Muuguzi Mkunga na Mteknolojia wa Maabara wakutwa na Tuhuma za kujibu, Wasimamishwa kazi

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
89AF6800-66BD-4911-AB12-EDF175ECE5A6.jpeg


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uyui mkoani Tabora amewasimamisha kazi Rose Shirima, aliyekutwa na tuhuma ya matumizi ya lugha isiyo na staha mahali pa kazi na James Chuchu aliyekutwa na tuhuma ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii na kuleta taharuki katika jamii.

Hatua hiyo inakuja kufuatia video iliyosambaa mitandaoni ikiwaonesha watumishi hao wa Zahanati ya Ishihimulwa iliyopo Uyui mkoani humo, wakijibizana kuhusu matumizi ya vifaa (vitendanishi) vya kupimia Malaria (mRDT) vilivyoisha muda wake wa matumizi.

Uchunguzi uliofanywa na Wizara ya Afya, TAMISEMI pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, wamebaini kuwa katika Zahanati ya Ishihimulwa iliyopo Uyui mkoani Tabora hakuna mgonjwa aliyepimwa malaria kwa kutumia vitendanishi vilivyoisha muda wake wa matumizi.

Licha ya uwepo wa vitendanishi vilivyoisha muda wake wa matumizi tangu mwezi Agosti 2022 na kwamba zahanati hiyo ina vitendanishi ambavyo vitaisha muda wake Aprili na Desemba 2023.

Aidha uchunguzi pia umebaini kuwa kuna mahusiano yasiyoridhisha kwa baadhi ya wafanyakazi katika zahanati hiyo, usimamizi wa kituo usioridhisha na kwamba watumishi wanne wa zahanati hiyo wamekutwa na tuhuma za kujibu.

Sambamba na hayo, Bi. Rose Shirima na Bw. Getogo James Chuchu wamefikishwa kwenye mabaraza yao ya kitaaluma kujibu tuhuma walizokutwa nazo. Pia, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uyui atachukua hatua za kinidhamj na za Kiutumishi kwa Watumishi wengine wawili (2), ambao ni Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Ishihimulwa na Mratibu wa Huduma za Maabara Halmashauri ya Uyui kwa sababu nao walikutwa na tuhuma za kujibu.


Kuhusu tukio hilo, soma >>> Tabora: Mtumishi wa Afya akijibu mbovu kwa watu kumstukia juu ya vitu vilivyo-expire
 
Walikua wanajibizana wao kwa wao, yaan mngesikia wanavyotujibu na sie wateja wala msingeamini
 
Back
Top Bottom