Sakata la Wazee EAC: Litaisha lini?

Iteitei Lya Kitee

JF-Expert Member
Jan 2, 2008
586
46
Taarifa zilizofika hivi punde ni kuwa wale wazee wetu wa iliyokua Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekuja na style mpya ya kushinikiza madai yao baada ya kuamua kufunga barabara ya Ali Hasan Mwinyi karibia na Salender ili kuonyesha ni jinsi gani wamechoshwa na usanii na uonevu huu wa serikali yetu.
Hii ni hatua mpya binafsi nimependa style yao LAKINI JE SERIKALI YETU ITAWASIKILIZA au ndo yale yale ya kuziba masikio?

Taarifa zinasema kuwa kikosi cha askari kimetumwa kikiambatana na gari la maji ya kuwasha kwenda kuwaondoa bara barani.
Habari ndio hiyo,
KWELI TUMECHOKA NA MFUMO HUU WA LICHAMA HILI LA JEMBE NA NYUNDO huku kiukweli NI UFISADI NA UBINAFSI
 
Usalama wa taifa uko wapi?

Mmambo kama hata kipindi cha mwalimu hayakuweza kutokea ila leo yamezidi sana

Nchii hii Rais hana uwezo na madaraka.

Usaniii umezidi,kipindi kile Zuma amekuja hapa nilizungumza naye alilaumu sana RAis kushindwa kuwalipa wastaafu na alimwambia JK kama ameshindwa kuwalipa wastaafu basi awaombe ANC wamsaidie Kulipa.

wastaafu wamevua nguo kwa sasa

RAis alianza kucheka cheka.

Now Naungana nao,.JK might be one term President.
 
Wazee wa EAC wametolewa bararani kibabe na sasa magari yameanza kupita. Kandoro na Kova hawakusikilizwa kabisa. Kule Kigamboni nako kivuko kimenasa kwenye mchanga na watu wengi sana wamenasa.
 
ni kweli. watu wanadai haki ya msingi wanapewa majibu ya kisanii sasa wanatafuta njia yoyote wapate haki yao. kielelezo kigine cha utawala tulio nao. hakuna viashiria zaidi ya hivi. waalimu ndio walishindwa kufanya kweli

magari hayaendi kabisa. wanaambiwa wapite morogoro road.
 
it means presdent kikwete is not aware of what is going on au ameamua tu kuwa kimya huku wazee wetu wakiendelea kuteseka kwa kudai mafao yao?ifike mahali watanzania tuamue kwa pamoja kuwa 2010 kikwete na serikali ya kifisadi isirudi madarakani maana sasa tumechoka na mogomo maandamano kila kukicha. KIWETE should be one term president.
 
Cha kusikitisha zaidi polisi wanawakamata wale wazee kwa ubavu jamani wale ni kama babu zao hao polisi kweli polisi ni kama mbwa akiambiwa kamata anakamata.
Ila wazee wanaushirikiano walivyo ona wenzao wanaingizwa kwenye karandinga na wengine nao wakaamua nao kuingia kwenye karandinga.
Sasa sijui wanawapeleka wapi jamani?
Wanadai jasho lau serikali inawapiga dana dana.
 
Leo tumejionea mengi kwa kweli...Kandoro, Kova na Kimbisa wakiongoza magari. Tusubiri tamko la serikali kuhusiana na hali hii...hasa hasa Rais Kikwete atakapoongea na taifa mwisho wa mwezi kama ilivyo ada.
 
ndugu wanajamvi, wastaafuu wa East Africa Community wameonyesha kwa vitendo kwa kujilaza katikati ya daraja la Salender tangu saa moja leo ikiwa ni ishara ya kudai haki zao. Maadam asilimia kubwa ya viongozi na watendaji wa serikali wanatumia barabara ya mwinyi kuingia mjini basi wazee hawa waliamua kufanya vitu vyao hapo.

kwa nini wahusika wasimalize matatizo yao badala ya kuendelea kuwa arrogant? nasikia Kandoro (RC wa DAr) alikuja kuwaomba waondoke akiambatana na wakuu wa polisi.

na bado!!! may be itumike tactic hiyo kudai mafisadi wote wa EPA washitakiwe kwa kosa la jinai na si wale wachache watakaotolewa kafara.
 
Ukiona wazee wa umri kama huu nao wameamua kulala barabarani ili kuishinikiza serikali iwalipe mafao yao basi ujue kwamba serikali haina nidhamu kwa wazee wa nchi nzima. Tanzania ya amani si ile tunayoiimba katika halaiki. Sasa imekuwa ni nchi inayoongozwa na viongozi waliokubuhu jeuri. Ifike wakati mkawapa heshima zao wazee hawa kuliko kuacha wakaharibu "image ya Tanzania katika siasa za kimataifa. Ni aibu sana kudhulum wazee kama hawa.
 
Last edited:
kwa kweli wazee walikuwa wanasikitisha kweli ila nawaunga mkono nitajaribu kuwaletea picha ila kwa sasa wameondolewa kwa nguvu na barabara inapitika foleni ni kubwa sana
 
Wazee wa EAC wametolewa bararani kibabe na sasa magari yameanza kupita. Kandoro na Kova hawakusikilizwa kabisa. Kule Kigamboni nako kivuko kimenasa kwenye mchanga na watu wengi sana wamenasa.
Wazee wawatu wamechoka ile mbaya nawaona hapa ndio wanapita barabara ya bibi titi karibu na maktaba kuu ya taifa.sijui hata wanakwenda wapi wakongwe wawatu.Kweli hii serikali ya kikwete sijui baada ya miaka miwili itakuaje
 
Asasi za kijamii zinazojali na kupigia kelele haki za binadamu watakuwa wamefanya la maana sana wakienda kwenye matukio kama hili. Uwepo wao ungekuwa na nguvu zaidi kuliko kauli wanazokuja kutoa baadae.


Kuna sheria inayoweza kuwaweka matatani? Mfano, wakienda pale na kuwapa maji ya kunywa waandamanaji?


Bravo kwa wazee wa EAC! Nasubiri picha kwa hamu.
Message sent and DELIVERED!






.
 
yani hawa wazee wanatia huruma kupitiliza, Baada ya kutangaziwa wanaombwa kuachia njia walihiari na kuondoka ila jeshi likaona bado haitoshi kuwaacha waondoke polepole bali waliwasweka wengine kwenye karandika lao na hatujui wamewapeleka wapi. Kandoro amelaani vikali mkutano huo aliouita ni haramu na kuwataka wazee hao kuendela kuwa na imani na serikali yao makini.
Our ears are close to capture what will happen to those taken by police.
 
Wazee wawatu wamechoka ile mbaya nawaona hapa ndio wanapita barabara ya bibi titi karibu na maktaba kuu ya taifa.sijui hata wanakwenda wapi wakongwe wawatu.Kweli hii serikali ya kikwete sijui baada ya miaka miwili itakuaje



Hao wanakuja maeneo ya bustani Mnazi mmoja ndo kijiwe chao kikubwa pale na mipango yote wanapangia pale.
Mida flani nitawazungukia kujua nini kinaendelea.
Lakini serikali haiwafanyii fair wazee wana doc. zote lakini ndo kwanza watendaji wa serikali wameweka pamba kwenye masikio yao.
Jamani tujiulize hizi pesa wanazo wazungusha wanazungushia kwenye biashara zao nini.Lazima tujue.
Isije ikawa kama Kandoro pesa za michango ya shule yeye anajinadi kwao Iringa kwa kutaka kugombea ubunge 2010.
 
Back
Top Bottom