Salim Kikeke na Charles Hilary wa BBC SWAHILI, hakunaga kama hawa jamaa...

bampami

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
5,697
2,000
Kusema ukweli mimi huwa navutiwa sana na salim kikeke pamoja na charles hilali wakitangaza BBCSWAHILI Tv kupitia Startv hawa jamaa hasa salim ana rafudhi fulani ya mvuto inayotengeneza attention ya kumwangalia. Salimu kikeke amekuwa ni mmojawapo watangazaji wabunifu zaidi na huwaga napenda sana anapotangaza speed yake na unadhifu wake.
Watangazaji wa Tbc1, Itv na startv tujifunze kusoma habari kama hawa jamaa mpo slow sana mnaposoma habari hasa startv na itv.
Watz 2jifunie hawa watz wanaopeperusha bendera ye2 nje.
 
Tuliwonda

Senior Member
Jun 29, 2012
120
195
kwa kweli hata mm wananivutia mno hawa jamaa! Siku hizi ikifika saa tatu usiku natune startv kuangalia BBC SWAHILI! Pamoko sana wakuu.
 
Chiya Chibi

JF-Expert Member
Jul 6, 2011
484
195
Watangazaj we2 hapa, wana visingizio vingi,
1; Vifaa duni
2; Mharir wa habar husika, haaminiki kwahyo habar inasomwa kwa mashaka.
3;Haikuwa zam yake kuwa studio, siku hiyo.
4;Mishahara imechelewa
5;Shida za kijamii/Familia
6;Amesemwa vibaya facebook, twitter, Jf n.k

Achen wakina Kikeke na mwenzake wajitanue pale, wana uhuru na uhakika kwa kila wanachokifanya.
 
Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,060
2,000
mimi nawapenda sana wanavyotangaza sana sana,asa salim kikeke anavyotingisha tingisha kichwa ni kama ana nywele nyingi,kumbe ana upala kichwan,yani ni vivutio tosha,mungu awabalik na kuwalinda tuzidi kufurahi kwa kweli
 
hippocratessocrates

JF-Expert Member
Jul 1, 2012
3,601
2,000
Ni kweli, Salim Kikeke na Charles Hillary ni moja ya watangazaji(wana habari) wa kuigwa kila unapotazama wanapowahoji watu, wanapotangaza n.k wanaonyesha kujiamini, kupenda kazi yao(no offense kwa watangaziji wetu) lakini ni kweli nanyi pia mnavutiwa na utendaji wao wa kazi.

Mara kadhaa, imekuwa kama desturi/kawaida/mazoea fulani kwa watangazaji kutuhabarisha wakiwa wamevaa T-shirts(fulana), hasa za kimichezo! Wakati mwingine unajiuliza hivi huyu yuko kazini kweli?Inamaana hata kazini(Studio) hapo hakuna Changing room iliyo equiped??! ..Natambua lengo ni kutuhabarisha, lakini hata ule mvuto wa kutotaka kuondoa wakati wa Commercial break haupo, inakuwa mtu unasubiri habari fulani tu!

Hebu watangazaji wetu, wabadilike..lakini tuwapongeze kwa jitihada zao za kila siku katika kuelekea mabadiliko hayo!
 
Marumia

JF-Expert Member
Feb 11, 2012
644
0
Salim yuko vizuri kwa kweli, maana anaheshimu muda wa mtazamaji hataki kukufanya ujiskie umepoteza muda wako kumsikiliza na kumtizama. Heko... kwa wawili hawa!
 
bampami

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
5,697
2,000
kwa kweli hata mm wananivutia mno hawa jamaa! Siku hizi ikifika saa tatu usiku natune startv kuangalia BBC SWAHILI! Pamoko sana wakuu.

Basi huwaga wanavijihabari fulani vya ajabu lakini vina mvuto kweli, kama jana walitoa habari ya bunge la ukraine walivokuwa wakizichapa bungeni was so fun kwakweli. Watz 2na haki ya kujivunia hawa wa2.
 
bampami

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
5,697
2,000
Ni kweli, Salim Kikeke na Charles Hillary ni moja ya watangazaji(wana habari) wa kuigwa kila unapotazama wanapowahoji watu, wanapotangaza n.k wanaonyesha kujiamini, kupenda kazi yao(no offense kwa watangaziji wetu) lakini ni kweli nanyi pia mnavutiwa na utendaji wao wa kazi.

Mara kadhaa, imekuwa kama desturi/kawaida/mazoea fulani kwa watangazaji kutuhabarisha wakiwa wamevaa T-shirts(fulana), hasa za kimichezo! Wakati mwingine unajiuliza hivi huyu yuko kazini kweli?Inamaana hata kazini(Studio) hapo hakuna Changing room iliyo equiped??! ..Natambua lengo ni kutuhabarisha, lakini hata ule mvuto wa kutotaka kuondoa wakati wa Commercial break haupo, inakuwa mtu unasubiri habari fulani tu!

Hebu watangazaji wetu, wabadilike..lakini tuwapongeze kwa jitihada zao za kila siku katika kuelekea mabadiliko hayo!

hippo umenena kweli kabisa
 
Aug 2, 2012
51
0
Utawapenda zaidi wakiwa wanatangaza mpira ligi ya Uingereza kwa vijimaneno vimisemo na utani wa hapa na pale inakuwa ni zaidi ya mpira,kuna jamaa aliwahi kuniambia kuwa huyu Saleem Kikeke ni mkeiii.?
 
bampami

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
5,697
2,000
Utawapenda zaidi wakiwa wanatangaza mpira ligi ya Uingereza kwa vijimaneno vimisemo na utani wa hapa na pale inakuwa ni zaidi ya mpira,kuna jamaa aliwahi kuniambia kuwa huyu Saleem Kikeke ni mkeiii.?

wanajitahidi japo hawamfiki enzi hizo za radio tanzania akina juma nkamia
 
Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
48,709
2,000
Daah hawa jamaa ni wazuri kiutangazaji wananifanya nisikose kipindi, kwakweli wanatangaza vizuri hadi mtu unatamani wasimalize!

Big up kwao!
 
Makala Jr

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
3,395
1,195
Nawakubali sana hawa jamaa haswa voice level,facial expressions,smartness,timeliness,confidence,proper interviewing when they invited a guest e.t.c Hawa ndiyo media professionals.Kwanza ni wacheshi,mfano juzi hapo Salim anakwambia Wabrazil wanapinga rekodi ya Messi kufunga mabao mengi kwa mwaka lakini hata yeye Salimu Kikeke alifunga mabao kama 200 alipokuwa shule ya msingi tatizo ni upatikanaji wa kumbukumbu sahihi...Mungu awabariki watu hawa kwani hizi media za bongo wamiliki wana kadi za ccm na chama hicho ndo kimeilemaza TBC 1 basi ndo hata hawajifunzi lol
 
PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,119
2,000
BBC swahili DIRA YA DUNIA wameanza kuniudhi siku za karibuni hasa baada ya kuanza kutangaza raia wa kenya kama watangazaji ambao hata kiswahili hawakielewi vizuri inaboa sana na hii ni baada ya TIDO kuondoka kama mkuu wa idhaa ya kiswahili yupo mkenya mmoja pale sasa kama Bosi wa idhaa ya kiswahili.Nawapenda sana akina Zuhura Yunis, Zawad Machibya, Salim Kikeke, Charles Hillal. Wanaoboa wanaongozwa na Odhiambo Joseph, Ngenda Angela na wenzake .
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom