Sakata la posho: Spika Anne Makinda alichemsha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata la posho: Spika Anne Makinda alichemsha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Dec 14, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Dec 14, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  Ni dhahiri kauli ya Spika Anne Makinda kuwa wabunge wanaongezewa posho kwa vile gharama ya maisha Dodoma iko juu inaonyesha udhaifu walionao viongozi wetu wengi; kukosa uelewa wa hali halisi.

  Kiukweli, kwa kauli ile, Spika Anne Makinda alichemsha. Na ili tuelewe ni vema tukaingalia picha pana badala ya kipande cha picha. Tatizo hapa si Anne Makinda bali ni mfumo. Ndio, Anne Makinda ni kielelezo cha tatizo la kimfumo. Kwamba mfumo wetu, mbali ya udhaifu mwingine, unaowafanya viongozi wetu wawe ’ masultani’. Wakae kwenye nyadhifa za kisiasa na kiserikali kwa muda mrefu sana kiasi cha kupoteza uelewa wa hali halisi za wananchi wanaowaongoza.

  Kwa mfano, tangu niko shule ya msingi nimelisikia jina la Anne Makinda katika nafasi za uongozi. Hivyo hivyo nimeyasikia majina ya akina Samwel Sitta, Malecela , Pius Msekwa na wengineo. Ndio, ni ukweli, kuwa nchi yetu ambayo asilimia kubwa ina raia vijana inaongozwa na wazee waliostahili kumpumzika na kuwaachia nafasi vijana.

  Sina maana kuwa wazee hawana sifa za kuongoza, isipokuwa, tufanye sasa juhudi za makusudi za kuandaa mifumo itakayotufanya nafasi za uongozi zisishikiliwe kwa muda mrefu na watu hao hao. Tuanze sasa kufikiria kwa dhati kuandaa utaratibu wa kuwaandaa vijana ili waje kuwa viongozi bora. Vile vile, utaandae utaratibu utakaofanya Mbunge asikae bungeni zaidi ya vipindi viwili kwa maana ya miaka kumi.

  Angalia sakata hili la wabunge na posho . Kwa hakika ni moja ya mambo ya kuhuzunisha yanayotufungia mwaka. Kwamba imefika mahali wabunge wetu wamefikiria kuongezewa posho kutoka shilingi elfu sabini hadi laki mbili kwa siku, tena katika wakati huu mgumu kiuchumi ambao mamilioni ya WaTanzania wanaupitia. Huu ni usaliti kwa nchi yetu na si kitu kingine.

  Kwa Spika Anne Makinda, kama mwanadamu yumkini alighafirika. Ulimi hauna mfupa na hakuna mwanadamu asiye katika hatari ya kunena lililo baya masikioni mwa wanadamu wenzake. Spika Makinda hajachelewa. Atoke sasa, na kwa sauti yake mwenyewe, awaombe radhi WaTanzania. Akifanya hivyo atasamehewa. Maana atambue, ya kwamba kuwaambia WaTanzania maisha ya Dodoma kwa Wabunge ni ya gharama ya juu inatoa tafsiri mbaya.

  Ni kauli mbaya maana Wabunge wetu ukilinganisha na mamilioni ya WaTanzania, hata bila posho ya shilingi hamsini kwa siku, bado watakuwa na maisha ya neema kubwa kuliko wapiga kura wao wengi. Yawezekana kabisa unavyosoma makala hii kuna mama MTanzania anayejifungua akiwa amelala sakafuni, au kuna mtoto wa KiTanzania anayekufa kwa malaria kwa vile zahati haina dawa. Ndio hali halisi. Huu ni wakati kwa viongozi wetu kuacha kuendekeza ubinafsi.

  Viongozi wakiwamo Wabunge waanze sasa kuwafikiria wananchi ambao wengi wako katika hali mbaya kiuchumi. Ni wananchi hawa ambao miongoni mwao kuna wakulima. Ni wakulima hawa ambao posho ya laki mbili kwa siku kwa mbunge ingetosha kwa mkulima huyu kununua mbolea mifuko mitatu ya kilo hamsini kwa mfuko. Ni mbolea ya kupandia na kukuzuia kwa ekari moja. Tujiulize; tuko sasa kwenye ” Kilimo Kwanza au Wabunge Kwanza?”

  Ndugu zangu, hii ni sehemu ya makala yangu ya juma hili kwenye gazeti la Raia Mwema. Nahitimisha.

  Maggid,
  Iringa.
  Jumatano, Novemba 14, 2011
   
 2. M

  MR NDEE Member

  #2
  Dec 14, 2011
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 54
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 15
  Bro ukichunguza kwa makini kauli ya Makinda utagundua kuwa serikali ina mpango wa kupandisha posho ila inapima upepo umekaa vipi,vyama pinzani,waandishi,wanaharakati wasipokemea hili itapanda tu.haiingii akilini kuwa eti garama Dodoma zimepanda hiki ni kisingizio na matusi kwa wananchi kuwa hawajui hali za wananchi, na upendeleo na ubaguzi wa kijiografia na huenda kwa mwendo kama ulivyojitokeza katika bunge la bajeti kwenye barabara wananchi watagawana kimikoa.

  Serikali imekuwa ikidai ni sikivu lakini ni maslahi kwanza,maombi kesho.wanatoa sababu za kutudanganya dhahiri shahiri na kwa maamuzi ya kibabe.WAKATI WA MABADILIKO NI SASA
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Dec 14, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Hawa ndo wa kuwabebea mabango maana hizo posho zao zinatokana na jasho letu moja kwa moja.
   
 4. MwafrikaHalisi

  MwafrikaHalisi JF-Expert Member

  #4
  Dec 14, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 1,746
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kipaumbele ni Kilimo au Posho? Actually, nchi hii kipaumbele ni UFISADI. Hakuna kinachopewa kipaumbele kwenye matendo kama UFISADI. Si Kilimo Kwanza, Nishati na Madini (kwa mwaka huu wa fedha, hasa suala la umeme), Elimu wala Afya. Ni maneno matamu tu aka blah blah! 'Hiri rinchi rinachosha'
   
 5. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #5
  Dec 14, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Maggid, NN na Ndee;

  Kwanza, msitarajie kuwa Makinda aliongea aliyoongea kwa bahati mbaya! Tushadharauliwa vya kutosha, wanasiasa wanatuona kama hatuna akili vile. Wapo wanaotujali, wamejaribu na inaelekea wananchi hatuwapi ushirikiano.

  Imagine, ili madudu kama haya yapite wanahakikisha wanapandikiza wapinzani (mamluki) ambao watatofautiana na wenzao na hivyo kuhakikisha hoja kama hii inapita bila kupingwa.

  Hili si la wapinzani wala wanaharakati tu kupigiwa kelele, hapana! Madaktari wa Tanzania wanaona mfano wa wenzao Kenya, japo hatupendi watanzania wenzetu wafe lkn umefika wakati ambapo madaktari wetu ambao badala ya kuwahudumia wagonjwa mahospitalini kila mmoja kaanzisha 'ujasiriamali' na kujiita 'specialist' hivyo kumlazimisha mgonjwa ahame hosp ya serikali na kumfata mtaani; waonyeshe njia! Wagome, waishinikize serikali kupata unafuu wa maisha.

  Wakufunzi/wahadhiri; ninyi ndo wasomi wa nchi hii. Tunawapenda wanetu na tungependa wasome kufikia wengine tuliko. Kukimbia tatizo si kutatua tatizo, msiikimbie nchi, wala msifanye migomo baridi. Wekeni wazi msimamo wenu juu ya mambo kama haya, serikali ikionyesha kukaidi kwa pamoja shikamaneni, waeleweshe wanafunzi ugumu wa maisha mnaokabiliana nao, wao badala ya kuandamana kwa ajili ya 'boom' watawasaidieni kuandamana kwa ajili ya ongezeko la mishahara yenu.

  Maisha ni magumu kwa kila mtanzania, hali inazidi kuwa tete na vitu vinapanda hakuna control, ni kama nyumba imekosa kinara wa kuiongoza. Ni wauza mafuta tu walofungwa kengele (sijui iliwezekanaje?).

  Inasikitisha sana
   
 6. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #6
  Dec 14, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Siasa zetu, viongozi wetu, in relation na mambo halisi yalo mzongo Mtanzania..... Kweli kabisa kama ni Mzalendo na wafuatilia kwa waweza wehuka kabisa!
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Dec 14, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Tatizo uwoga wetu kukabiliana na wanasiasa matumbo na posho.

  Hawa jamaa utakuta wanawaingilia wataalamu katika fani zao lengo kujipatia masilahi binafsi ambazo ni posho na cha juu.
   
 8. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #8
  Dec 14, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  You mean it? So mnawaogopa?
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Dec 14, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ni dhahiri tunawaogopa hawa jamaa wenzetu wanaishia kusema huyo ni chaguo la Mungu.
   
 10. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #10
  Dec 14, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hivi anne makinda ana cheo gani vile?
   
 11. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #11
  Dec 14, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Madiwani wa Mkoa wa Dodoma nao wamechachamaa wanadai waongezewe posho kutoka 120,000 kwa Mwezi hadi 300,000 kwa vile gharama za maisha zimepanda Dodoma!

  Tunasubiri kauli za watendaji wa kata Dodoma nao watangaze madai yao!
   
 12. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #12
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Dawa ya bunge hili la POSHO liko jikoni.

  Tutawafyekeni kwa kutumia Uwezo wa Kura zetu ifikapo 2015 kwa zaidi ya asilimia 85 % kuwavuteni shati kuwaondoa kabisa hapo Bungeni. Wabinafsi wakubwa hawa bila hata chembe cha UTU.

  Tena kwa kuanzia vizuri ni kwamba vijana tunahitaji watu wazuri wajitokeze na tutawapigieni kura nyingi sana kuondoa huyu 'spika MASLAHI YA CHAMA' pamoja na naibu wake na huyu mwanauchumi uchwara Shibuda.

  Si kero tu, ni simanzi kwa wabunge wetu hawa kudai maziwa toka kwa ngombe asiyelishwa chochote Tanzania hii; vilema kibao wa UFISADI tena tuendelee kuwabebeni mabegani kwa miaka kibao?????????
   
 13. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #13
  Dec 14, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  lets face it, the vause of the problem ni viongozi wazee au mfumo wa kibinafsi na wakutokuhoji? Kama tatizo ni mfumo kama maggid anavyosema, basi hatunabudi kufanya overhaul ya system.

  Sasa tujiulize, hii system imekikaje na inatetewa na nani? Tukimjua mhusika, tumuondoe.....asitudanganye atabadilika, atuonyeshe kwamba amebadilika akiwa nje, apumzike.

  Maggid, tatizo sio uzee wa viongozi, tatizo ni mfumo uliowaweka na unaowafanya watutawale. Mfumo ambao unapelekea mtanzania hata wa mjini mwenye access ya taarifa kufikiri huduma za kijamii kama hospitali na maji ni favour kutoka serikalini.

  Mfumo unaomfanya mama mjamzito wa Tunduru aseme tunaomba serikali itusaidie ......sio tunataka serikali ilete dawa na vitanda.

  Sasa tufanyeje??? Labda tuanzie na ushauri wa invizibo......lakini je, wakulima wamgomee nani??? Na hawa ndo mtaji wa hawa ndugu zetu, na ndio wanaotaabika, ndio wanaopelekewa ambulance za bajaji, ndio wanaoambiwa wanunue power tiller katika inflated price n.k.

  Tafakari.........nitarudi.
   
 14. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #14
  Dec 14, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  madiwani wa Morogoro nimesikia leo nao wanadai ongezeko la posho toka 130k kwa mwezi mpaka laki 2 kama sijakosea.....wanadai wao wana deal sana na wananchi zaidi ya wabunge.....kesho polisi,manesi......
   
 15. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #15
  Dec 14, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,923
  Likes Received: 631
  Trophy Points: 280
  MSIBISHANE HAYA MAJIBU HAPA CHINI.


  For the last two weeks there has been a fierce debate on allowances given to members of parliament fuelled by recent revelations by two leading dailies Mwananchi and The Citizen. The revelations were first denied by the Clerk of the National Assembly but later in a swift move confirmed by the Speaker.

  Members of Parliament herein referred as MPs are entitled to various allowances in conducting their affairs. According to the National Assembly administration act these are subsistence allowance, travel allowances, constituency allowance and for those holding parliamentary portfolios a responsibility allowance. Sitting allowance is paid to MPs everyday he or she attends a committee meeting or parliamentary debate. However this allowance is not mentioned in the law. Currently an MP receives TZS 70,000 ($40) a day as sitting allowance.

  A member of Parliament in Tanzania receives a monthly salary as a renumeration for the legislative, representative and oversight role he or she does. On top of that he or she is paid for sitting! Sounds ridiculous for sure.

  During the 5th session of Parliament which ended in November 2011, MPs lobbied for an increase in allowances claiming that costs of living have skyrocketed. MPs are paid per diem to cover costs of living, but in an interesting move the Parliamentary service commission passed a resolution to increase a sitting allowance to TZS 200,000 ($130) a day.

  Sitting allowance doesn't address the challenge of cost of living, it is subsistence allowance that is pegged to costs of living. I asked one of my colleague who serves in the Parliamenatary Service Commission about this and she said, per diem applies to all civil servants so an increment to it would mean an increment to all civil servants so it must be avoided. And they did avoid and went ahead directing The Clerk to effect new rates.

  The Clerk refused as the law requires that the President of the United Republic approve the new increment in writing. Hence the divided stand between the Clerk and the Speaker. When the news reached investigative and news hungry editors of the media the difference between them was all out and the public outcry was huge.

  The President hasnt approved the new increment so far, some credible sources say that Speaker didn't even attempt to send the requests to the President. The Parliamentary Service Commission met over the weekend and revoked their proposal. Media has played its role and the public won.

  A senior parliamentary staff told me the other day, that the whole matter was a hoax. MPs pressured the Speaker to increase allowances and even threatened her that she will be relieved from her post. Speaker in turn pressured the Clerk to pay new rates contrary to the laws and regulations. Public through media pressured both of them and the President did not dare increase the sitting allowances rate. So far the public has won.

  Is it a temporary victory? Definitely yes.

  The highest prize is scrapping sitting allowances regime altogether. Paying an MP for sitting isn't justified. The public, NGOs/civil society organisations and the media should campaign towards this to the very end. The allowances culture is killing our Nation as it misdirect public funds from public investments to current spending.

  It kills our working culture as public office holders keep attending meeting after meeting to earn sitting allowances instead of working.

  Our country faces mountain of challenges, it requires us to work and create an enabling environment for economic activities that create jobs, add value to our produce, increase our exports, produce more food and generate more electricity. Otherwise no one will call us a nation.
  Scrap sitting allowances, create jobs to the people.


  Source: http://zittokabwe.wordpress.com/2011/12/13/scrap-sitting-allowances...
   
 16. MwafrikaHalisi

  MwafrikaHalisi JF-Expert Member

  #16
  Dec 14, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 1,746
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Really??
   
 17. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #17
  Dec 14, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Mkuu maisha yamepanda Dodoma, siyo kwa wabunge tu, na wananchi watahitaji huruma ya spika!
   
 18. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #18
  Dec 14, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mtoa mada, tambua kuwa baadhi ya wanaotaka posho ziongezwe ni VIJANA pale bungeni, hao je wanawekwa kwenye kundi gani?

  Nadhan mnawajua wana JF, so haijalishi mtu amekaa pale bungeni kwa muda gani, issue ni kwamba anatambua wajibu wake?
   
 19. Bob Lee Swagger

  Bob Lee Swagger JF-Expert Member

  #19
  Dec 14, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Najaribu kuangalia uwiano wa malipo ya 'wateule wetu' na wafanyakazi wengine wa umma...

  Daktari katika hospitali zetu za umma analipwa call allowance ya shilingi 10,000/= kwa masaa 12 au 24 anayofanya (masaa yanategemea na utaratibu wa hospitali) na tena basi, sehemu nyingine wanaikata kodi!

  Nimeambiwa barua ya kuongeza hiyo 'posho' kutoka 10 hadi 30 ilipigwa danadana hadi wakasahau! Kwa sasa haijulikani ilipo,so now hakuna mwongozo wa hayo malipo kwa sababu hakuna basis, kama kawaida mwajiri anafurahia hali kama hii, so wengi wanapewa 10 kwa sasa!

  Nadhani, ndiyo maana nasikia madokta wamekuwa wengi bungeni kwa sasa.
   
 20. King2

  King2 JF-Expert Member

  #20
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 1,289
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Anna Makinda ndio Tatizo!
   
Loading...