Ni kweli, Salim Kikeke na Charles Hillary ni moja ya watangazaji(wana habari) wa kuigwa kila unapotazama wanapowahoji watu, wanapotangaza n.k wanaonyesha kujiamini, kupenda kazi yao(no offense kwa watangaziji wetu) lakini ni kweli nanyi pia mnavutiwa na utendaji wao wa kazi.
Mara kadhaa, imekuwa kama desturi/kawaida/mazoea fulani kwa watangazaji kutuhabarisha wakiwa wamevaa T-shirts(fulana), hasa za kimichezo! Wakati mwingine unajiuliza hivi huyu yuko kazini kweli?Inamaana hata kazini(Studio) hapo hakuna Changing room iliyo equiped??! ..Natambua lengo ni kutuhabarisha, lakini hata ule mvuto wa kutotaka kuondoa wakati wa Commercial break haupo, inakuwa mtu unasubiri habari fulani tu!
Hebu watangazaji wetu, wabadilike..lakini tuwapongeze kwa jitihada zao za kila siku katika kuelekea mabadiliko hayo!