Sakata la vitendanishi; Aliyerekodi ageukwa, Rose hana kosa

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,245
103,946
Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA) kimesema kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii tarehe 05 January 2023, na kuzua taharuki kwa jamii ikiwahusisha Watumishi wa Kada ya Afya wawili ambao ni Rose Shirima (Muuguzi Mkunga) na James Getogo Chuchu (Mtekenolojia wa maabara), wote wakitokea Halmashauri ya Wilaya ya Uyui Zahanati ya Ishihimulwa Mkoani Tabora.

Kufuatia tuhuma hizo Chama hicho kwa kushirikiana na Viongozi wa tawi la Tabora walifanya uchunguzi ili kujiridhisha na uhalisia wa tukio hilo ambapo Chama kimewatoa hofu Wananchi hasa wanaopata huduma za afya katika Zahanati hiyo kuwa hakuna vitendanishi vyovyote vilivyoisha muda wake ambavyo vilikuwa vinatumika katika kituo hicho kama ilivyokuwa inaelezwa na Mtekinolojia wa Maabara katika video iliyosambaa na hata kusababisha taharuki nchini.

“Vitendanishi vilivyopo vinakaribia kuisha muda wake yaani bado vina miezi 3 mbele mpaka tarehe 14.04.2023, hivyo alichokuwa anasimamia Muuguzi (Rose) kilikuwa sahihi kwa kufuata utaratibu wa mfumo wa udhibiti bidhaa (Stock control system using FIFO and FEFO principles), lakini pia alikuwa akisimamia maamuzi ya kikao chao cha ndani”

My Take
Nilijua tu yule jamaa ni mzushi, dume zima unakaa kurekodi watu. Kama mwanaume si upeleke kwenye vikao?
 
Lazima wamsaidie means ndo tabia zao

James akiambiwa atoe ushahidi atabaki kubabaika kuwa niliona, niliona!
Angetakiwa awe mjanja, awe na Akili, Akili yake, iende mbali.
Kama aliamua kufanya kitu angefanya kweli.

Angerekodi kwanza hivyo vifaa vilivyo-expire kisha ndio akamrekodi huyo Bidada.
Lakini Kwa vile anaakili ndogo, akashindwa kuona kitakachomtokea.

Ingawaje hata angerekodi hivyo vifaa bado isingemsaidia kutopewa adhabu Kali.
Ila ingemsaidia kutufanya Sisi tusiopenda maneno matupu kuuelewa ukweli.
Vinginevyo ameifanya kesi yake kuwa na maswali mengi.
Wapo watakaoona anaugomvi na Yule Rose.
Wapo watakaomuona mkweli lakini ushahidi WA maneno yake kuthibitisha ukweli haupo.

Mwisho ameichafua serikali. Na ukiwa Mtumishi WA serikali ukiichafua serikali matokeo yake yanajulikana
 
Ni wasioelewa tu wanaomponda jamaa ,mimi naamini vilikuwa vimeisha,maana yule dada hakuna sehemu alitamka bado vinafaa ,au vina miezi mitatu,na yule jamaa si mjinga afanye alivyofanya kama hakuwa na uhakika,, mahospital kuna matukio kila kukicha yanatokea,inaniwia vigumu kuamini,mimi niko upande wa wagonjwa
 
Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA) kimesema kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii tarehe 05 January 2023, na kuzua taharuki kwa jamii ikiwahusisha Watumishi wa Kada ya Afya wawili ambao ni Rose Shirima (Muuguzi Mkunga) na James Getogo Chuchu (Mtekenolojia wa maabara), wote wakitokea Halmashauri ya Wilaya ya Uyui Zahanati ya Ishihimulwa Mkoani Tabora.

Kufuatia tuhuma hizo Chama hicho kwa kushirikiana na Viongozi wa tawi la Tabora walifanya uchunguzi ili kujiridhisha na uhalisia wa tukio hilo ambapo Chama kimewatoa hofu Wananchi hasa wanaopata huduma za afya katika Zahanati hiyo kuwa hakuna vitendanishi vyovyote vilivyoisha muda wake ambavyo vilikuwa vinatumika katika kituo hicho kama ilivyokuwa inaelezwa na Mtekinolojia wa Maabara katika video iliyosambaa na hata kusababisha taharuki nchini.

“Vitendanishi vilivyopo vinakaribia kuisha muda wake yaani bado vina miezi 3 mbele mpaka tarehe 14.04.2023, hivyo alichokuwa anasimamia Muuguzi (Rose) kilikuwa sahihi kwa kufuata utaratibu wa mfumo wa udhibiti bidhaa (Stock control system using FIFO and FEFO principles), lakini pia alikuwa akisimamia maamuzi ya kikao chao cha ndani”

My Take
Nilijua tu yule jamaa ni mzushi, dume zima unakaa kurekodi watu. Kama mwanaume si upeleke kwenye vikao?
Mimi sipendi watu vielehele hasa maofisini Ila napenda wanaochukia uchafu makazini Ila Kwa nchi hii ukishajifanya unataka kuwa msafi mmoja Kati ya wachafu 100 utapotea wewe na kupoteza ajila,kingine Yule aliyerekodiwa Ni mwanamke mujue nguvu yake katika mambo yetu.
Mwisho ni Bora kuishi kutegemeana na mazingira Ni ngumu kuichafua taasisi kabla wewe ujachafuka.
 
Sawa dada rose Hana makosa VP lugha aliyotumia wakat akiongea na yule jamaa nayo siyo kosa au ?
 
Hakuna sehemu rose alitamka kuwa vilibaki miezi mitatu,tulichosikia ni kusema katumie hivyohivyo,hatumuamini rose na hatuwamini na ninyi,napata uhakika baada ya jamaa kumwAmbia rose kavitumie wewe,haki ichukue mkondo wake
 
Hii nchi kumbe humu wengi maofisini wa hovyo tu kaahhh....mnamtetea rose kabisa?kosa la James ni lipi?
Tuwe wazalendo bwana
 
Back
Top Bottom