2019
JF-Expert Member
- Dec 31, 2018
- 2,982
- 4,458
Kisa hiki kitakuwa na episode 2 tu ili nisichoshe wasomaji. Kisa cha kweli ambacho huwa nakumbuka kinaniuma sana nilishaapa sitorudia tena,nikikumbuka yaliyotokea naamini kabisa wanawake wakipenda wanakuwa vipofu kabisa hawaoni madhara ya mbele.
Ilikuwa mwaka 2012 nikiwa nimepanga getto pale Side A,geto tulipanga wawili (mchango) lakini badae walikuja washkaji na baadhi ya ndugu wa jamaa kwa hiyo tulifika mpaka watu 6 wakati mwingine. Geto kulikuwa hakupikwi na hakukuwa na vitu vingi sana ni radio na deki tu.
Baadae kwenye hiyo nyumba alikua jamaa mmoja kupanga alikua na mke na mtoto 1 wa kike ana miaka kama 3 hivi huyo jamaa alikua mtu tungi sana,hakuna siku atarudi nyumbani hajanywa na pesa alikua nayo.
Pale geto kila mtu alikua na mishe zake mm nikua nafanya kazi duka la nguo KKoo tulikua tunafunga saa 11 kamili jioni na kutoka kkoo mpaka geto ni dk 30 kwa mguu kwa hiyo mimi nilikua nawahi kuliko watu wote pale geto. Nilikua sina makundi kabisa mtaani yani nikirudi nafika ndani najifungia nachezea simu yangu mpaka saa 2 usiku naenda kula narudi zangu kulala sababu nilikua nawahi kuamka pia.
Sasa baada ya jamaa kuhamia pale na familia yake hakutua tumezoana sana ni ile salamu tu kila mtu anapita zake. Ukapita muda kidogo mke wa jamaa alikua mama wa nyumbani alikua na mimba ndogo.
Muda mwingi nikitoka kazini namkuta kakaa nje amepumzika kumbe ananichora na kujiuliza maswali kadhaa kichwa. Siku moja akaniita akaniambia kwanini napenda kukaa ndani mwenyewe? Nikamwambia sina mazoea ya kupiga stori na watu,akaniambia njoo nje tupige stori,basi nikaitikia lakini kwa shingo upande sababu kwanza sipendi mazoea na wake za watu.
Kikubwa aliniambia ana simu yake ya kubadilisha cover nokia flani hivi zilikua na keyboard ya Qwerty nimesahau model yake. Basi ikawa kawaida kila nikitoka kazini badala ya kwenda ndani nakuta katoa mkeka wake nakaa tunapiga stori za kawaida kabisa.
Akanidokeza kuwa mumemwe anataka kumunua TV kubwa flat screen (walikua wanatumia chogo) kwa hiyo nifanye mpango niinunue hiyo tv na hata kama nina pesa kidogo nisijali nimwachie yeye. Basi alifanya mpango kweli mumewe akaniuza ile tv kwa 40k tu.
Pale hawakukaa sana sababu ya migogoro ya umeme wakatafuta nyumba sehemu ya karibu Side B,basi kabla ya kuhama akanishawishi sana nihame nitafute chumba cha peke yangu sababu kukaa geto na watu wengi siwezi kufanya mambo mengi na nitajichelewesha kimaendeleo sababu sitanunua vitu vya ndani. Alikomaa sana na mimi hata akaniambia kuna chumba kimepatikana karibu na wanapohamia lakini mm pale ilikua bado miez 3 kodi iishe. Sikukubaliana na wazo lake japo lilikua zuri lakini mimi niliwaza kodi yangu na kwenda kupanga mwenyewe miezi 6 niandae 180k🤔 nikaona haiwezekani.
Basi ikafika siku ya kuhama akanipa namba yake ya simu na kujitahidi sana kunielekeza lakini bado sikupajua sababu Side B sikuwah kufika huko. Akaniakarubisha kwake niwe namtembelea nikamwahidi nitakuja(nifanya hivyo ili aridhike tu) lakini sikuwa na wazo la hata kumpigia simu.
Akahama na mimi nikafuta namba yake kwa sababu hizi
1. Sio jirani yangu tena,nimpigie simu nimwambie nini?
2. Ni mke wa mtu kwanini niwe nawasiliana naye,mumewe akijua atanihisije?
3. Sina biashara nae iwe lazma tuwasiliane kwa karibu.
Basi maisha yakasonga kodi pale ikaisha kuna ndugu yangu nae alitaka hifadhi na pale geto nafasi hakuna ikabidi nijipe changamoto za kikubwa sasa,nikaamua kwenda kupanga mwenyewe ila niliwaza sana kununua vitu vya ndani ndio mana nilikua sitaki.
Katika kutafuta nyumba nikapata Side B wakati huo nishasahau hata nilikua na jirani anaeitwa mama fulani. Nikahamia geto na ndugu zangu wawili mmoja alikua chuo Muhimbili na mwingine ni mgangaji ka mimi.
Muda kidogo ukasonga siku narudi zangu kazini ilikua saa 8 mchana jumapili tulikuwa tunafunga mapema mpaka nifike geto nilikua napita maduka mtaani nikashangaa naitwa 2019 nikageuka nikakuta ni mama fulani...badi alikua anasuka ilibidi atoke nje haraka sana kuja kunisalimi, basi tulipiga stori kidogo lawama kama zote namba kanipa lakini sikumtafuta basi mm nikajitete namba nilipoteza mana kipindi hicho nikua nabadili sana simu.
Akanielekeza kwake alikua kashajifungua ilikua 2014 mwanzoni hapo na kuniambia yule ndugu yako anaesoma anapitaga karibu na anapokaa kama vipi nimwambie anilete,mimi nikaitikia kusema kweli bado sijuona faida ya kwenda kwake. Akanipa namba upya pale akarudi kusukwa.
Sikudumu sana na ile namba wala sikuitumia nikaifuta muda tena ukapita tena akajanitega pale pale saluni nikapita akaniita tukaongeaa kila nikikutana nae ni lawama tu. Basi akanipa namba tena mara hii nikajisemea mh!
Huyu ataniona nina dharau sasa,yule jamaa angu nikajaribu kumuuliza unamiumbuka mama fulani tulipanga nae nyumba moja kule Side A? Akasema anajua alipo,basi nikapanga jumapili 1 tuende kukamsalimie,jpili iliyofuata tukafanya hivyo tukaenda mpaka kwake,tulikuta kalala.
Itaendelea someni kwanza hiyo naendelea kutype ingine...