Salma Kikwete anapomfanyia kampeni Rais ajaye

Salma Kikwete anapomfanyia kampeni Rais ajaye

Mkuu CTU, ni vyema ukasoma na kuelewa kabla huja anza kujivua nguo zako kwa kuonyesha uwezo wako mdogo wa kufikiria mambo.

  1. Nashukuru kwa kunifumbua macho mkuu CTU, kumbe Salma ndiye aliye mruhusu Kikwete kugombea urais mwaka 2005, mie nilidhani ni chama chake cha CCM. Hili nalo neno...........
  2. Hakuna aliyehoji Salma Kikwete kumpigia mumewe kampeni, bali ni Salma na watoto wao kushika nafasi kubwa za maamuzi kwenye chama. Jiulize, je hiki kilitokea kwa marais wengine walio tangulia?
  3. Ni dhahiri Dr.Slaa anawanyima usingizi, na msipoangalia kuna hatari ya kupata pressure, Stroke au vyote kwa pamoja ifikapo 2015. Tuambie Josephine Mshumbusi ana nafasi gani katika chama cha CHADEMA?
  4. Mkuu CTU ni vyema ukajibu maswali kwa kutoa hoja na siyo porojo na kutokwa na mapovu. Kwa mfano great thinker ameuliza kwa nini JK ameamua kupanga familia yake, ndugu na jamaa zake kwenye safu ya maamuzi ya chama? Ni dhahiri kuna kitu kinafichwa nyuma ya pazia. Je wajua Membe na Jakaya ni ndugu? na ndo huyo anayepigiwa upatu na Salma Kikwete ili awe mrithi wa Jakaya? on other hand wanataka kugeuza urais uwe wa familia? Tafakari.......chukua hatua !!!!!

Wanajanvi naomba kuwasilisha.
Hili ni jibu zuri saana kwa CTU na Magamba wenzie.
 
Bernard Membe ametangaza kutokugombea Ubunge 2015.(1) Niseme atagombea urais. Bernard Membe akishinda Urais 2015, basi shukrani zitamuendea Mama Salma Kikwete. Kwani hii shuguli imeonekana wazi pale Dodoma katika mkutano mkuu wa CCM ambako (2) mama Salma Kikwete, Nyalandu na Ridhiwani walifanya kampeni za waziwazi hadi hasa za kugawa hela na vitisho ili Membe na Rais Kikwete wachaguliwe kwenye kamati kuu. Hali iliyoleta mvutano mkubwa kati ya kada maarufu wa CCM Bashe na Waziri Membe. Ni katika nchi chache tu rais na familia yake wanajiingiza kwenye utawala wa nchi, ila kwetu hii familia ya Kikwete imeweza.

(3) Mama Salma ndiye mpiga debe mkuu wa Bernard Membe akisaidiwa na Dr. Kikwete na Mwanaye Ridhiwani.
(4)Lakini ni kwa nini Mama kama huyu na heshima zake ajiingize kwenye siasa? Kwa sasa mama kikwete ndiye mwakilshi wa Lindi NEC (CCM) Kadhalika mtoto wa Rais, Ridhiwani Kikwete ambaye ndiye mwakilishi kutoka Bagamoyo ambaye pia alipita bila kupingwa. Ndugu zake Kikwete nao wamechukua nafasi nyingi sana ndani ya CHAMA na serikali. Je tujiulize ni kwa nini?

Rais amemaliza muda wake, (5) anachokiogopa ni nini hadi kuwaweka watu wake kwenye nafasi nyeti mpaka kwenye urais? Rais mstaafu anapewa stahiki zake. Anapewa ulinzi maisha yake yote, anapewa, wasaidizi, Gari pamoja na Nyumba. Kwa nini hii familia iwe na hofu kiasi cha kuhakikisha madaraka wanabaki kwenye nafasi nzuri za madaraka?

Je(6) Familia ya Kikwete imewafanyia nini kibaya watanzania kiasi cha kuogopa? Wana nini cha kuficha? Je wamo kwenye ufisadi? Rais anajaribu kulinda maslahi gani? Ni maslahi ya kifedha au ni madhambi gani? Najaribu kutafakari kwa maana huyu mama kujikita kwenye siasa pindi mume wake akielekea kustaafu kunatia shaka. Mama mwinyi hakujiingiza kwenye siasa. Wake za rais waliopita hasa mwinyi na mkapa walijiingiza kwenye ufisadi lakini siyo siasa. Mama Nyerere hakujiingiza kwenye siasa. Mama mkapa hakujiingiza kwenye siasa. Kwa nini Mama Salma Kikwete? Hasa anapojaribu kutupachikia Waziri Membe kuwa Rais.

Mods: Tafadhalini. Huyu mama siyo mwanafamilia tena, bali mwanasiasa. Inabidi ajadiliwe kwani amekuwa mke wa kwanza wa Rais kujiingiza kwenye siasa ya nchi yetu. Tunaomba msiondoe au kuunganisha hii thredi
kwa nini una wasiwasi na mods? au habari yako ya kupika?majibu ya maeneo yenye bold kwa namba ni haya;

1.wewe anayekupa mamlaka ya kutangaza kwamba mtu flani atagombea urais ni nani?acha ;kama atagombea atasema mwenyewe.

2.wewe ulikuwepo dodoma na ukawaona watu hao wakimfanyia kampeni membe?kama haukuepo basi jupe chanzo cha habari unachorejea.

3.wewe ndiye unayempa mama salma hicho cheo au ni nani?

4.watu wenye heshma hawatakiwi kushiriki kwenye siasa?kama ndio kwa nini?hebu naambie kwa mujibu wa sheria za tanzania ni watu gani ambao hawana haki ya kushiriki katika siasa.

5.wewe nani kakuambia kwamba anaogopa?kawaida wewe unavyojua mtu anatafuta kuwa kiongozi sababu ya woga?

6.mimi kama mtanzania sioni kama familia hii imetufanyia watanzania ubaya wowote! sijui wewe mwenzangu familia hii imekufanyia ubaya wowote kwa sababu naamini nawe ni mtanzania.
 
Hivi kama hatumtaki Benard Membe, watatushikia BUNDUKI kumpigia kura!? Ninawaahangaa sana Watanzania mnapolalamikia Salma Kikwete, wakati sisi (Watanzania) wenyewe ndio tutakaomua nani awe RAIS na SI SALMA KIKWETE au UKOO WA KIKWETE.

Hamna uhalisia unaonyesha kuwa rais anayechaguliwa ametoka kwa wananchi kwa kura
 
kwa nini una wasiwasi na mods? au habari yako ya kupika?majibu ya maeneo yenye bold kwa namba ni haya;

1.wewe anayekupa mamlaka ya kutangaza kwamba mtu flani atagombea urais ni nani?acha ;kama atagombea atasema mwenyewe.

2.wewe ulikuwepo dodoma na ukawaona watu hao wakimfanyia kampeni membe?kama haukuepo basi jupe chanzo cha habari unachorejea.

3.wewe ndiye unayempa mama salma hicho cheo au ni nani?

4.watu wenye heshma hawatakiwi kushiriki kwenye siasa?kama ndio kwa nini?hebu naambie kwa mujibu wa sheria za tanzania ni watu gani ambao hawana haki ya kushiriki katika siasa.

5.wewe nani kakuambia kwamba anaogopa?kawaida wewe unavyojua mtu anatafuta kuwa kiongozi sababu ya woga?

6.mimi kama mtanzania sioni kama familia hii imetufanyia watanzania ubaya wowote! sijui wewe mwenzangu familia hii imekufanyia ubaya wowote kwa sababu naamini nawe ni mtanzania.

Tafakari maneno yako kwa maisha ya vizazi vijavyo na taifa lako
 
Tafakari maneno yako kwa maisha ya vizazi vijavyo na taifa lako
ni vizuri ukitaka mjadala uende vizuri uwe unajibu kilichoulizwa kuliko kufanya kazi ya kulaumu watu huku hutoi hoja.
 
Hivi nyie vijana wa Chadema mtaacha lini hizi siasa za kinafiki na majungu? Mama Salma ana kazi ya kumlea na kumuenzi mumewe; mama wa watu kajituliza bado mnawashwa na kuja kupiga majungu JF mbona hamumsemi Josephine anayekesha JF kupiga fitina kwa watu ambao ni tishio kwa slaa?

Chama
Gongo la mboto DSM

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:

ndio maana hata nyerere alisema "ukiona mtu anaanza kutajataja majina ya watu tu badala ya kutoa hoja ujue kafilisika."wamewataja taja viongozi wooote wameona haitoshi sasa wameamua kumchafua mama wa watu.

ninapata hofu na hatima ya Tanzania huko mbele ya safari kwani inaonekana mpaka sasa ndani ya ccm hakuna hasa anayefaa kuongoza nchi hii bali kinachofanyika ni kupapasa na kuwekana kwa faida za wachache.
 
Jamani naomba kujua nafasi ya mama Salma Kikwete ndani ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Maana kila siku nasikia alikuwa kwenye ziara mara Arusha, Mara, Mbeya, Rukwa. na katika kila ziara yake anatumia magari na rasimali za serikali, je yeye kama "First Lady" ni Kiongozi wa Serikali?
 
Nadhani ni mshauri mkuu wa rais kwenye mambo yote ya nchi...
 
Jamani naomba kujua nafasi ya mama Salma Kikwete ndani ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Maana kila siku nasikia alikuwa kwenye ziara mara Arusha, Mara, Mbeya, Rukwa. na katika kila ziara yake anatumia magari na rasimali za serikali, je yeye kama "First Lady" ni Kiongozi wa Serikali?
wewe kwanza kabla ya yote unatakiwa ujifunze ni nini serikali,ni nini taifa,ni nini chama cha siasa,na vitu kama hivi.kwa sababu hili la mama salma ni nani;nadhani hata ukiuliza barabarani watakujibu; ila hayo niliyokuambia mpaka usome kitabu cha uraia cha form one.
 
Jamani naomba kujua nafasi ya mama Salma Kikwete ndani ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Maana kila siku nasikia alikuwa kwenye ziara mara Arusha, Mara, Mbeya, Rukwa. na katika kila ziara yake anatumia magari na rasimali za serikali, je yeye kama "First Lady" ni Kiongozi wa Serikali?
katiba yetu inasemaje juu ya kumtambua mke wa rais na majukumu yake? kama haisemi chochote basi anatumalizia hela zetu na kampeni zake za shuka kwa shuka zisizoisha.
 
View attachment 78730

Ila ataiweza kambi ya EL? Maana kina NAPE na jasusi MKama walimshindwa kwenye operation ya GAMBA. Na pia ameweza kupandikiza wajumbe wengi kwenye NEC.
 
Kichwa cha hii thread jakiendani na ulichoandika! Nahisi unayo hoja ila ni namna tu unavyotoa hoja ndio inatia shaka! Angalia wasije wakasema umetumwa na Bashe?!

.....
Bernard Membe ametangaza kutokugombea Ubunge 2015. Niseme atagombea urais. Bernard Membe akishinda Urais 2015, basi shukrani zitamuendea Mama Salma Kikwete.

Kwani hii shuguli imeonekana wazi pale Dodoma katika mkutano mkuu wa CCM ambako mama Salma Kikwete, Nyalandu na Ridhiwani walifanya kampeni za waziwazi hadi hasa za kugawa hela na vitisho ili Membe na Rais Kikwete wachaguliwe kwenye kamati kuu. Hali iliyoleta mvutano mkubwa kati ya kada maarufu wa CCM Bashe na Waziri Membe.

Ni katika nchi chache tu rais na familia yake wanajiingiza kwenye utawala wa nchi, ila kwetu hii familia ya Kikwete imeweza.

Mama Salma ndiye mpiga debe mkuu wa Bernard Membe akisaidiwa na Dr. Kikwete na Mwanaye Ridhiwani. Lakini ni kwa nini Mama kama huyu na heshima zake ajiingize kwenye siasa?

Kwa sasa mama kikwete ndiye mwakilshi wa Lindi NEC (CCM) Kadhalika mtoto wa Rais, Ridhiwani Kikwete ambaye ndiye mwakilishi kutoka Bagamoyo ambaye pia alipita bila kupingwa. Ndugu zake Kikwete nao wamechukua nafasi nyingi sana ndani ya CHAMA na serikali. Je tujiulize ni kwa nini?

Rais amemaliza muda wake, anachokiogopa ni nini hadi kuwaweka watu wake kwenye nafasi nyeti mpaka kwenye urais? Rais mstaafu anapewa stahiki zake.

Anapewa ulinzi maisha yake yote, anapewa, wasaidizi, Gari pamoja na Nyumba. Kwa nini hii familia iwe na hofu kiasi cha kuhakikisha madaraka wanabaki kwenye nafasi nzuri za madaraka?

Je Familia ya Kikwete imewafanyia nini kibaya watanzania kiasi cha kuogopa? Wana nini cha kuficha? Je wamo kwenye ufisadi? Rais anajaribu kulinda maslahi gani?

Ni maslahi ya kifedha au ni madhambi gani? Najaribu kutafakari kwa maana huyu mama kujikita kwenye siasa pindi mume wake akielekea kustaafu kunatia shaka. Mama mwinyi hakujiingiza kwenye siasa.

Wake za rais waliopita hasa mwinyi na mkapa walijiingiza kwenye ufisadi lakini siyo siasa. Mama Nyerere hakujiingiza kwenye siasa. Mama mkapa hakujiingiza kwenye siasa. Kwa nini Mama Salma Kikwete? Hasa anapojaribu kutupachikia Waziri Membe kuwa Rais.

Mods: Tafadhalini. Huyu mama siyo mwanafamilia tena, bali mwanasiasa. Inabidi ajadiliwe kwani amekuwa mke wa kwanza wa Rais kujiingiza kwenye siasa ya nchi yetu. Tunaomba msiondoe au kuunganisha hii thredi.
 
Bernard Membe ametangaza kutokugombea Ubunge 2015. Niseme atagombea urais. Bernard Membe akishinda Urais 2015, basi shukrani zitamuendea Mama Salma Kikwete. Kwani hii shuguli imeonekana wazi pale Dodoma katika mkutano mkuu wa CCM ambako mama Salma Kikwete, Nyalandu na Ridhiwani walifanya kampeni za waziwazi hadi hasa za kugawa hela na vitisho ili Membe na Rais Kikwete wachaguliwe kwenye kamati kuu. Hali iliyoleta mvutano mkubwa kati ya kada maarufu wa CCM Bashe na Waziri Membe. Ni katika nchi chache tu rais na familia yake wanajiingiza kwenye utawala wa nchi, ila kwetu hii familia ya Kikwete imeweza.

..........

Hii yote ni kwa sababu nchi haina miiko ya uongozi. Kila raisi anayeingia madarakani anakuja na style yake. Binafsi haya ni kati ya matumizi mabaya ya madaraka ya viongozi wetu.

Haiwezekani mke wa raisi au watoto au ndugu wanaibuka ghafla na kuanza kushika nyazifa mbalimbali za juu ktk chama wakati kuna wakada wengi waliokitumikia chama hiki ktk maeneo hayo.

Hii ni jeuri ya madaraka na matusi kwa wasio na uwezo. Haya ndio matatizo ya wanaCCM kuendelea kuhabudu wenye pesa na madaraka.
 
Mna upeo mdogo nyie, kwani babu ni rais, hapa tunazungumzia mke wa urais basi nimekuelewa kumbe babu ni rais ajae.

umesoma post yangu ya kwanza kwa umakini? au umesoma juu juu tu?? bila kuipambanua
 
Membe bado hata CCM wenyewe na wanasema bado? Na hakuna katika historian ya Tanzania MTU ambaye aliungwa mkono na familia namba moja akapita. Rejea awamu zote za utawala utabaini ukweli huu!
 
Back
Top Bottom