habari Ikulu inaonekana kutangaza biashara ya WAMA badala ya wizara za serikali. Ajabu hakuna anayestuka wala kupiga kelele.

  Kama umma ukishupaa NGO hii inaweza kufutwa hata na mahakama kutokana na mgongano wa maslahi. Na kutokana na kutokuwapo kwa sheria kuchuja na kutangaza wafadhili wake, WAMA inaweza kujikuta katika mgogoro wa kuchangiwa fedha chafu.

  Hata neno Jamhuri ya Muungano, kisheria, halipaswi kutumiwa na mtu au taasisi yoyote isipokuwa mihimili mitatu ya dola – Bunge, Mahakama na Utawala. Cheo cha mke wa rais (First lady) hakimo katika katiba yetu.

  Bali kwa mtindo huu, Tanzania inaweza kuwa nchi pekee ambapo rais na mkewe wote ni marais. Kikwete ni rais wa Jamhuri huku mkewe akiwa rais wa WAMA.

  Ukitaka kujua hili angalia mapokezi ambayo Mama Salma anapewa na taarifa zake zinavyochapishwa na kutangazwa na vyombo vya habari. Ukitafuta uhalali wake kikatiba, hakika haupo.

  Hata kama anajulikana kwa ubabe na upayukaji wake, bado mke wa rais wa Kenya, Lucy Kibaki hana mamlaka kama aliyo nayo Salma ambaye anaweza kuingia mkoa wowote kwa kisingizio cha NGO yake na kufanya shughuli za kisiasa kama kulakiwa na viongozi wa mikoa na kukagua miradi ya maendeleo ukiachia mbali kutoa kauli mbiu zinazoonyesha wazi kumpigia debe mumewe.

  Kile ambacho Salma anamzidi Lucy, ni ile hali ya kufanya kitu waitacho Waingereza, “one woman show.” Kwani kila lilipo jina WAMA yupo. Maana yake ni kwamba, yeye anapenda madaraka na anataka kufanya kila kitu peke yake.

  Kwa nini hatuoni makamu wake au hata wasaidizi wengine wakifanya shughuli za WAMA kama kweli ni ya umma kama anavyodai? Kuthitibitisha hili, tembelea tovuti ya WAMA uone ukweli huu. Hii haiwezi ikawa taasisi ya wanawake na watoto wa Tanzania.

  Kuonyesha kuna namna ya kampeni na kutumia mamlaka ya mume wake, hivi karibuni, Mama Kikwete amewahi kutoa namba yake ya simu ya mkononi ambayo ni 0754-294450.

  Aliitoa kwa wanawake mkoani Singida ili waweze kumpigia au kumtumia ujumbe mfupi wa maneno pindi waume zao watakapowanyanyasa kutokana na kitendo cha wao kwenda kupima kwa ajili ya kujua afya zao.

  Japo kwa juu hili linaweza kuonekana ni jambo bora, kwa mtu anayejua mipaka ya mamlaka yake na utaratibu wa utawala kisheria, angeshauri wahusika waelekeze madai yao kunakohusika: polisi, vituo vya kutetea haki za binadamu na hata wizarani.

  Licha ya kuwa ubabe, hii ni kampeni ya wazi kuonyesha wahusika wanawajali wananchi jambo ambalo si kweli. Kwanini hasira zake zisielekezwe kwenye kumshauri mumewe kupambana na ufisadi kama ana uchungu na nchi hii?

  Ina maana hajui kuwa ujinga na umaskini ndivyo vyanzo vya yote haya? Sijui kama, hata kwenye kupokea misaada, anauliza usafi wa mtoaji.

  Kwa kadri nijuavyo upenzi wa sifa wa watawala wetu na watu wao, kama utafanyika uchunguzi huru juu ya matumizi ya WAMA, usishangae pesa inayotumiwa kwenye ziara ikawa kubwa kuliko hiyo inayowafikia walengwa. Bahati mbaya sijawahi kusoma popote taarifa ya hesabu za mwaka za WAMA au EOTF.

  Wengi wanaweza kuona kama tunamuandama mke wa rais au kutotambua umuhimu wa kupigania haki za akina mama. Lakini swali ni, kwa nini mke wa rais, wakati tuna wizara yenye watendaji wanaolipwa pesa ya kodi yetu?

  Kwa nini misaada anayopokea isipelekwe moja kwa moja wizarani au kwenye mashirika huru kama kweli ana uchungu na walengwa na si kujipatia umaarufu? Kubwa zaidi ni kutumia ikulu kwa manufaa binafsi, yawe yake au mumewe na marafiki zake.

  Je, akina mama wa Tanzania wataingia mkenge wake huku waume na kaka zao wakizidi kuteswa na sera za Kikwete za kuvumilia mafisadi?

  Je, atawalainisha wasahau kuwa Kikwete hajatimiza ahadi zake? Je, watahoji uhalali wa NGO yake na kumwambia ukweli kuwa ni ya mashaka na utata?
  Chanzo: MwanaHALISI Desemba 23, 2009.
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,607
  Trophy Points: 280
  WAMA tunaomba majibu ya hoja hizo.......maana tumesikia upande mmoja!!
   
 3. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2010
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Mnyonge Mnyongeni haki yake mpeni huyu mama amekuwa akifanya kazi kubwa ya WAMA na nakumbuka kuna kipindi tulikuwa na opinion kuwa anafanya kazi kubwa kuliko Mumewe tena on the grass roots level mikoa na vijiji vingi sana Tanzania na binafsi najua vikundi vingi ambavyo vimepata misaada ya ki taalam,hali na mali toka WAMA kuliko ile NGO ya Mama ANNA MKAPA


  Tatizo la na SNOBS humu ni kuwa Mama Salma na mumewe hawakuenda kwenye Ivy League universities na wala hawakutoka kwenye privileged background kama watawala wetu wengine na hata social circles zao si kama za baadhi yawatawala na wanasiasa wetu waliopita na walipo madarakani ndio maana utasikia ohhh Mbona mama Salma haongei English mara ohhh kwa nini havai nguo za Kizungu as if hao walengwa wa WAMA ndio priorities zao!

  Hebu mpumzisheni mama wa watu
   
 4. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2010
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kaka mtoa hoja kaiwasilisha ili ijibiwe....naona umejump kwenye issue ya uonevu...binafsi sitaongea chochote mpaka kwanza wahusike waelezee kwa ufafanuzi tuhuma hizi then from there nitatoa comments zangu...by now nipo neutral kwasababu ndo kwaanza naanza kuzisikia hizi tuhuma humu ndani.
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Jan 9, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,521
  Likes Received: 5,752
  Trophy Points: 280
  huyu mama atulie tu
  siku zote akuwa anazunguka mikoani leo kaona muda umefika

  2...ameshaambiwa na shehe yahya bin huseein kwamba mumewe anashinda asifanye kampeni,,,aoni anapingana na mtabiri aliewaambia wala wasizunguke mitaani au ndio pesa za kampeni lazima ziliwe hata kama ushindi upo??
   
 6. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #6
  Jan 9, 2010
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,402
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Don't reveal too much of yourself, because they'll use what they learned and use it against you. Of all the First Ladies of the URT?? Go to your ARCHIVES!! Hey GT!!

   
 7. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #7
  Jan 9, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  mbona tayari amepumzika, swala la msingi kwanini inataka kuwa mtindo wa kila anaeingia Ikulu kama mke wa Rais kuanzisha NGO na kisha kuondoka nayo pindi anapoondoka Ikulu, hapa kama kuna umuhimu wa hizi NGOs kwanini wasiziache ziendeshwe na mama wengine wake za marais wakiingia ikulu Magogoni.
  Jambo la pili mrs KIKWETE mara kadhaa amekua akitoa maagizo kama ni mtu mwenye mamlaka kikatiba, akiwaagiza wakuu wa wilaya kufanya hiki na kile, na katika mizunguko yake yote akitumia pesa za umma amekua akivaa uwakilishi wa CCM za si mama wa kila mmoja kama ambavyo ilitegemewa na watu wengi na kwakuzingatia kua katiba yetu haina nafasi inayoelezewa kuhusu FIRST LADY.
   
 8. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #8
  Jan 9, 2010
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  nafikiri title ya thread hii ingependeza iwe Salma Kikwete na WAMA na si Salma Kikwete na kampeni za Urais maana kampeni hizo hazijatajwa popote pale inatuchanganya wengine.
  pia humu ndani naona nyingi ni brabra.
  kama WAMA inafanya kazi nzuri kama GT alivyodokeza ni vizuri ila kama kuna ufisadi basi uanikwe hapa. hatuwezi kusema tu WAMA si nzuri ili tuendelee lazima watu wafikirie namna mbalimbali (ubunifu) wa kuleta maendeleo katika nchi hii kwa njia halali
   
 9. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #9
  Jan 9, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280

  Heshima kwako Game Theory,

  Sina tatizo na mama Salma Kikwete kutembelea mikoani na kufanya kampeni kwaajili ya mumewe.Nimekuwa nikijiuliza mara kadha ni kwanini wake wa marais kuanzia enzi za Mkapa wamekuwa wakitumia kodi za wananchi kuanzisha NGO zao kwa manufaa binafsi.Mama Anna Mkapa alikuwa na NGO yake enzi mumewe alipokuwa pale magogoni lakini baada ya Mkapa kuondoka madarakani hatuisikii tena.

  NGO ya mama Salma Kikwete itakufa mara moja siku Muungwana atakapoondoka Ikulu.Wake za marais yafaa waache kujiingiza katika utendaji wa shughuli za kiserekali.Wakati mwingine nashangaa sana utamsikia mama Salma akitoa maagizo utadhani ni waziri.
   
 10. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #10
  Jan 9, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Mke wa Rais Mama Salma alianzisha hii NGO ya WAMA baada ya kuona jinsi aliyemtangulia alivyofaidika KWAKUITUMIA ofisi ya mumewe kuanzisha NGO iliyomuwezesha kukusanya fedha nyingi kutoka kwa watu mbalimbali.Hicho ndicho kilichomvuta huyu mama kuanzisha taasisi hii wala haikuwa mapenzi yake kwa wanawake na watoto hicho ni kisingizio; ama sivyo angeanzisha alipokuwa mwalimu anafundisha!! Pili nadhani alianzisha hii taasisi kama security ya maisha kwani Jakaya akiondoka Magogono na yeye ataondoka na WAMA yake kama alivyofanya aliyemtangulia; hapo baadae Muungwana akiamua kuongeza mwenza mwingine a' la Jacob Zuma, Mama Salma will keep herself busy tendering the gotten wealth through her NGO!! Hawa wake wa viongozi na NGO zao ndio vichochoro wanamopitia mafisadi ili kuwafikia viongozi; na hili halina mjadala kwani "THERE IS NO HUSBAND WHO IS A HERO TO HIS WIFE"
   
 11. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #11
  Jan 9, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hivi hizi safari za hapa na pale kwa niaba ya WAMA zinalipiwa na WAMA au zinalipiwa na Ikulu?
   
 12. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #12
  Jan 9, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Bulesi hapo umenena, heshima kwako.
   
 13. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #13
  Jan 9, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Mke wa Rais akisafiri hata kwenda kuangalia sindimba kwao LINDI gharama zinalipwa na kodi za Watanzania masikini, maana ana dereva wake, Mlinzi/Mpambe wake, ana gari ya escote yenye walinzi wanne. na bado kila mkoa anaoingia watawala hapo lazima wajulishwe ili kuhakikisha maswala ya ULINZI na usalama yanakua katika hali nzuri.
   
 14. b

  bnhai JF-Expert Member

  #14
  Jan 9, 2010
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Ohpss
  Bonafsi sioni tatizo kwa wake wa viongozi kumiliki (kuongoza/kuanzisha) mashirika yasiyokuwa ya kiserikali. Maana ni njia mojawapo ya kusaidia wananchi. Pia mheshimiwa anasema ameanza kuonekana hivi karibuni akitembea mikoani. Huu ni uongo Salma ameanza kutembea mara baada ya mumewe kuchaguliwa kuwa rasmi. Ni kimuhemuhe cha uchaguzi au nini. Hebu tuweni wakweli.
  Anna Mkapa hakuna shida katika NGO'S bali tatizo ni kufanya biashara na hapo ndiyo mgongano wa kimaslahi maana utanunua kwake. Km NGO ni tatizo tujulishwe kivipi. Kumbuka km NGO zikisimamiwa ipasavyo basi zinawasaidia saana wananchi maana baadhi ya wafadhali hawaamini serikali za Kiafrika wanataka kuona impact siyo impavt after years na huwa wanatarget maeneo maalum.
  Ukiangalia kinachofanywa na WAMA hakina tofauti na kile kinachofanywa na EOTF. Ni vema mama Salma akajifunza kutoka kwa wengine. Ajifunze kwa kilichompata Regina Chiluba, mke wa zamani wa rais wa Zambia, Fredrick Chiluba.
  Mkuu mie ninashaka na unachotaka kukisema maana mgongano wa kimaslahi wakati NGO's kazi zake sio biashara, sijui ni maslahi yapi. Nimeona point moja ya maana juu ya usafi wa hao wanaotoa msaada. Hebu tutajie ni akina nani tuwaangalia hapo ndiyo conflict of interest inaweza ikaanza.
  Lazima tukubali kwamba kuna resources tukitumia baadhia ya prominent figure ndio zitapatikana. Hebu wewe andaa fundrising hapo tuone utapata kiasi gani. Tunahitaji saana resources zenye maadili na sio maneno yasiyo na evidence.
   
 15. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #15
  Jan 9, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  KWA HARAKA hakuna tatizo kwa hawa kina mama wake za marais kufanya hayo wyafanyayo kwa gharama ya pesa za walipa kodi......maana wanapokua kwenye harakati za hayo mambo ya NGOs wanatumia pesa zetu nje ya taratibu maana katiba haisemi nafasi yao, tambua hizo perdiems tunazowalipa wapambe/walinzi, wapambaji wake nakadhalika ni jumla ngapi kwa mwaka..by the way we dont see positive output toka kwa miradi hiyo zaidi ya kufuja pesa zetu.
   
 16. b

  bnhai JF-Expert Member

  #16
  Jan 9, 2010
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  How do you measure outputs? (Subjective). Pia kumbuka NGO's inaendeshwa kwa donatations subscrptions etc. Unless uwe na evidence kwamba wakati wa kikao cha bunge kuna bajeti inakwenda kwa mama Anna na Salma ili waendeshe hizo NGO's. Ninachofaham waume zao kuwapo madarakani kunawarahisishia wao kukusanya funds. Hebu angalia ishu ya mimba mashuleni ilivyopigiwa kelele, angalau inaeleweka. Madarasa yamejengwa. Halafu kumbuka yeye kama mke wa Rais anastahili zake kutokana na maisha anayotakiwa kuishi.
   
 17. b

  bnhai JF-Expert Member

  #17
  Jan 9, 2010
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Unaushahidi na hili au ndiyo tunajaribu kujifikirisha tu? Nani kasema wanatumia kodi za wananchi kuanzisha NGO's. Binafsi nawaona wanakuwa wabunifu kuwasaidia wananchi badala ya kubweteka. Inamaana ukiwa mke wa Rais mchango wako hauhitajiki.
   
 18. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #18
  Jan 9, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  bahati mbaya sana umesahau kuwa NGO hizo zinaendeshwa kwa sehemu kubwa na kodi zetu, msafara wa mke wa rais wote unalipwa perdiems maana wanaomzunguka kuanzia msusi, mtandika kitanda, muaandaa msosi wote ni watumishi wa umma, akiwa nao huko mikoani wanatafuna pesa za umma. sasa ni heri uwepo wa hawa wake za maraisi uwe wazi kikatiba maana wanaconsume sana kuliko hizo kelele za mimba za wanafunzi kazi ambayo ingeweza kufanywa na wakuu wa wilaya.
   
 19. b

  bnhai JF-Expert Member

  #19
  Jan 9, 2010
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Mie naona hizi arguments ni baseless. Nadhani kuwa kwenye nafasi ya mke wa Rais kuna mfanya akipiga kelele inasikika zaidi. NGO's hiyo imefanya kazi vyema hasa mikoani huko. Maana kuna watu ninahakika kuna siku wataandika kwamba NGO's hiyo na ya mama Anna Mkapa zimewasaidia. Unakumbuka mabinti wangapi wamesaidiwa kwenda shule. Kuwa mke wa Rais kumemfanya atoke kulitumikia Taifa kwa level ndogo ya ualimu na kwenda level kubwa. Kumbuka amekuwa akimobilise resources kwa ajili ya NGO's. Mie nadhani waendelee na kazi zao maana wafadhili wanatoa pesa kule wanakoamini kuna usimamizi. Hoja ya kwamba anasafiri na mtandika kitanda, haina tofauti na kusema anasafiri na kitanda. Ah jamani nyingine ni zaidi ya porojo
   
 20. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #20
  Jan 10, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Subirini ngwe inayokuja wataanza kuwalipa mishahara kama Kenya. Sheria lazima iwe wazi kuhusu matumizi ya pesa za walipa kodi inapokuja kwenye matumizi ya mke wa rais. Haya ni katika yale mapungufu yaliyopo kwa sababu ya kuwa na rais wa kwanza ambaye alitenganisha na hatukuweza kuona shopping za nguvu za marekani na Ulaya kama hivi sasa.

  Kama wakiweza kuweka wazi hapa matumizi hayo yale ya Gavana wa Benki na nyumba yatakuwa hayafui dafu. Huu ni uzembe wa bunge letu tukufu ambalo kwao ni kuangalia mapato na maslahi yao binafsi na si ya walipa kodi.
   
Loading...