ugali dagaa
JF-Expert Member
- Oct 18, 2013
- 1,286
- 1,131
Hongera sana kuwa kiongozi wa muhimili mahakama kuaminiwa inaonyesha uadilifu wako, kuna tafiti zilifanywa kipindi ha nyuma zilionyesha kuwa mahakama ni moja ya taasisisi zenye rushwa hapa nchini hivyo kupelekea watu kudhulumiwa haki zao naomba uje na mbinu bunifu ya kupambana na hii, kero nyingine ambayo ina umiza wananchi wenye mashauri yao ni kitendo cha hakimu kuwa na hudhuru, mfano mimi nina kesi na nina mwanasheria nimemkodi ananiwakilisha amekwenda mahakamani maratatu mfululizo kesi zinahairishwa hakimu hayupo ama ana mashauri mengi hivyo mwanasheria bado ananidai kwani nimempotezea muda wake ushauri kungekuwa na jinsi ya kuwajulisha wananchi siku ilyotajwa kesi kama mh atakuwepo ama la ili tusiingie gharama..inaumiza unaambiwa kesi itatajwa mwezi ujao unaenda unaambiwa hakimu amekwenda semina kesi tunahairisha mpaka wiki ijayo ukienda unaambiwa hakimu amefiwa siku nyingine ukienda unaambiwa mashauri yamekuwa mengi hivyo tunahairisha mpaka wiki mbili zijazo namna hii haki inachelewa tu akata tamaa tunapoteza imani na muhimili huu sisi watu wa kanda maalum ndipo tunapolazimika kujichukulia sheria mkononi.