Salam za mwaka mpya: Je Maaskofu watajibiwa?

Salam za mwaka mpya: Je Maaskofu watajibiwa?

Imekuwa ni utaratibu mpya zama hizi, serikali na idara zake kusoma nini kimetokea mitandaoni ama kuna mjadala gani na wao kuja na majibu kwa mtindo huohuo ama kuandaliwa hafla fulani na huko majibu ya kufungia mjadala hutolewa.

Kuna shida mahali kwenye organs za serikali, hawana team work, hawana mawasiliano, hawaachiani majukumu nani aseme nini... Kikitokea kitu wengine bila hata kuulizwa tayari wana post mitandaoni kujibu, hapo utafuata msururu wa majibu na yote yakiwa ni ya wasemaji ama viongozi wanaoiwakilisha serikali... Na mpaka leo hawaoni kuwa hili ni tatizo... Wajitahidi mwakani kuwasiliana wao kwa wao... La kichama lijibiwe na msemaji wa chama la kiserikali lijibiwe na wanaohusika... Na wajibu hoja kwa hoja na sio mipasho, vitisho na kejeli....

Askofu Zakaria Kakobe kawa mshindi wa drama za mwaka mzima, kafunika bovu... Matamko yametoka kila kona ya viongozi wa nchi... Bahati mbaya sana hakuna aliyeweza kujibu hoja zake hata mmoja... Pengine atajibiwa wakati wa salam za mwaka mpya
Nilikuwa na hamu ya kujua ni drama gani itatufungia mwaka... Nikajaribu kufanya makisio, kamwe sikujua litakuja hili... Japo linaweza kutafutwa tukio la kufunika hili.... Tusubiri bado masaa zaidi ya 24 kubadili mwaka.

Kitu kingine cha kusikitisha ni kwamba hata hao viongozi na wasemaji wa serikali katika kujibu mapigo wameshindwa kabisa kujitenga kwa hoja, mwisho wa siku nao wamezua malumbano tu kama malumbano mengine mitandaoni nao wamekuwa sehemu ya kebehi ubabe na vitisho... Hakuna hata mmoja alikuja na hoja ama majibu makini... Labda tusubiri salam za mwaka mpya.
Pongezi kwake mchungaji wa kondoo wa mungu.Baba wa mbinguni azidi kukupa kina aina ya mawazo mema ya kuwapa binadamu somo.Wapo wagumu wa kuelewa lakini mwisho wa siku watakuelewa tu.Ubarikiwe sana .
Kuna hili andishi.. Ninaloweza kuliita andishi bora litakaloishi muda mrefu... Andiko hili ni fikirishi na limebeba ujumbe mzito sana lakini shuhudia majibu yaliyotolewa, yalikuwa majibu ya jumla mno na yalikuwa majibu yenye kukimbia ukweli... Andiko lenyewe hili hapaView attachment 663216

Tunapoelekea kuumaliza mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka 2018, naamini kwa dhati ya moyo kuna maandiko mengine yatatolewa LAKIJI je yatavumiliwa? Yatajibiwa kwa weledi? Ama yatafanyiwa kazi kimya kimya? Je baada ya vyama makini vya upinzani kuminywa sana hii ni aina mpya ya siasa?

Nasubiri salam za mwaka mpya!!!!!
 
Kwanini haukusubiri unayoongelea siku hiyo ifike kwanza.
Yaani nyie upinzani mnatia kukaa kimya hadi viongozi wenu.. na nyie mkijipigisha madebe kiunyongeee kisa JPM kaongelewa makanisani.

Mnatia huruma sana.. mwaka 2017 mmejimaliza kabisa. Acheni viongozi wenu washibe.. ila si mnaliaga au? Kuna kipindi natamani niwasaidie kuanzisha chama kipya niwape maujanja.. yaani nyie wa humu ili basi nanyi muonje pesa za ruzuku ambazo mnastahili mgao.. mmejitahidi sana ile eeeeh aiseeee.. sasa leteni hoja za kusaidia wananchi sio haya..

Ila serikalini wanalao.. na Polepole nae na chama chake nae anayake..
Tabu ingine ni nyie mnaokuza majambo na kuyageuza.. hadi kama wana makosa mnatufanya tuone wapo sawa wanachi sisi.. bikozi mnaboaaaa upinzani nyie. Mngekuwa smati mngeacha wananchi wajiulize wao makwao na kuona kama kuna makosa.. sasa hawa wameongea matatu tofauti nyie hao mnadandia hamjipimi.. eeeeeeeh JPM ananifanya niandike haya.. 2018 na siasa mie hukooooo humu ha ha haa

Ya kujibu ya mtandaoni sioni sababu ya nyie kushangaaa.. maisha ndivyo yamekuwa miaka hii.. au unataka wawasubiri upinzani muwape habari hizo mkifika bungeni.. ondia ushamba baai

Haya najiona hili ni gazeti la kufungia 2017 humu...
Uwezo mdogo wa kufikiri ndo huandika andiko kama hili
 
Eeeeeeeeh
Subiri labda Coco atabadilika mwakani.. na sio mbali ujue ni kesho kutwa tu IJN.

Uliponiita wapi ni tagi tena basi.. au ndio uzi huu eeeeh
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] ukinikataa nakuroga
 
Huu uzi siyo saizi yangu!
ila niweke tu maki kwenye hii:
ed651912ffa59ba0025495908b636efb.jpg
 
Hizo Nondo za Askofu Benson Bagonza number 4,5,6

Ni hatar sanah ukizipambanua vizur na namba 1 kamaliza
 
Niambie huyu nini haswa kilimuwasha washa hadi kumwagika na hayo?

Je mmemjadili weeee na kuna faida ipi imepatikana kwake na pia kwenu nyie upinzani? Nasubiria majibu kwa hamu

Heri ya mwaka mpya kwako pia..

Nashukuru kujua u lavu me.. tabu mimi hilo neno huwa gumu sana kulitoa kutoka mdomoni au akilini mwangu.. eeeeeeh
Nilipitia comment kama 3 sehemu tofauti nikaona comments zako nikasema cocochanel amechange dp na amekuwa na akili apost pumba siku hizi dooh leo mwezi sijui umerudi..

Umerudi kwenye akili zile zile bora sikukusifia kwanza nilitaka kujiaminisha maana sikutegemea upone mapema mno
 
Eeeeeeh

Bujibuji.. sina chama ujue.. wala sipo serikalini.. ushabiki wa siasa humu na kujadili kiki nawaachia nyie.. mimi mwakani nitaburudika kivingine humu na breki juu

Siasa zinaboa.. bora uzi zisizo na siasaaaa.. mfano za mshana jr
Na wewe ushaguswa nin!? [emoji16][emoji16][emoji16]
 
ukisoma comment zilizonyingi za watu waliopo ktk Uzi huu
utapat majibu ya haraka kuwa sizonje nimiongoni mwa adui wakwanza wa watanzania

sasa najiuliza ziletakwimu zao kuwa anaungwa mkono dhidi ya utendaji wake na asilimia kubwa ya wa tz huwa wanaitoa wapi...au
wachangiaji wengi wahumu ni raia wa ghana nini. !!?
 
Mrisho Gambo kasema atalichunguza kanisa la Kakobe kama linaongozwa Na roho wa Mungu au shetani. Sijui uchunguzi huo utatumia kipimo gani?
Kwaua nammfahamu shetani na Mungu ndio muda muafaka wakutujulisha kuwa Mungu na rushwa wapina wapi na bado mkulu anawabeba.
Ila yana mwisho, kuna mambo nikikumbuka huwa najiapiza moyoni mwangu ya kua niheri kuwa masikini kuliko kuwa tajiri ukiwa mwanachama wa ccm.
 
Back
Top Bottom