Salamu yangu ilivyovunja ndoa ya mtu, niliumia sana, mpaka leo nakumbukaga tu

2019

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
2,982
4,457
Kisa hiki kitakuwa na episode 2 tu ili nisichoshe wasomaji. Kisa cha kweli ambacho huwa nakumbuka kinaniuma sana nilishaapa sitorudia tena,nikikumbuka yaliyotokea naamini kabisa wanawake wakipenda wanakuwa vipofu kabisa hawaoni madhara ya mbele.

Ilikuwa mwaka 2012 nikiwa nimepanga getto pale Side A,geto tulipanga wawili (mchango) lakini badae walikuja washkaji na baadhi ya ndugu wa jamaa kwa hiyo tulifika mpaka watu 6 wakati mwingine. Geto kulikuwa hakupikwi na hakukuwa na vitu vingi sana ni radio na deki tu.

Baadae kwenye hiyo nyumba alikua jamaa mmoja kupanga alikua na mke na mtoto 1 wa kike ana miaka kama 3 hivi huyo jamaa alikua mtu tungi sana,hakuna siku atarudi nyumbani hajanywa na pesa alikua nayo.

Pale geto kila mtu alikua na mishe zake mm nikua nafanya kazi duka la nguo KKoo tulikua tunafunga saa 11 kamili jioni na kutoka kkoo mpaka geto ni dk 30 kwa mguu kwa hiyo mimi nilikua nawahi kuliko watu wote pale geto. Nilikua sina makundi kabisa mtaani yani nikirudi nafika ndani najifungia nachezea simu yangu mpaka saa 2 usiku naenda kula narudi zangu kulala sababu nilikua nawahi kuamka pia.

Sasa baada ya jamaa kuhamia pale na familia yake hakutua tumezoana sana ni ile salamu tu kila mtu anapita zake. Ukapita muda kidogo mke wa jamaa alikua mama wa nyumbani alikua na mimba ndogo.

Muda mwingi nikitoka kazini namkuta kakaa nje amepumzika kumbe ananichora na kujiuliza maswali kadhaa kichwa. Siku moja akaniita akaniambia kwanini napenda kukaa ndani mwenyewe? Nikamwambia sina mazoea ya kupiga stori na watu,akaniambia njoo nje tupige stori,basi nikaitikia lakini kwa shingo upande sababu kwanza sipendi mazoea na wake za watu.

Kikubwa aliniambia ana simu yake ya kubadilisha cover nokia flani hivi zilikua na keyboard ya Qwerty nimesahau model yake. Basi ikawa kawaida kila nikitoka kazini badala ya kwenda ndani nakuta katoa mkeka wake nakaa tunapiga stori za kawaida kabisa.

Akanidokeza kuwa mumemwe anataka kumunua TV kubwa flat screen (walikua wanatumia chogo) kwa hiyo nifanye mpango niinunue hiyo tv na hata kama nina pesa kidogo nisijali nimwachie yeye. Basi alifanya mpango kweli mumewe akaniuza ile tv kwa 40k tu.

Pale hawakukaa sana sababu ya migogoro ya umeme wakatafuta nyumba sehemu ya karibu Side B,basi kabla ya kuhama akanishawishi sana nihame nitafute chumba cha peke yangu sababu kukaa geto na watu wengi siwezi kufanya mambo mengi na nitajichelewesha kimaendeleo sababu sitanunua vitu vya ndani. Alikomaa sana na mimi hata akaniambia kuna chumba kimepatikana karibu na wanapohamia lakini mm pale ilikua bado miez 3 kodi iishe. Sikukubaliana na wazo lake japo lilikua zuri lakini mimi niliwaza kodi yangu na kwenda kupanga mwenyewe miezi 6 niandae 180k🤔 nikaona haiwezekani.

Basi ikafika siku ya kuhama akanipa namba yake ya simu na kujitahidi sana kunielekeza lakini bado sikupajua sababu Side B sikuwah kufika huko. Akaniakarubisha kwake niwe namtembelea nikamwahidi nitakuja(nifanya hivyo ili aridhike tu) lakini sikuwa na wazo la hata kumpigia simu.

Akahama na mimi nikafuta namba yake kwa sababu hizi
1. Sio jirani yangu tena,nimpigie simu nimwambie nini?
2. Ni mke wa mtu kwanini niwe nawasiliana naye,mumewe akijua atanihisije?
3. Sina biashara nae iwe lazma tuwasiliane kwa karibu.

Basi maisha yakasonga kodi pale ikaisha kuna ndugu yangu nae alitaka hifadhi na pale geto nafasi hakuna ikabidi nijipe changamoto za kikubwa sasa,nikaamua kwenda kupanga mwenyewe ila niliwaza sana kununua vitu vya ndani ndio mana nilikua sitaki.

Katika kutafuta nyumba nikapata Side B wakati huo nishasahau hata nilikua na jirani anaeitwa mama fulani. Nikahamia geto na ndugu zangu wawili mmoja alikua chuo Muhimbili na mwingine ni mgangaji ka mimi.

Muda kidogo ukasonga siku narudi zangu kazini ilikua saa 8 mchana jumapili tulikuwa tunafunga mapema mpaka nifike geto nilikua napita maduka mtaani nikashangaa naitwa 2019 nikageuka nikakuta ni mama fulani...badi alikua anasuka ilibidi atoke nje haraka sana kuja kunisalimi, basi tulipiga stori kidogo lawama kama zote namba kanipa lakini sikumtafuta basi mm nikajitete namba nilipoteza mana kipindi hicho nikua nabadili sana simu.

Akanielekeza kwake alikua kashajifungua ilikua 2014 mwanzoni hapo na kuniambia yule ndugu yako anaesoma anapitaga karibu na anapokaa kama vipi nimwambie anilete,mimi nikaitikia kusema kweli bado sijuona faida ya kwenda kwake. Akanipa namba upya pale akarudi kusukwa.

Sikudumu sana na ile namba wala sikuitumia nikaifuta muda tena ukapita tena akajanitega pale pale saluni nikapita akaniita tukaongeaa kila nikikutana nae ni lawama tu. Basi akanipa namba tena mara hii nikajisemea mh!
Huyu ataniona nina dharau sasa,yule jamaa angu nikajaribu kumuuliza unamiumbuka mama fulani tulipanga nae nyumba moja kule Side A? Akasema anajua alipo,basi nikapanga jumapili 1 tuende kukamsalimie,jpili iliyofuata tukafanya hivyo tukaenda mpaka kwake,tulikuta kalala.

Itaendelea someni kwanza hiyo naendelea kutype ingine...
 
Basi akaamshwa na mtoto wake yule mkubwa akatoka nje akatukarisha lakini hatukutaka kuingia ndani sababu nilimwabia tutakuja rasmi leo tumekuja kupajua tu anapokaa,akasema kwanini sikumpa taarifa hata atuandalie chochote kitu lakini nikamtoa wasi wasi kuwa asijali tuko vizuri,tukaondoka pale.

Sasa hapo ikabidi niwe namtafuta siku moja moja kwa salamu tu ila mara nyingi sikutaka kutumia muda kuchat nae sana.

Tena nakumbuka text ya kwanza ilikua wasap nilimwambia "kumbe upo wasap?"Akacheka tukaendelea kidogo nikaachana nae.

Nani anakumbuka kipindi kile cha migomo ya wafanyabishara kariakoo kukataa madhine za EFD? Nakumbuka ilikua j4 hapo ilikua mwishoni mwa 2014 nimeenda kkoo nikakuta kuna mgomo siku hiyo ikabidi nirudi home l,nimefika geto tu ikaingia text yake "mambo" nikajibu powa akauliza "uko wapi"? Nikajib leo kuna mgomo nimerudi nyumbani akareplay "nielekeze kwako nije" dah! Hata nilibak kwanza mdomo wazi najiuliza aje!!!! Akionekana anaingia huku nitaonekanaje? Mwenye nyumba akimuona je? Wakati najiuliza maswali hayo akatuma ingine "au hutaki kusalimiwa" nikamwelekeza afu mwisho nikamalizia lakini natoka saivi naenda Karume sokoni akasema ngoja aoshe vyombo aje mara moja, akasema kwan Karume unakaa mpaka saa ngap? Nikamwambia mpaka saa 10 jioni basi akasema ukirudi nistue basi...

Nikaenda ila nikakaa makusudi ili nichelewe kurudi mana sikutaka aje pale geto,nilirud mida ya saa 1 🌃 nikamtumia Text ndio narusi akajibu basi tena mpaka siku ingine mana mume wake kasharudi afu anapika,nikajisemea bora.

Tukazoeana kawaida akanikopa 20k kuna zaga alitaka nlkununua kwa miadi mumewe akirudi atarejesha nikampa kweli kesho yake ikarudi, tumechat kama wiki hakupatikana tena kwenye simu.

2015 katikati akanicheki yeye kwa namba mpya akadai ile mumewe aliikatakata sababu ya wasi was wa chat zake. Kwa muda wote huo sikuwahi kumwambia chochote kuhusu mahusiano wala yeye hakuniambia pia.

Akasema namba yangu hatosave ila anaijua kichwani na mume wake ameshaikariri pia,basi akafunguka mwenyewe aliandika hivi "2019 NAJUA KUNA KITU UNATAKA KUNIAMBIA LAKINI UNAOGOPA USIOGOPE NIAMBIE TU UKO HURU". Nikaona sasa hapa nikizubaa tena atanidharau au hata kunihizi vibaya basi mimi nikamjibu "WEWE MWENYEWE UNAJUA MBONA"

Dah!! Kwanza mwili ulikua unasisimuka sana kwa wasi wasi nikiwaza huyu ni mke wa mtu,mumewe hamtoshelezi? Basi akanimbia ni siku gani nina muda anifurahishe? Nikamwambia labda jpili mana ndio huwa narudi mapema,jpili kwake ikawa ngumu sababu siku hiyo pia mumewe haendi kazini muda mwingi anakuwa home.

Akanimbia nisingizie naumwa nibaki nyumbani ili nitimize lengo lake, nikamwambia nikisema naumwa boss wangu atanifata na gari kunichukua sa ataniona muongo,swala la siku ikawa mtihani mwingine tena...aliniambia jambo ambalo sikulipenda kabisa "kwa mfano nikiachana na huyu jamaa utanioa"🙄 nikamjibu usifanye hivyo haitaleta picha nzuri mbele ya jamii(sikutaka kujua sababu ya yeye kutaka kuachana nae) baada ya muda tena akapotea tena hewani tena mara ya pili hii.

Nilikuja kukutana nae tena 2015 siku ya uchaguzi nikiwa na jamaa angu(sio yule wa kusoma) jirani ambaye tulishibana sana. Tulitoka kupiga kura tukapita karibu na anapokaa akaja fasta akaniita pembeni akaniambia kabadilisha namba sababu ile ilivunjwa tena na mumewe siku si nyingi atanipa hiyo mpya. Wakati huu mi mwenyewe nina mpango wa kuishi na mtu mwakani 2016.

Basi toka siku ya uchaguzi nilikuja kumuona mwezi kama wa 11 tulikua na jamaa angu baa flani tunakula kilaji akaja yeye na rafiki yake alikua amependeza sana mana alitoka kaka sio mama wa nyumbani alivaa kisichana sana,afu alikua kaumbika kiasi mfupi kidogo,nikawachukulia 🍺 1 kila mtu (kabla ya siku hiyo sikuwahi kujua kama anakunywa) wakamaliza akasema akimsindikiza rafikiye sehemu sa acha awahi home sababu ana familia.

Baada ya kutoka pale jamaa angu akameza sana mate kumuhusu hata akataka nimuungie. Nilimweleza kwa kifupi tu tulivyojuana lakini jamaa alinitoa akili sana na kuona mi ni mshamba. Hapo sina namba yake tumeonana sasa mara ya pili bila kuwasiliana siku ile ya uchaguzi na siku hiyo.

Ilikua tar 24-12-2015 yan kesho ni Xmas akaja mjini kufanya manunuzi,dukani kwetu tulikua tunauza mpaka nguo za kutoto na pembeni yake kulikua na goli la nguo za kike akaja kwenye hilo goli akaniona akasogea mpaka dukani,nilikua natundika nguo na bos wangu nae alikua kasimama,akasalimia lengo lake alitaka kunipa namba lakini akajifanya anapita tu akazunguka akarudi akakuta nipo mwenyewe na akaniachia namba tena...

Siku ikaisha tukaamkia tar 25 Xmas yenyewe mimi mzigoni kama kawaida lakini tukua tunafunga mapema,baada ya kufunga nikamchek jamaa angu yuko free tukaingia chimbo kula vitu,ilikua saa tisa kama na nusu hivi nikajisemea ngoja nimchek alieniachia namba nikamtumia msg "HABARI?" Lengo la kutuma text ka hiyo ili hata ikisomwa na yeyote isilete shida kaka mtuhumiwa


inaendelea ya mwisho hii...
 
Vivulana vya kariakoo na wake za watu.MTU aliyeserious na kutodate na mbunye ya MTU asingeweza pitia mlolongo wote huo.Eti anatoa mkeka tunapiga story za kawaida;!?! Aisee,kweli kuna haja ya kuelimisha watoto wa kiume namna ya kuwa wanaume.Kiufupi ulivunja ndoa ya mtu bila bahati mbaya
 
Back
Top Bottom