Salam za mwaka mpya: Je Maaskofu watajibiwa?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
375,662
Reaction score
870,346
Imekuwa ni utaratibu mpya zama hizi, serikali na idara zake kusoma nini kimetokea mitandaoni ama kuna mjadala gani na wao kuja na majibu kwa mtindo huohuo ama kuandaliwa hafla fulani na huko majibu ya kufungia mjadala hutolewa.

Kuna shida mahali kwenye organs za serikali, hawana team work, hawana mawasiliano, hawaachiani majukumu nani aseme nini... Kikitokea kitu wengine bila hata kuulizwa tayari wana post mitandaoni kujibu, hapo utafuata msururu wa majibu na yote yakiwa ni ya wasemaji ama viongozi wanaoiwakilisha serikali... Na mpaka leo hawaoni kuwa hili ni tatizo... Wajitahidi mwakani kuwasiliana wao kwa wao... La kichama lijibiwe na msemaji wa chama la kiserikali lijibiwe na wanaohusika... Na wajibu hoja kwa hoja na sio mipasho, vitisho na kejeli....

Askofu Zakaria Kakobe kawa mshindi wa drama za mwaka mzima, kafunika bovu... Matamko yametoka kila kona ya viongozi wa nchi... Bahati mbaya sana hakuna aliyeweza kujibu hoja zake hata mmoja... Pengine atajibiwa wakati wa salam za mwaka mpya
Nilikuwa na hamu ya kujua ni drama gani itatufungia mwaka... Nikajaribu kufanya makisio, kamwe sikujua litakuja hili... Japo linaweza kutafutwa tukio la kufunika hili.... Tusubiri bado masaa zaidi ya 24 kubadili mwaka.

Kitu kingine cha kusikitisha ni kwamba hata hao viongozi na wasemaji wa serikali katika kujibu mapigo wameshindwa kabisa kujitenga kwa hoja, mwisho wa siku nao wamezua malumbano tu kama malumbano mengine mitandaoni nao wamekuwa sehemu ya kebehi ubabe na vitisho... Hakuna hata mmoja alikuja na hoja ama majibu makini... Labda tusubiri salam za mwaka mpya.

Kuna hili andishi.. Ninaloweza kuliita andishi bora litakaloishi muda mrefu... Andiko hili ni fikirishi na limebeba ujumbe mzito sana lakini shuhudia majibu yaliyotolewa, yalikuwa majibu ya jumla mno na yalikuwa majibu yenye kukimbia ukweli... Andiko lenyewe hili hapa
IMG_20171230_023508_820.jpg

Tunapoelekea kuumaliza mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka 2018, naamini kwa dhati ya moyo kuna maandiko mengine yatatolewa LAKIJI je yatavumiliwa? Yatajibiwa kwa weledi? Ama yatafanyiwa kazi kimya kimya? Je baada ya vyama makini vya upinzani kuminywa sana hii ni aina mpya ya siasa?

Nasubiri salam za mwaka mpya!!!!!
 
Isije wakajibiwa kwa kejeli na matusi. Kumbuka [HASHTAG]#ngwinimkazavyuma[/HASHTAG] hajaribiwi wastaafu aliwatusi kwamba wanawashwa washwa. Hekima na busara kwa huyu jamaa zilimpitia mbali. Tusubiri tuone kama kutakuwa na jipya au muendelezo wa yale ambayo tumeshayazoea.
 
Si wewe tu bali Watanzania kwa mamilioni ambao wamechoshwa na haya maovu nchini na bila shaka Watanzania wengi tungependa kuona hawa Viongozi wa dini hawalegezi kamba mpaka kieleweke.
Isifikiriwe kuwa nataka kuleta hoja ya ubaguzi lakini nimeshangazwa mno na ukimya wa maaskofu wengi wakatoliki ambao huwa hawarembi na kupenda kuongea ukweli ulio uchi... Kwenye nyeupe wataita nyeupe na kwenye nyeusi wataita nyeusi... Ila mwaka huu naona kuna kigugumizi na sijaona waraka wowote toka kwao... Hii sio kawaida yao[emoji15] [emoji15] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144]
 
Mkuu Mshana nilichojifunza Mimi kuelekea kumaliza mwaka 2017, juu ya salamu za askofu Kakobe na majibu ya wapambe na watumishi wa chama tawala na serikali; kuna mtu ni mwepesi mno ndo maana kumbe vitisho, kamatakamata ya wakosoaji haviishi!
 
Wengi tunawashangaa hawa Mkuu lakini hawajachelewa kusimamia haki na uhuru wa Watanzania. Pia ukiondoa Sheikh Ponda Viongozi wa dini ya kiislamu nao wamekuwa kimya mno na wengine hata wamethubutu kuendelea kummwagia sifa huyo mtenda maovu.

Tumechoshwa na hatutaki kuishi nchi inayoongozwa kama ilivyokuwa ikiongozwa na Afrika ya Kusini na wale Makaburu na Wabaguzi wa rangi.

Isifikiriwe kuwa nataka kuleta hoja ya ubaguzi lakini nimeshangazwa mno na ukimya wa maaskofu wengi wakatoliki ambao huwa hawarembi na kupenda kuongea ukweli ulio uchi... Kwenye nyeupe wataita nyeupe na kwenye nyeusi wataita nyeusi... Ila mwaka huu naona kuna kigugumizi na sijaona waraka wowote toka kwao... Hii sio kawaida yao[emoji15] [emoji15] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144]
 
Kwanini haukusubiri unayoongelea siku hiyo ifike kwanza.
Yaani nyie upinzani mnatia kukaa kimya hadi viongozi wenu.. na nyie mkijipigisha madebe kiunyongeee kisa JPM kaongelewa makanisani.

Mnatia huruma sana.. mwaka 2017 mmejimaliza kabisa. Acheni viongozi wenu washibe.. ila si mnaliaga au? Kuna kipindi natamani niwasaidie kuanzisha chama kipya niwape maujanja.. yaani nyie wa humu ili basi nanyi muonje pesa za ruzuku ambazo mnastahili mgao.. mmejitahidi sana ile eeeeh aiseeee.. sasa leteni hoja za kusaidia wananchi sio haya..

Ila serikalini wanalao.. na Polepole nae na chama chake nae anayake..
Tabu ingine ni nyie mnaokuza majambo na kuyageuza.. hadi kama wana makosa mnatufanya tuone wapo sawa wanachi sisi.. bikozi mnaboaaaa upinzani nyie. Mngekuwa smati mngeacha wananchi wajiulize wao makwao na kuona kama kuna makosa.. sasa hawa wameongea matatu tofauti nyie hao mnadandia hamjipimi.. eeeeeeeh JPM ananifanya niandike haya.. 2018 na siasa mie hukooooo humu ha ha haa

Ya kujibu ya mtandaoni sioni sababu ya nyie kushangaaa.. maisha ndivyo yamekuwa miaka hii.. au unataka wawasubiri upinzani muwape habari hizo mkifika bungeni.. ondia ushamba baai

Haya najiona hili ni gazeti la kufungia 2017 humu...
 
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji23] [emoji23] [emoji23] happy new year Coco... You know how much I love you... Hebu tumsome kwa pamoja huyu mtumishi alichoandika
IMG_20171230_023508_820.jpg
Sidhani huyu naye ni mmojawapo wa hawa wapinzani wa mitandaoni wanaojua kukosoa tuu... Wasioona jema hata moja.. Sidhani kama ni mmojawapo
 
Wengi tunawashangaa hawa Mkuu lakini hawajachelewa kusimamia haki na uhuru wa Watanzania. Pia ukiondoa Sheikh Ponda Viongozi wa dini ya kiislamu nao wamekuwa kimya mno na wengine hata wamethubutu kuendelea kummwagia sifa huyo mtenda maovu.

Tumechoshwa na hatutaki kuishi nchi inayoongozwa kama ilivyokuwa ikiongozwa na Afrika ya Kusini na wale Makaburu na Wabaguzi wa rangi.
Mliahidiwa kuishi maisha ya kishetani. Ndio Haya maisha yenyewe. Asili ya ushetani ni kuikataa toba.
 
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji23] [emoji23] [emoji23] happy new year Coco... You know how much I love you... Hebu tumsome kwa pamoja huyu mtumishi alichoandika View attachment 663221Sidhani huyu naye ni mmojawapo wa hawa wapinzani wa mitandaoni wanaojua kukosoa tuu... Wasioona jema hata moja.. Sidhani kama ni mmojawapo
cocochanel hawezi kuyasoma kwa sauti maneno yaliyojaa kweli.
 
Wengi tunawashangaa hawa Mkuu lakini hawajachelewa kusimamia haki na uhuru wa Watanzania. Pia ukiondoa Sheikh Ponda Viongozi wa dini ya kiislamu nao wamekuwa kimya mno na wengine hata wamethubutu kuendelea kummwagia sifa huyo mtenda maovu.

Tumechoshwa na hatutaki kuishi nchi inayoongozwa kama ilivyokuwa ikiongozwa na Afrika ya Kusini na wale Makaburu na Wabaguzi wa rangi.
Mkuu,lililopo kwenye kanisa Katoliki ni kama mapadre wapo jeshini.Kila kitu kinaenda kwa vikao,mijadala,kupima,na amri za haohapo.Sina nia ya kuwatetea ila tuwape muda.Ni tofauti na jumuiya zingine ambazo wakuu wao ni mmojammoja na ana uhuru wa kutoa tamko bila kufuata au kusubiri mkubwa wake kuidhinisha.
 
Isifikiriwe kuwa nataka kuleta hoja ya ubaguzi lakini nimeshangazwa mno na ukimya wa maaskofu wengi wakatoliki ambao huwa hawarembi na kupenda kuongea ukweli ulio uchi... Kwenye nyeupe wataita nyeupe na kwenye nyeusi wataita nyeusi... Ila mwaka huu naona kuna kigugumizi na sijaona waraka wowote toka kwao... Hii sio kawaida yao[emoji15] [emoji15] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144]
Huko kuna Niwemugizi na Mapunda tu wengine wanafuata maelekezo kwani mhusika ni mtoto wa nyumbani!!
 
Back
Top Bottom