Salamu ya HUJAMBO ni sawa kuipokea kwa mtu unayemzidi umri?

frenderPH

JF-Expert Member
Oct 30, 2019
619
806
Kama kichwa cha habari kinavyosema, ninapenda kujua tu Kwa upende niliokulia mimi sio sawa kwa mtu ninayemzidi umri kuniambia UJAMBO bali hii salamu ni kwa ajili ya mtu mzima akimwambia mtu mdogo ambae ni tegemezi kwake mfano

Baba: Ujambo mwanangu?

Mtoto kama kuna inshu inamtatiza atajibu NINA JAMBO na kama hana shida yoyote atajibu SIJAMBO.

Sasa leo katika pita pita zangu hapa kitaa ninapokaa, kuna binti Jirani na nimtoto wa 2004 ila anamwili mkubwa, hatujawahi kuongea wala kusalimiana cuz ni aina ya binti wale maslay queen ambao kwa upande wangu sio type yangu, ila hua uwa tunaonana kwa mbali na the way anavyoniangalia ni mithiri ya kwamba anahitaji kuongea na mimi, waliosoma saikolojia wanaelewa cuz unaweza kumsoma mtu kwa body language na facial expression anayoionesha kwako. Basi leo kipindi natoka Job nimemkuta ameketi kibalazani kwao na kwakua njia iko karibu na kibalaza chao nikaona sio mbaya nikimpa hai Convo ilikua hivi

Me: Za saizi binti
Her: Salama aka-pause alafu then UJAMBO?
Me: Nini?
Her: Ujambo?
Me: Mmh hii mpya

Nikamuacha anacheka huku hajiamini flani hivi

Sasa sijui kama nimemjibu vibaya au laa hio kwangu sio inshu cuz sina time nae, ninachotaka kujua ni hii salamu ya UJAMBO inafaa kuulizwa na mtoto mdogo kweli au mimi ukoloni unanisumbua?
 
'kibalazani - kibarazani', 'ujambo - hujambo', 'za saizi - za saa hizi'!

Huwa nasimama kinyume na baadhi ya watu wanaoiharibu lugha adhimu ya Kiswahili!

Baadhi ya sehemu salamu ya 'Hujambo' hutumika kwa wenye rika sawa pia hivyo isikuchanganye sana, naamini alikuwa sawa kwa upande wake, hukupaswa kushtuka hivyo kama vile umeshuhudia muujiza!
 
'kibalazani - kibarazani', 'ujambo - hujambo', 'za saizi - za saa hizi'...!
Huwa nasimama kinyume na baadhi ya watu wanaoiharibu lugha adhimu ya Kiswahili..!!

Baadhi ya sehemu salamu ya 'Hujambo' hutumika kwa wenye rika sawa pia hivyo isikuchanganye sana, naamini alikuwa sawa kwa upande wake, hukupaswa kushtuka hivyo kama vile umeshuhudia muujiza..!!

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Ni dharau mdogo kumwambia ujambo wakati yeye ni mdogo...

Hizi salamu mara nyingi ni za watu wakubwa wanasalimu wadogo..

Mf; Baba kwa mtoto

Mama kwa mtoto

Nb: Salamu sio lazima
 
Swali

Hujambo = unajambo/una tatzo

Jibu

Sijambo = sina jambo/sina tatzo...Yani nipo salama.

Nadhan nimeeleweka
 
Mkuu take it easy, kwa upande wangu nilemzidi umri akinambia hivyo huwa namjibu sijambo kisha namalizia shikamoo. Huwa lazima ajione mduwanzi na harudii tena siku nyingine kuniuliza ujambo?

Akirudia siku nyingine ujue nati zimelegea kichwani huyo.
 
'kibalazani - kibarazani', 'ujambo - hujambo', 'za saizi - za saa hizi'...!
Huwa nasimama kinyume na baadhi ya watu wanaoiharibu lugha adhimu ya Kiswahili..!!

Baadhi ya sehemu salamu ya 'Hujambo' hutumika kwa wenye rika sawa pia hivyo isikuchanganye sana, naamini alikuwa sawa kwa upande wake, hukupaswa kushtuka hivyo kama vile umeshuhudia muujiza..!!
Rika langu kiaje wakati nimeshasema huyo binti ni mtoto wa 2004.
 
'kibalazani - kibarazani', 'ujambo - hujambo', 'za saizi - za saa hizi'...!
Huwa nasimama kinyume na baadhi ya watu wanaoiharibu lugha adhimu ya Kiswahili..!!

Baadhi ya sehemu salamu ya 'Hujambo' hutumika kwa wenye rika sawa pia hivyo isikuchanganye sana, naamini alikuwa sawa kwa upande wake, hukupaswa kushtuka hivyo kama vile umeshuhudia muujiza..!!
Ni haujambo sio hujambo na ujambo... Tawachapeni kuharibu lugha adhimu..😎
 
Mkuu take it easy, kwa upande wangu nilemzidi umri akinambia hivyo huwa namjibu sijambo kisha namalizia shikamoo. Huwa lazima ajione mduwanzi na harudii tena siku nyingine kuniuliza ujambo?

Akirudia siku nyingine ujue nati zimelegea kichwani huyo.
 
Sio sawa mdogo kumsalimia hivyo mkubwa.

Hata kama kimaana hainashida, ila kwa desturi zetu inaleta ukakasi.
 
Back
Top Bottom