Salamu hizi ziwafikie Shekhe Kishki, Mazinge na wahadhiri wengine wa Kiislamu

Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
2,216
2,821
Salaam,

Kwanza nianze tu kwa kusema mimi ni Mwislamu na kama ilivyo kwenye dini kukumbushana, kutahadharishana, kunasihiana na kupendeleana mema ni sehemu ya maagizo na maamrisho tunayolazimika kuyafuata.

Mikoa ya kusini hususani vijiji vya Ruangwa (naongelea pahala nilipo na ushahidi napo zaidi) kumekuwa kuna mambo au taratibu za tofauti kabisa katika serikali na katika dini. Utofauti huo umetokana na elimu wanayomezeshwa watu kutoka kwa mashehe uchwara waliopo katika jamii.

Sasa kinachonihuzunisha zaidi watu hawa hawajawahi kupata kutembelewa hata na shekhe mmoja (nimedodosa dodosa nikagundua hilo)akaja kufanya mihadhara walau kupatiwa chakula cha nafsi. Kwa maana hiyo yote ninayoyaona wanaenda kinyume kumbe wapo sahihi kwakuwa wanafunzwa hivyo na mashekhe zao na hawajawahi kuambiwa (kuonywa) kwamba sivyo

Hali hii imenifanya nishangae sana maana hawa wahadhiri wamekuwa maarufu sana kwenye maeneo mengi mengineyo kwa kuurudisha umma kwenye mstari na sehemu zingine nimeshuhudia wakirudia kwenda kupiga kambi hata zaidi ya mara mbili je vipi kwa maeneo ya huku... kwamba;

a. Ni miongoni mwa maeneo ambayo hayakupata bahati kufikwa ila yapo kwenye mkakati (basi ndo mfanye mfike) au
b. Ni miongoni mwa maeneo yaliyoonekana yapo vizuri kidini hivyo hayakupewa kipaumbele kwahiyo hakukuwa na haraka ya kuja (basi ndo mjue kumeharibika sasa) au

c. Ni miongoni mwa maeneo yaliyosahaulika hayakuwa kwenye mkakati (basi ndo myafikirie kuyajia) au

d. Ni miongoni mwa maeneo ambayo mlifika zamani labda mkaishia baadhi ya sehemu za mjini tu mkahisi imetosha (basi sivyo! Mambo bado mabichi)

Mifano ni mingi sana lakini hapa nitatoa michache ambayo watu wa huku wanajishikamanisha nayo wakidhani ndio sheria za dini (au za serikali)

A. Kuachana (talaka) ni jambo la kawaida sana na wakiachana cha kwanza ni kugawana pasu kwa pasu. Mwanzo nilionaga kina Pembe wakiigiza nikajua muvi tu kumbe huku ndo mpango yaani unaoa halafu after mwezi mke anadai talaka na mali yako anashadadia mpaka ikatwe nusu apewe. Nimeshuhudia mtu akijenga nyumba nyingine ya pili huku akisema hii ni maandalizi siku tukigawana na mke wangu basi hatuna haja ya kuuza hii nyumba bali kila mtu apate nyumba yake (kwamaana ni salwala la kawaida talaka-pasupasu) na kweli kama mwezi mbele ikawa vilevile alivyosema

B. Uchumba, huku mtu akishatoa posa (wenyewe wanaita hela ya barua) basi huyo mke ni wake tayari na akija wazazi wa mwanamke wanampisha anajitawala bali hata kumchukua akalale naye kisha amrudishe kesho pia ruksa. Wengi sana wanaishi hata miaka 5-6 pamoja na huku hawajaoana na hata kuzaa wanazaa. Nimeshuhudia ndoa nyingi ambazo kabla yake wanandoa wamekuwa wakiishi pamoja kama mke mume (yaani hakuna tofauti na dizaini ile ya manaswara ya kubariki ndoa)

C. Swala Swaumu na Zaka, kuna kijiji 99% ni waislamu ila ni 20% tu wanafunga mwezi mtukufu huku 01% pekee (asilimia moja na wala siyo kumi) ndo wanaoswali. Ukiuliza wanakwambia sheria ya kufunga hauruhusiwi mtu wa kike ambaye hajaolewa kufunga wala mtu ambaye kula yake anaipata kwa njia za haramuharamu (mfano kuhongwa) naye haruhusiwi kufunga. Hawajaishia hapo tena wanaaminishana kwamba mwenye kula ya wasiwasi hatakiwi kufunga (tena bora ingekuwa wanamaanisha chakula hasa bali eti futari futari na matunda matunda muda wa magharibi)

Anayeishi na huyo mchumba wake ambaye bado hajamtolea mahari ndoa ipite basi wote wawili hawaswali wala hawafungi. Yaani wanaamini ni sahihi kuishi na kimada bora tu umeshatoa posa huku tena wanaamini kwamba kuishi na kimada ni dhambi (uzinifu) kwahiyo hafai hata kuswali wala kufunga swaumu kwa dhambi hiyo

D. Kuchinja, sisi tunahangaika kujielimisha juu ya kwamba kuelekea kibla au kuvua viatu kwenye kuchinja ni lazima au laa kumbe kuna jamii ambazo wao bado wapo kwenye kwamba aliyechinja apewe (nyama ya) shingo asepe nayo ( wenyewe wanaita uchinjo). Tena bora apewe tu kwa hiari ya mwenye kinachochinjwa basi... lahasha mtu anasema kabisa nipeni uchinjo wangu niondoke mie maana wa kwenda kuuliza juu ya roho ya kiumbe huyu ni mimi mchinjaji

E. Sherehe za idd
sijui pasaka na nyinginezo hazina nafasi huku japokuwa waislamu ni kama wote. Ikifika Dec vile wachaga wakirudi kwao kwajili ya Christmas basi kwa kipindi cha nyuma ndo ilikuwa ikifika misimu ya korosho na ufuta wamwera wanarudi kwao kwajili ya ngoma za asili (zipo sherehe nyingi mf kiangulo, manyago).

Sasa hivi baada ya serikali kuingilia kati hizo ngoma kwajili ya wanafunzi basi ndo mpira umehamishiwa kwenye mziki. Yaani kijijini hamlali kila siku watu wanakodi mziki tena mziki mnene kwajili ya sherehe hizo basi hapo kwenye mziki ni kufuru tupu usiku kucha.

Wanaweza kuanza saa 12 jioni mpaka 12 jioni tena ndo mziki unaisha watu wakitoka hapo sauti hawana nguo ni tope mwili mzima yaani hawatamaniki. Yaani serikali ilizuia ile mikusanyiko ya kuchangishana na kufanya sherehe siku za masomo ambapo process zake ni karibu wiki 2-3 sasa wao wameamua kila mtu anafanya mwenyewe kwake lakini kitu ni kilekile.

F. Ulevi,
watu wengi wanatumia bangi na/au pombe za kienyeji na ni kitu cha kawaida tu. Ubaya huku sioni viongozi wa dini wala wa serikali za vijiji wakikemea jambo baya lolote.

G. Matusi, huku matusi ni kionjo cha kawaida katika maongezi... kama ni mgeni mwanzo utapata tabu sana. Nidhamu katika utendaji hakuna unakuta kwenye mikusanyiko kiongozi anaongea (ukiacha viongozi wanaoambatana na polisi) huku watu wanapiga zao stori tena kwa nguvu tu. Mfano makabirini harusini mabaraza ya dini wachache sana mnakuwa concentrate na jambo husika lakini wengine shekhe anaongea wao ndo kwanza wanapiga kelele tu na shekhe hakemei

H. Kuna utaratibu wa kunyweshana sijui ni kitu gani hata lakini wanakunywaga watu wale wa qadiria shamsia na shazilia.
Basi huku kama hukunywa hiyo unakuwa hujajinasibisha katika kundi fulani wenyewe wanadai hata ukifa mashekhe watasuasua kwenye kukusitiri

I. Mtu akizini au akifumwa na mwanafunzi au mke wa mtu au makosa mengine yoyote basi ni kitega uchumi kwani anashikwa faini kubwa sana na kesi inakuwa imekwisha.
Hilo yawezekana la kawaida kwa baadhi ya makosa lakini siyo kwa mtoto wa shule na mke. huku mtu yupo radhi kuusuka mchongo kabisa na mwanawe au mkewe ili wakupige hela yaani anairuhusu zinaa ili apate kipato na hili limeenea sana.

Nimeongelea upande wa dini tu kama nilivyotangulia kusema mwanzo mimi ni Mwislamu na wengi katika wahusika ni waislamu hivyo naongelea (kuwa si sahihi) kwa kiislamu. Upande wa kiserikali napo kuna mengi mfano ni ule uzi nilileta humu kwamba watu wanaunguza sana misitu bila hatua zozote kuchukuliwa.

Hayo na mengine mengi yanakwenda kinyume mimi nimejitahidi kwa kiwango changu kuyasemea ila sina ushawishi wala elimu ya kufanikiwa kivile kama mashekhe waliobobea kwahiyo yeyote mwenye uwezo na awajibike.
 
Sasa hivi mashehe na maostadhi wa mitaani hamna kitu wao wanajua tu maana za maneno ya kiarabu bila ya kuyafanyia kazi na pia vilevile wanafanya dini kwa mazoea kabisa hawana uchungu na hamu ya kuendeleza elimu yan elimu aliyoipata kwa she he wa kijiji inamtosha eti na yy kuanzisha madrasa sasa unafkir inakuaje but all in all tunakaz kubwa ya kufanya ili kuondoa balaa hili
 
Salaam Alaykum
Mkuu naomba direction eneo la tatizo naomba unijuze tatizo unaloliona japo umeandika lkn Sorry sijaelewa kiundani..
Swali;Je eneo hilo kuna nyumba za wageni?
Usafiri ukoje?
Samahani kama kuna maswali nimekosea..
 
Dini yako iliwakuta hao watu wana mila na taratibu zao,wataamua wanayoona yanafaa kuachwa na yanayofaa kuendelea nayo.
 
I see. Umeandika vizuri sana ndugu na umeeleweka. Ubarikiwe kwa kuchukua initiative. Natumaini masheikh watapita na kusoma au kutumiwa huu ujumbe. Na hali hii sio huko tu, bali na sehemu nyingine nyingi tu. Allah ndie mjuzi wa yote
 
Inabidi Elimu dunia iperekwe sana huko,kuanzia Ruangwa,Nachingwea,Kibutuka,Mpaka Liwale,Nakapanya,Nanyumbu,Michiga,Masuguru,Masasi Bado wapo nyuma sana.
Pale Ndada Richa ya kuwepo misheni,lakini Bado kazi kubwa inahitajika,
Jamii inabidi iperekewe Elimu Kwanza,ingekuwa Bora shule zote ziwe boarding,maana unakuta mzazi hajasoma,anajua unyago tu,mtoto itakuwaje?
 
hao watu washamsiya wanakunywa nini?? huku mbona kunayo hayo matabaka, zaharau, tamta, shamsil maa'rif, bakhresa, maa'wal sjawah kusikia wananywesha hayo mambo na hata ukiwa zahrau utazikwa na matawi yote watakaojaaliwa kukuzika
 
hao watu washamsiya wanakunywa nini?? huku mbona kunayo hayo matabaka, zaharau, tamta, shamsil maa'rif, bakhresa, maa'wal sjawah kusikia wananywesha hayo mambo na hata ukiwa zahrau utazikwa na matawi yote watakaojaaliwa kukuzika
Hayo matabaka.mbona Mimi sijawai yasikia.kabisa...NIYAPO.KATIKA UISLAMU.au Ni vitu vyakutungwa na Watu.

Mpaka bakhresa..
 
dhima ya kuamrisha mema na kukataza mabaya ni letu sote, na wala si la kikundi fulani miongoni mwetu. kila mmoja wetu afanye ambalo liko ndani ya uwezo wake mahali popote alipo.mwenyezi mungu atufanyie wepesi
wallahu aalam!!
 
hao watu washamsiya wanakunywa nini?? huku mbona kunayo hayo matabaka, zaharau, tamta, shamsil maa'rif, bakhresa, maa'wal sjawah kusikia wananywesha hayo mambo na hata ukiwa zahrau utazikwa na matawi yote watakaojaaliwa kukuzika
Hii comment yako inasound Kama wewe Ni Mtanga au mwenyeji wa Tanga!...
 
Hayo matabaka.mbona Mimi sijawai yasikia.kabisa...NIYAPO.KATIKA UISLAMU.au Ni vitu vyakutungwa na Watu.

Mpaka bakhresa..
Hayo matabaka ukitaka kuyafahamu vizuri tembelea Tanga tu mkuu utayaona na kuyajuavizuri....wacha bakhresa tu Kuna mpaka BAKWATA!
 
hao watu washamsiya wanakunywa nini?? huku mbona kunayo hayo matabaka, zaharau, tamta, shamsil maa'rif, bakhresa, maa'wal sjawah kusikia wananywesha hayo mambo na hata ukiwa zahrau utazikwa na matawi yote watakaojaaliwa kukuzika

Ahlul sunnah waljamaa hawapo huko?
 
maeneo ya Gatundu,msambweni au sio. Kwan kujua hayo madarris ndio uwe Tanga? kama aliwahi kusoma huko
Ndio maana nikasema either ametokea Tanga au mwenyeji wa huko..kwamaana huo uwenyeji wake ameupata either kwakusomea huko au ktk harakati zingine za maisha...
Otherwise bila kufika huko au kua mtu wahuko hizo madrassa huwezi kuzijua Wala kuzisikia popote pale nchini...kuthibitisha hilo ndio maana Kuna mmoja aliuliza hata BAKHRESA PIA!
 
Sasa unamlalamikia nani? Hivi wewe imekaa ukaangalia ukaona hao eti ndio mashehe?
Pambana na changamoto kama umeona hayo waelimishe,fungua madrasa wasomeshe watu wawe na elimu na sio kukimbilia mitandaoni na kuja kujiliza Liza kama LOFA. Isitegemee kwa muhibiri anayezungumza siku moja na kuondoka eti kuwa ataweza kuirekebisha jamii. Somesheni vijana na nyie wenyewe someni.
 
Sasa unamlalamikia nani? Hivi wewe imekaa ukaangalia ukaona hao eti ndio mashehe?
Pambana na changamoto kama umeona hayo waelimishe,fungua madrasa wasomeshe watu wawe na elimu na sio kukimbilia mitandaoni na kuja kujiliza Liza kama LOFA. Isitegemee kwa muhibiri anayezungumza siku moja na kuondoka eti kuwa ataweza kuirekebisha jamii. Somesheni vijana na nyie wenyewe someni.
Inawezekana kuna walionielewa na wasionielewa pia yawezekana kuna nitakaowaelewa na ambao sitawaelewa

Kwahiyo hata wewe upo sahihi tu, Mola anajua zaidi
 
Back
Top Bottom