Sakho na Phiri waomba kuondoka Simba

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
Wawakilishi wa Mchezaji Pape Ousmane Sakho hawaridhishwi na kukosekana kwa muda wa kucheza kwa Mteja wao ndani ya Simba, wakiamini Msenegal huyo anastahili muda zaidi wa kucheza.

Kutokana na hilo kwa mujibu wa taarifa nilizopata ni kuwa kuna baadhi ya ofa watazifikisha Msimbazi kumhusu Mteja wao ambazo zitakuwa na maslahi kwa Simba kiuchumi ili POS aweze kuondoka kusaka changamoto mpya.

Sakho alisaini kandarasi ya miaka mitatu na Wekundu wa Msimbazi, akiwa ametumikia miaka miwili huku kipengele cha mkataba kikimtaka alipe mshahara wa miezi mitatu tu ili avunje mkataba wake, tayari ameshaandika barua.

Wanaamini Kijana anastahili muda wa kucheza zaidi, ijapo mpaka sasa bado hakuna ofa mezani kwa Simba huku zikitarajiwa mwishoni mwa msimu.

Mchezaji mwingine aliyeomba kuondoka Simba ni Mzambia Mosses Phiri, ambapo wanakuwa ni wachezaji watatu mpaka Sasa hivi baada ya Awali Joash Onyango kuandika barua ya kuondoka klabuni hapo.
 
1. Phili ni mchezaji wa KAWAIDA sana.
ZORAN MARK NA ROBERTINHO MAKOCHA WOTE HAWAKUMUAMINI.


2. ALAFU Bahati Mbaya zaidi phili ni no 10.
Hiyo namba Ina watu kama
Sackho.
Chama.
Saido.

3. JARIBU kumuangalia Phili vizuri akiwa na mpira anaanguka sana, anapoteza mno, anapata majeraha mengi.

Mechi ya Simba na yanga 1.1 ndio nilipomchunguza phili vizuri. Alikuwa mbovu mno

UBORA WA PHILI.

Phili ni mzuri kwenye kufunga tu
 
Haya Makolo, Sakho akilipa mishahara ya miezi mitatu mtakubali aondoke? Au ni kiherehere tu huwa kinawasumbua kwenye kesi ya Feisal?
Kwani mkataba wake una hicho kipengele?
Kama unacho na alipe aende kutafuta changamoto mpya.
Ni upumbavu kuwa na kipengele kama hicho kwa mchezaji unayemtegemea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom