Salam za mwaka mpya: Je Maaskofu watajibiwa?

Salam za mwaka mpya: Je Maaskofu watajibiwa?

Nilipitia comment kama 3 sehemu tofauti nikaona comments zako nikasema cocochanel amechange dp na amekuwa na akili apost pumba siku hizi dooh leo mwezi sijui umerudi..

Umerudi kwenye akili zile zile bora sikukusifia kwanza nilitaka kujiaminisha maana sikutegemea upone mapema mno

Mmmmmmh!!!
 
Kwanini haukusubiri unayoongelea siku hiyo ifike kwanza.
Yaani nyie upinzani mnatia kukaa kimya hadi viongozi wenu.. na nyie mkijipigisha madebe kiunyongeee kisa JPM kaongelewa makanisani.

Mnatia huruma sana.. mwaka 2017 mmejimaliza kabisa. Acheni viongozi wenu washibe.. ila si mnaliaga au? Kuna kipindi natamani niwasaidie kuanzisha chama kipya niwape maujanja.. yaani nyie wa humu ili basi nanyi muonje pesa za ruzuku ambazo mnastahili mgao.. mmejitahidi sana ile eeeeh aiseeee.. sasa leteni hoja za kusaidia wananchi sio haya..

Ila serikalini wanalao.. na Polepole nae na chama chake nae anayake..
Tabu ingine ni nyie mnaokuza majambo na kuyageuza.. hadi kama wana makosa mnatufanya tuone wapo sawa wanachi sisi.. bikozi mnaboaaaa upinzani nyie. Mngekuwa smati mngeacha wananchi wajiulize wao makwao na kuona kama kuna makosa.. sasa hawa wameongea matatu tofauti nyie hao mnadandia hamjipimi.. eeeeeeeh JPM ananifanya niandike haya.. 2018 na siasa mie hukooooo humu ha ha haa

Ya kujibu ya mtandaoni sioni sababu ya nyie kushangaaa.. maisha ndivyo yamekuwa miaka hii.. au unataka wawasubiri upinzani muwape habari hizo mkifika bungeni.. ondia ushamba baai

Haya najiona hili ni gazeti la kufungia 2017 humu...
faizafoxy was better than this.
 
faizafoxy was better than this.

Embu jifananishe wewe na yeye.. mkome kudakia nayoandika. Nimekuja mwenyewe humu JF kuburudika kivyangu.. kama unaona hauna nondo unavizia kuzipata kwa watu basi subiria wengine.. mimi simwagi zangu ovyo ovyo haswa kwenu waviziaji mlio hewa kwa sana up huko.
 
MRISHO GAMBO NA SIZONJE
wote [HASHTAG]#wakatubu[/HASHTAG]

[HASHTAG]#ATUBU[/HASHTAG]
 
Imekuwa ni utaratibu mpya zama hizi, serikali na idara zake kusoma nini kimetokea mitandaoni ama kuna mjadala gani na wao kuja na majibu kwa mtindo huohuo ama kuandaliwa hafla fulani na huko majibu ya kufungia mjadala hutolewa.

Kuna shida mahali kwenye organs za serikali, hawana team work, hawana mawasiliano, hawaachiani majukumu nani aseme nini... Kikitokea kitu wengine bila hata kuulizwa tayari wana post mitandaoni kujibu, hapo utafuata msururu wa majibu na yote yakiwa ni ya wasemaji ama viongozi wanaoiwakilisha serikali... Na mpaka leo hawaoni kuwa hili ni tatizo... Wajitahidi mwakani kuwasiliana wao kwa wao... La kichama lijibiwe na msemaji wa chama la kiserikali lijibiwe na wanaohusika... Na wajibu hoja kwa hoja na sio mipasho, vitisho na kejeli....

Askofu Zakaria Kakobe kawa mshindi wa drama za mwaka mzima, kafunika bovu... Matamko yametoka kila kona ya viongozi wa nchi... Bahati mbaya sana hakuna aliyeweza kujibu hoja zake hata mmoja... Pengine atajibiwa wakati wa salam za mwaka mpya
Nilikuwa na hamu ya kujua ni drama gani itatufungia mwaka... Nikajaribu kufanya makisio, kamwe sikujua litakuja hili... Japo linaweza kutafutwa tukio la kufunika hili.... Tusubiri bado masaa zaidi ya 24 kubadili mwaka.

Kitu kingine cha kusikitisha ni kwamba hata hao viongozi na wasemaji wa serikali katika kujibu mapigo wameshindwa kabisa kujitenga kwa hoja, mwisho wa siku nao wamezua malumbano tu kama malumbano mengine mitandaoni nao wamekuwa sehemu ya kebehi ubabe na vitisho... Hakuna hata mmoja alikuja na hoja ama majibu makini... Labda tusubiri salam za mwaka mpya.

Kuna hili andishi.. Ninaloweza kuliita andishi bora litakaloishi muda mrefu... Andiko hili ni fikirishi na limebeba ujumbe mzito sana lakini shuhudia majibu yaliyotolewa, yalikuwa majibu ya jumla mno na yalikuwa majibu yenye kukimbia ukweli... Andiko lenyewe hili hapaView attachment 663216

Tunapoelekea kuumaliza mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka 2018, naamini kwa dhati ya moyo kuna maandiko mengine yatatolewa LAKIJI je yatavumiliwa? Yatajibiwa kwa weledi? Ama yatafanyiwa kazi kimya kimya? Je baada ya vyama makini vya upinzani kuminywa sana hii ni aina mpya ya siasa?

Nasubiri salam za mwaka mpya!!!!!
Alipokuwa kwenye kampeni Kagera alimwambia Kilaini wajiangalie kwani akibana mafisadi lazima sadaka itapungua, sijuhi kama walimwelewa ama hawakumelewa. Sasa hivi sadaka zimepungua wanaanza kuja na vijimisemo, waache habari na waanze kupambana na hari zao.
 
Isifikiriwe kuwa nataka kuleta hoja ya ubaguzi lakini nimeshangazwa mno na ukimya wa maaskofu wengi wakatoliki ambao huwa hawarembi na kupenda kuongea ukweli ulio uchi... Kwenye nyeupe wataita nyeupe na kwenye nyeusi wataita nyeusi... Ila mwaka huu naona kuna kigugumizi na sijaona waraka wowote toka kwao... Hii sio kawaida yao[emoji15] [emoji15] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144]
Kisu kimekata mfupa
 
Alipokuwa kwenye kampeni Kagera alimwambia Kilaini wajiangalie kwani akibana mafisadi lazima sadaka itapungua, sijuhi kama walimwelewa ama hawakumelewa. Sasa hivi sadaka zimepungua wanaanza kuja na vijimisemo, waache habari na waanze kupambana na hari zao.
Sadaka ni kitu kidogo mno kuna makubwa zaidi ya sadaka
 
Huu ujumbe hauchoshi kusoma
IMG_20171230_023508_820.jpg
 
Back
Top Bottom