Salma Kikwete anapomfanyia kampeni Rais ajaye

Salma Kikwete anapomfanyia kampeni Rais ajaye

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2009
Posts
3,444
Reaction score
265
Bernard Membe ametangaza kutokugombea Ubunge 2015. Niseme atagombea urais. Bernard Membe akishinda Urais 2015, basi shukrani zitamuendea Mama Salma Kikwete. Kwani hii shuguli imeonekana wazi pale Dodoma katika mkutano mkuu wa CCM ambako mama Salma Kikwete, Nyalandu na Ridhiwani walifanya kampeni za waziwazi hadi hasa za kugawa hela na vitisho ili Membe na Rais Kikwete wachaguliwe kwenye kamati kuu. Hali iliyoleta mvutano mkubwa kati ya kada maarufu wa CCM Bashe na Waziri Membe. Ni katika nchi chache tu rais na familia yake wanajiingiza kwenye utawala wa nchi, ila kwetu hii familia ya Kikwete imeweza.

Mama Salma ndiye mpiga debe mkuu wa Bernard Membe akisaidiwa na Dr. Kikwete na Mwanaye Ridhiwani. Lakini ni kwa nini Mama kama huyu na heshima zake ajiingize kwenye siasa? Kwa sasa mama kikwete ndiye mwakilshi wa Lindi NEC (CCM) Kadhalika mtoto wa Rais, Ridhiwani Kikwete ambaye ndiye mwakilishi kutoka Bagamoyo ambaye pia alipita bila kupingwa. Ndugu zake Kikwete nao wamechukua nafasi nyingi sana ndani ya CHAMA na serikali. Je tujiulize ni kwa nini?

Rais amemaliza muda wake, anachokiogopa ni nini hadi kuwaweka watu wake kwenye nafasi nyeti mpaka kwenye urais? Rais mstaafu anapewa stahiki zake. Anapewa ulinzi maisha yake yote, anapewa, wasaidizi, Gari pamoja na Nyumba. Kwa nini hii familia iwe na hofu kiasi cha kuhakikisha madaraka wanabaki kwenye nafasi nzuri za madaraka?

Je Familia ya Kikwete imewafanyia nini kibaya watanzania kiasi cha kuogopa? Wana nini cha kuficha? Je wamo kwenye ufisadi? Rais anajaribu kulinda maslahi gani? Ni maslahi ya kifedha au ni madhambi gani? Najaribu kutafakari kwa maana huyu mama kujikita kwenye siasa pindi mume wake akielekea kustaafu kunatia shaka. Mama mwinyi hakujiingiza kwenye siasa. Wake za rais waliopita hasa mwinyi na mkapa walijiingiza kwenye ufisadi lakini siyo siasa. Mama Nyerere hakujiingiza kwenye siasa. Mama mkapa hakujiingiza kwenye siasa. Kwa nini Mama Salma Kikwete? Hasa anapojaribu kutupachikia Waziri Membe kuwa Rais.

Mods: Tafadhalini. Huyu mama siyo mwanafamilia tena, bali mwanasiasa. Inabidi ajadiliwe kwani amekuwa mke wa kwanza wa Rais kujiingiza kwenye siasa ya nchi yetu. Tunaomba msiondoe au kuunganisha hii thredi
 
Ingawa huna utafiti, Salma hana kosa ikizingatiwa kuwa kwa sasa kuna usultani wa Kikwete ambaye anaweza kumrithisha yeyote amtakaye. Laiti Salma angetumia huu muda lau kujiongeza elimu kuliko kuendelea kuonekana kihiyo kama alivyo. Anyways, kwa vile urais wa Bongo sasa ni kijiko cha dhahabu, kila mwizi atapenda aupate kwa gharama yoyote.
Nilisahau. Urais ni swala la Familia..... JK
 
Mwanaasha si alifeli si ataingia ktk siasa pia...!!!!?

~~ Huyu mama has a very low ACADEMIC QUALIFICATIONS.... angejiendeleza kuliko kutia aibu...
 
Bernard Membe ametangaza kutokugombea Ubunge 2015. Niseme atagombea urais.......

Mama Salma ndiye mpiga debe mkuu wa Bernard Membe akisaidiwa na Dr. Kikwete na Mwanaye Ridhiwani. Lakini ni kwa nini Mama kama huyu na heshima zake ajiingize kwenye siasa?
Rais amemaliza muda wake, anachokiogopa ni nini hadi kuwaweka watu wake kwenye nafasi nyeti mpaka kwenye urais? Rais mstaafu anapewa stahiki zake. Anapewa ulinzi maisha yake yote, anapewa, wasaidizi, Gari pamoja na Nyumba. Kwa nini hii familia iwe na hofu kiasi cha kuhakikisha madaraka wanabaki kwenye nafasi nzuri za madaraka?........

...........Je Familia ya Kikwete imewafanyia nini kibaya watanzania kiasi cha kuogopa? Wana nini cha kuficha? Je wamo kwenye ufisadi? Rais anajaribu kulinda maslahi gani? Ni maslahi ya kifedha au ni madhambi gani? Najaribu kutafakari kwa maana huyu mama kujikita kwenye siasa pindi mume wake akielekea kustaafu kunatia shaka. Mama mwinyi hakujiingiza kwenye siasa. Wake za rais waliopita hasa mwinyi na mkapa walijiingiza kwenye ufisadi lakini siyo siasa. Mama Nyerere hakujiingiza kwenye siasa. Mama mkapa hakujiingiza kwenye siasa. Kwa nini Mama Salma Kikwete? Hasa anapojaribu kutupachikia Waziri Membe kuwa Rais......
Hapo kwenye RED, naomba ufafanuzi wako kuhusu "heshima" ya Bi. Salma unayoizungumzia, ili nichangie kwa uhuru zaidi.
 
Mtajuta kumchagua jk kuwa rais wa tz.kwa akili zake anadhani atatawala hata kwa kutuchagulia mtu ili tu alinde ubongo fleva wake
 
Bernard Membe ametangaza kutokugombea Ubunge 2015. Niseme atagombea urais. Bernard Membe akishinda Urais 2015, basi shukrani zitamuendea Mama Salma Kikwete. Kwani hii shuguli imeonekana wazi pale Dodoma katika mkutano mkuu wa CCM ambako mama Salma Kikwete, Nyalandu na Ridhiwani walifanya kampeni za waziwazi hadi hasa za kugawa hela na vitisho ili Membe na Rais Kikwete wachaguliwe kwenye kamati kuu. Hali iliyoleta mvutano mkubwa kati ya kada maarufu wa CCM Bashe na Waziri Membe. Ni katika nchi chache tu rais na familia yake wanajiingiza kwenye utawala wa nchi, ila kwetu hii familia ya Kikwete imeweza.

Mama Salma ndiye mpiga debe mkuu wa Bernard Membe akisaidiwa na Dr. Kikwete na Mwanaye Ridhiwani. Lakini ni kwa nini Mama kama huyu na heshima zake ajiingize kwenye siasa? Kwa sasa mama kikwete ndiye mwakilshi wa Lindi NEC (CCM) Kadhalika mtoto wa Rais, Ridhiwani Kikwete ambaye ndiye mwakilishi kutoka Bagamoyo ambaye pia alipita bila kupingwa. Ndugu zake Kikwete nao wamechukua nafasi nyingi sana ndani ya CHAMA na serikali. Je tujiulize ni kwa nini?

Rais amemaliza muda wake, anachokiogopa ni nini hadi kuwaweka watu wake kwenye nafasi nyeti mpaka kwenye urais? Rais mstaafu anapewa stahiki zake. Anapewa ulinzi maisha yake yote, anapewa, wasaidizi, Gari pamoja na Nyumba. Kwa nini hii familia iwe na hofu kiasi cha kuhakikisha madaraka wanabaki kwenye nafasi nzuri za madaraka?

Je Familia ya Kikwete imewafanyia nini kibaya watanzania kiasi cha kuogopa? Wana nini cha kuficha? Je wamo kwenye ufisadi? Rais anajaribu kulinda maslahi gani? Ni maslahi ya kifedha au ni madhambi gani? Najaribu kutafakari kwa maana huyu mama kujikita kwenye siasa pindi mume wake akielekea kustaafu kunatia shaka. Mama mwinyi hakujiingiza kwenye siasa. Wake za rais waliopita hasa mwinyi na mkapa walijiingiza kwenye ufisadi lakini siyo siasa. Mama Nyerere hakujiingiza kwenye siasa. Mama mkapa hakujiingiza kwenye siasa. Kwa nini Mama Salma Kikwete? Hasa anapojaribu kutupachikia Waziri Membe kuwa Rais.

Mods: Tafadhalini. Huyu mama siyo mwanafamilia tena, bali mwanasiasa. Inabidi ajadiliwe kwani amekuwa mke wa kwanza wa Rais kujiingiza kwenye siasa ya nchi yetu. Tunaomba msiondoe au kuunganisha hii thredi

Membe ameshaharibu nyumbani kwake kutowaunga mkono suala la gas
 
Ndugu Tunguli, kwa kuwa Rais wetu wa sasa ndie ataongoza katika kuzungumzwa mambo hasi (negative) kuliko marais wote waliopita basi amejitahidi kuwaweka ndugu zake ili wapunguze kasi yake ya kuzungumzwa mambo hasi kwenye vyombo vya maamuzi, pia ulivyosema ni sahihi zaidi kwamba first lady ameanza kampeni, rais kuweka familia yake kwenye vyombo vya maamuzi ni kuhakikisha anaweka rais anaemtaka.

Sasa Tunguli thread yako imeanzisha rasmi kitu kipya, makundi yanayogombea urais katika chama cha mapinduzi ni mawili
1.Kundi la Lowasa na wapambe wake
2.Kundi la Membe na wapambe wake
 
benard membe anaitwa nani jina lake la asili ukiacha hili la shule? kuhusu urais sema vile imezoeleka kuwa chama kilichopo madarakani kinapita by crooks and hooks, kwa hiyo imani ipo kwa yule atakayepitishwa na chama. vinginevyo mambo yakibadilika hatapita, hata chama chake kikimpitisha, mazingira yakiwafavour raia wanaochagua rais basi atapita rais anayetakiwa na wananchi
 
Hujaeleweka unaposema kuwa mama salma kikwete unapomshangaa kujiingiza kwenye shughuli za kisiasa

Ila hujashangaa yule mke wa babu yenu kujiingiza kwenye siasa za maandamano mpaka kupigwa mkong'oto wa akili na wale polisi kule arusha...
Anyway hivi umesahau kuwa kitendo chanyeye kumruhusu jk agombee urais tayari kashajiingiza kwenye siasa so alijiingiza kwenye siasa since 2005

2005 alikuwa anapiga kampeni jk na shein umesahau

Unaposema kuwa ndio mke wa raisi wa kwanza sio kweli mama anna mkapa naye since 1995 alikuwapo kwenye kampeni
 
Umempa jibu sahihi analolote kinachomsumbua ni chuki
 
Mkuu CTU, ni vyema ukasoma na kuelewa kabla huja anza kujivua nguo zako kwa kuonyesha uwezo wako mdogo wa kufikiria mambo.

  1. Nashukuru kwa kunifumbua macho mkuu CTU, kumbe Salma ndiye aliye mruhusu Kikwete kugombea urais mwaka 2005, mie nilidhani ni chama chake cha CCM. Hili nalo neno...........
  2. Hakuna aliyehoji Salma Kikwete kumpigia mumewe kampeni, bali ni Salma na watoto wao kushika nafasi kubwa za maamuzi kwenye chama. Jiulize, je hiki kilitokea kwa marais wengine walio tangulia?
  3. Ni dhahiri Dr.Slaa anawanyima usingizi, na msipoangalia kuna hatari ya kupata pressure, Stroke au vyote kwa pamoja ifikapo 2015. Tuambie Josephine Mshumbusi ana nafasi gani katika chama cha CHADEMA?
  4. Mkuu CTU ni vyema ukajibu maswali kwa kutoa hoja na siyo porojo na kutokwa na mapovu. Kwa mfano great thinker ameuliza kwa nini JK ameamua kupanga familia yake, ndugu na jamaa zake kwenye safu ya maamuzi ya chama? Ni dhahiri kuna kitu kinafichwa nyuma ya pazia. Je wajua Membe na Jakaya ni ndugu? na ndo huyo anayepigiwa upatu na Salma Kikwete ili awe mrithi wa Jakaya? on other hand wanataka kugeuza urais uwe wa familia? Tafakari.......chukua hatua !!!!!

Wanajanvi naomba kuwasilisha.
 
''Safari hii ni zamu ya mikoa ya pwani kutoa rais''.. cjuhi ilisemwa ama ndo naisema mimi leo.Tafakari,Chukua hatua.
 
Rais ajaye ni Migiro samahani ni mwanamke kwa hisani ya CHAMA CHA WATABIRI NA WAGANGA WA KIENYEJI TANZANIA
 
Hivi kama hatumtaki Benard Membe, watatushikia BUNDUKI kumpigia kura!? Ninawaahangaa sana Watanzania mnapolalamikia Salma Kikwete, wakati sisi (Watanzania) wenyewe ndio tutakaomua nani awe RAIS na SI SALMA KIKWETE au UKOO WA KIKWETE.
 
Mbona mama Salma Kikwete ni mwanasiasa siku nyingi tu, tangu mumewe awe rais na yeye aliingia kwenye siasa rasmi, so mimi hata simshangai
 
mama salma.JPG

Kinachomfanya awe na wasiwasi hata kujihami kiasi hiki ni BOFYA HAPA
 
Back
Top Bottom