SoC02 Salama ya mabinti shule za sekondari katika ‘punjabi’

Stories of Change - 2022 Competition
Aug 27, 2022
2
2
Kuna changamoto kadhaa katika mavazi ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari. Changamoto hizi huathiri matendo ya ufundishaji na ujifunzaji hali kadhalika mielekeo ya wanafunzi kwa namna fulani. Katika kujadili hili, nitajikita katika mavazi ya wanafunzi wa kike wa sekondari kwa sababu tatu. Kwanza ni uwepo wa ukomo wa maneno katika shindano hili; pili, ni ukubwa wa changamoto za mavazi ya wasichana zikilinganishwa na zile za mavazi ya wavulana; na tatu ni sababu ya mpevuko wa maumbile ya wanafunzi wa sekondari yakilinganishwa na yale ya wanafunzi wa shule za msingi.

Vazi rasmi kwa wanafunzi wa kike katika shule za sekondari ni sketi na blauzi. Katika muktadha wa kiimani, baadhi yao huruhusiwa kuvaa suruali, blauzi na hijabu. Changamoto za vazi la sketi na blauzi huenda hazijasemwa kwa hoja zenye mashiko na wanafunzi wenyewe au walezi wao kwa kuwa tu ni desturi kwa wanawake kuvaa sketi na blauzi. Aghalabu linaposemwa, basi huwa ni kwa kuutazama ufupi na ushawishi wake katika ngono; jambo linalokinzana na miiko ya kidini. Kwa mtazamo wa jicho la tatu, zipo sababu kadhaa zinazoliondolea ubora vazi la sketi na blauzi katika mazingira ya shule za sekondari.

Mosi: Huwaondolea wanafunzi wakike sitara. Kuna matendo yasiyoepukika katika mazingira ya shule kama vile kuinama mfano wakati wa kudeki, kuchuchumaa, kukaa na kuinuka, kupanda au kuruka vizuizi na vidato kama ngazi zenye vimo virefu kiasi, kuanguka kwa kuteleza na kukimbia mfano kwenye wito wa kengele au katika adhabu. Kwa kufanya matendo haya, wasichana hujikuta pasipo kupenda kwao au kujua wakiacha sehemu za miili na mavazi yao ya ndani bila sitara mbele ya wavulana, walimu na watumishi wengine. Hili huwapunguzia heshima yao.

httpswww.rfi.frsweac20120723-wanafunzi-kuvaa-nguo-fupi-ni-tatizo.jpg

chanzo:httpswww.rfi.frsweac20120723-wanafunzi-kuvaa-nguo-fupi-ni-tatizo

httpsweb.facebook.comafmradiotzphotosleo-katika-mahanjam-mix-na-ednawanafunzi-kuvaa-sketi-fupi...jpg

chanzo:https://web.facebook.comafmradiotzphotosleo-katika-mahanjam-mix-na-ednawanafunzi-kuvaa-sketi-fupi-mashuleni-je-unafikiri667086126789208

Pili: Huchochea mihemko ya kimapenzi. Chanzo cha hili ni kuachwa wazi kwa sehemu nyeti za miili. Mathalani, kazi kama vile za kudeki madarasa, veranda za shule na ofisi za walimu wanafunzi wa kike huhusika zaidi. Wanapoinama kudeki, hulazimisha blauzi au sweta hushuka kutoka kiunoni kuja vifuani na kuacha sehemu ya mgongo kuanzia kiunoni wazi. Hali kadhalika, sehemu ya nyuma ya sketi huvutikia mbele nakuziacha baadhi ya nguo za ndani na sehemu za miili yao zilizopaswa kusitiriwa wazi yaani robo utupu mbele ya upeo wa walimu au wanafunzi wavulana.

Ikumbukwe pia, wanafunzi hawa wa kike katika sekondari za Tanzania, wengi ni watoto kutoka familia za kipato cha kati na cha chini. Ni familia chache sana kati ya hizo humudu kuwanunulia mabinti hawa sare mpya yaani sketi na blauzi kuendana na ukuaji wa maumbile yao. Wengi hujikuta wakivaa sketi zilezile walizoanza nazo shule kwa miaka kadhaa ya masomo ambazo hugeuka kuwa fupi kulinganisha naukuaji wa maumbile yao.

Kuachwa wazi kwa maumbile ya wasichana ambayo kwa tamaduni zetu za Kitanzania hupaswa kusitiriwa hugeuka kishawishi na kichocheo cha mihemko ya kimpapenzi kwa baadhi ya walimu wa kiume na wanafunzi wavulana shuleni. Hatima ya hili ni kushuka kwa nidhamu, kuendelea kwa tatizo la mimba shuleni na hatimaye mdondoko wa wanafunzi wa kike.

httpswww.hrw.orgsitesdefaultfilesreport_pdftanzania0217kish_insert_lowres_spreads_2.pdf.jpg

httpswww.hrw.orgsitesdefaultfilesreport_pdftanzania0217kish_insert_lowres_spreads_2.pdf


Tatu: Huumiza miili nakuondoa mkazo wakimasomo: Yapo maeneo yakijiogafia ambayo kwa kipindi kirefu cha mwaka yana baridi. Mfano maeneo ya nyanda za juu kama vile Iringa, Kilimanjaro, Njombe, Arusha na Mbeya. Uvaaji wa sketi hufuatwa kwa kuwa ni sheria tu. Hata mapungufu yake ambayo ni bayana hayasemewi kwa kuwa ni desturi tu kwa wasichana kuvaa sketi na wavulana kuvaa suruali. Ila kiuhalisia muundo wa sketi huongeza athari za baridi kwa mabinti. Sketi hazifuniki sehemu yote ya miguu na uwazi wake mpana kwa chini huwa nikipitisho kikubwa cha hewa baridi kuufikia mwili. Hivyo kama ilivyo kwa visababishi vingine mfano njaa, joto kali au kelele, athari ya baridi katika sehemu ya miguu tu nayo huwapunguzia mabinti mkazo katika kujifunza.

Je, sketi ndefu zaweza kuwa suluhu kwa haya yote?

Sketi ndefu ni zile zinazotambuliwa urefu wake kutoka katika unyayo (Mfano yenye urefu unaoacha inchi sita kutoka katika unyayo). Katika mazingira fulani ambayo ni nadra mno laweza kuwa sahihi (Bweni na pasipohususha kazi kwa wanafunzi)

sketi ndefu.jpg

Chanzo cha picha:

Lakini kwa wasichana wanaotembea umbali mrefu kufika shuleni, wanaopita katika barabara za vumbi au umande wakati wa asubuhi siketi hizi huweza kuongeza changamoto ya unadhifu kwa maana ya kuchafuka kirahisi kwa vumbi na kulowa kwa wepesi kwa umande. Kwa upande mwingine sketi ikiwa ndefu sana yaweza kuwa kikwazo katika matendo ya kutembea na kukimbia. Halikadhalika, mwanafunzi anapoinama kufagia au kudeki vazi huweza kuburuza chini kwa mbele.

africaid.org.jpg

Sketi ndefu huweza kuburuza chini. Chanzo cha picha: africaid.org

PENDEKEZO: Mamlaka za elimu katika nchi yetu zilitazame na kulipitisha vazi litambulikanalo kwa jina la PUNJABI. Vazi hili ni mwigo wa vali la Kihindi. Muundo wake hujumuisha blauzi na suruali. Blauzi huwa ndefu isiyochomekwa katika suruali na inayofika usawa wa nusu ya mapaja. Pia hupasuliwa kidogo pembeni, kushoto na kulia ili kurahisisha ukaaji. Suruali huwa pana eneo la baada ya kiuno na inayobana kiasi kwa chini-mwishoni kabla ya vifundo vya miguu.

Ubora wa vazi la Punjabi ni kama ifuatavyo:

Mosi: Vazi hili husitiri maumbile ya wasichana wanapofanya matendo mbalimbali kwa mfano kuinama wanapodeki, wanapokaa na kuinuka au wanapopanda vidato vyenye kimo kirefu kiasi.

alhikmatanzania.wordpress.jpg

Punjabi limejaa sitara Chanzo cha picha: alhikmatanzania.wordpress

Pili: Vazi la punjabi huwapa wasichana uhuru katika matendo ya kutembea, kuinama, kukimbia na kuruka. Tatu: Ni vazi bora zaidi katika mazingira ya upepo, baridi na joto, ya vumbi na umande likilinganishwa na sketi zitumikazo kwa sasa.

Tatu: Katika mazingira ya baridi, Huweza kumpa mwanafunzi fursa ya kuvalia ndani nguo ndefu za kuongeza joto zenye muundo wa suruali za kubana bila kuleta athari katika muonekano wa sare za shule.

Nne: Ni vazi ambalo huweka ugumu wa kiwango fulani kwa mwanafunzi kuendelea kulivaa pale ambapo maumbile yake yameongezeka ukubwa na vazi kuwa dogo.

Ikiwa mantiki ya hoja zilizomo katika andiko hili zitazingatiwa na utekelezaji wake ukawekewa umakini hasa katika vipimo sahihi basi kuna changamoto katika malezi zitapungua kwa walimu wa nidhamu shuleni na kwa wazazi/ walezi na kuchangia katika ufaulu wa mwanafunzi.​
 

Attachments

  • sua.ac.tz.jpg
    sua.ac.tz.jpg
    10.6 KB · Views: 7
Back
Top Bottom