Sala au maombi gani ambayo uliwahi kusali yakaleta matokeo tushirikishe

Sala au maombi gani ambayo uliwahi kusali yakaleta matokeo tushirikishe

Montania

Member
Joined
Aug 30, 2019
Posts
34
Reaction score
42
Kama wewe ni Mkristo mkatoliki ni sala, Novena, Rozali au uliwahi funga kuombea kitu na kikafanikiwa?
Mfano kwenye kuomba kazi, mke au mume au masomo n.k tushirikishe

Pia madhehebu mengine karibuni kushuhudia kulingana na MUNGU alivyokutendea.
 
Novena ya nguvu ya msalaba

Nilipata ushindi mkubwa sana
Ushuhudia kidogo kaka kukuza Iman za wengine kama pia una pdf yake tuma humu huwenda ikamsaidia mtu anayepitia magumu kwasas ili nayeye apone
 
Sala ya baba yetu ,nilikanyaga kitu kibaya (nahisi)nikapotea Kwa masaa 7 porini,nilipokosa tumaini na ufaham kunijia kua nitakua nmepotea/kupotezwa kishirikina,
nikasali Sala ya baba yetu mana ndo Sala pekee nlikua naijua vzr.kufumba macho na kufumbua nikapata njia iendayo Hadi nyumban Moja Kwa Moja.
 
Ushuhudia kidogo kaka kukuza Iman za wengine kama pia una pdf yake tuma humu huwenda ikamsaidia mtu anayepitia magumu kwasas ili nayeye apone
Mnakosea sana kumuomba MUNGU MWENYEZI wakati wa shida tu

Sali kila siku njia ya msalaba
Then jitamkie baraka kwa njia ya msalaba unaitaja baraka then una iamuru ishuke kwa nguvu ya msalaba

Kama kulaan unalaan kwa nguvu hicho kinachokusumbua kwa nguvu ya msalaba

Jitaidin uwe unafunga acha anasa na ujinga

Mtumainie BWANA YESU KRISTO maana ndiye MFALME
 
Kama wewe ni Mkristo mkatoliki ni sala, Novena, Rozali au uliwahi funga kuombea kitu na kikafanikiwa?
Mfano kwenye kuomba kazi, mke au mume au masomo n.k tushirikishe

Pia madhehebu mengine karibuni kushuhudia kulingana na MUNGU alivyokutendea.
Ni nyingi ila nitaelezea moja, Mama alininunulia kile kitabu cha mawaridi ya sala nilivyoanza form one, so nilikua nasali zile sala mara kwa mara, sasa nakumbuka kipindi nipo form three ilipokaribia mitihani ya mwezi wa sita basi nikaweka nia , nikaanza kusali novena ya "mt Anthony" ipo kwenye mawaridi ya sala.

kila siku asubuhi kabla ya kuanza mitihani nasali na jioni nasali ombi langu lilikua "Mungu anisaidie nifaulu vizuri mitihani yangu, anikumbushe yale yote nitakayosoma na awe pamoja na mimi kwenye chumba cha mtihani".nilikua ni mmoja wa wanafunzi wazuri tu kwa darasa langu nilikua najua siwezi kufeli lakini basi tu, niliamua kujiombea,😃.

Basi bwana siku hiyo tukaletewa paper ya physics(lilikua somo langu pendwa pamoja na Maths), yaani ile paper ilikua kama mwalimu anatukomoa hivi, kwa kifupi nilitoka sina matumaini mazuri kabisa, sasa wenzangu wanatoka wanaelezea njia walizofanya, maana tulikua na group discussion naona watu wanatiririka tu jinsi walivyojibu maswali ambayo mimi yalinitatiza, lakini niliyafanya, kwakweli niliona hali yangu ni tete nikifaulu sana basi 60sivuki hapo.

Hatimaye siku zikaenda, sikuhiyo tupo uwanjani ilikua siku ya michezo,tukaja kuitwa form three science wote tunaitwa na mwalimu "Adrian" alikua mkali balaa , kapanga karatasi from the worst to the best na fimbo mbili zimenyooka.

Kwanza kaanza kutupiga beat hapo, kauliza nikifundisha hamuelewi au shida nini? akasema nusu ya darasa wapo below fifty, watu kimyaaa.

kaanza kuita majina unatajiwa na marks zako mbele ya wanafunzi wote then kama upo below fifty unakula fimbo za kutosha halafu unaenda kukaa, halafu kama ni mwanafunzi mzuri lakini sikuhiyo hujafanya vizuri kama kawaida yako unakula fimbo hatakama umepata above fifty.

hapo natetemeka balaa naona karatasi zinaenda tu siitwi, mwisho wakaitwa wote ikabaki ya kwangu akaniambia njoo mbele nikaenda, akaniuliza unahisi umepata ngapi? Nikamwambia 85, maana aliyekua wa pili alikua ana 80%, akaniambia NO una 98% daah!!!! nikaanza kulia😄😄😄 mwalimu anacheka ananiambia ukiendelea kulia nakuchapa ili ulie vizuri😃😃, wanafunzi wenzangu wakapiga makofi meengi , hii moment huwa siisahau na mpaka leo ule mtihani ninao nimeutunza.

Nilianza kukagua yale maswali ambayo nilikua nauhakika sijafanya vizuri nikakuta nilifanya kwa njia ambayo mwalimu hakufundisha nikawa najiuliza hii njia nilitoa wapi?? So kwenye kila swali mwl alikua anasahihisha anaweka comment "great job" au " excellent" , paper ilichafuka kwa remark nzuri za mwalimu.

Hapa ndipo mbegu ya kumtegemea Mungu ilipandwa.
Hata sasa hivi nimeshakua mtu mzima,( mwaka 2019 niliokoka rasmi) nguzo yangu ya kwanza kwenye maisha ni kumtegemea Mungu wakati wote na nyakati zote niwe na raha au shida nipo na Mungu tu.

huwa nikipita kwenye changamoto naona kama sioni mbele, sioni kama nitatoboa basi huwa nakumbuka hiki kipindi hapa nasema Mungu anasikia maombi na anajibu so naendelea kukomaa.Kwa kifupi maisha yangu mpaka hapa nilipo ni Mungu tu na hakuna kitu naogopa kama kumkosa Mungu kwenye maisha yangu.
" Kwa maana ndani yake tunaishi,tunakwenda na kuwa na uhai wetu"(Mdo 17:28).
 
Back
Top Bottom